Baada ya Ardhi kuuza viwanja gezaulole, wahuni wanageuza jangwa kwa kukata Miti kwa kasi

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Hivi punde baada ya serikali kutangaza viwanja gezaulole - kigamboni na kulipa fidia wenyeji na wamiliki wa mashamba, sasa wahuni wamevamia na kukata miti kwa kasi ya ajabu manake wenyeji walishahama na kubomoa nyumba zao. Minazi wanaondoka nayo na miti mingine wanachoma mkaa, mnazi mmoja wenye umri zaidi ya miaka mitano wanauza kwa Tshs. 5,000.

Kama kuna waliopata fursa ya kuuziwa viwanja hivyo please nendeni makaone na kuokoa mandhari nzuri ya kigamboni, jamaa wanatumia chain saw yenye engine kudondosha miti fasta. Sijui wanapeleka wapi, barabarani wanaogopa lakini ukiingia ndani kidogo utaona kazi yao kama mafinga.
 
Back
Top Bottom