Baada ya Ajali.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,436
1,020
Mwendesha pikipiki mmoja alimgonga mwenda kwa miguu mmoja aliyekuwa kabeba mfuko wa rambo.Baada ya kufunga breki,mwendesha pikipiki aliangalia nyuma akamwona yule aliyemgonga kalala chini halafu utumbo umetapakaa barabarani.Jamaa akajua ameua,akaondoka kwa spidi kali kwenda kujisalimisha kituo cha polisi kuepukana na raia wenye hasira kali.Wakati akiendelea kujieleza kwa polisi wa zamu,mara akaja yule jamaa aliyegongwa akiwa na makovu kibao akasema;"masuala ya ajali ni ya kawaida tu,mi naomba anilipe kilo zangu mbili za utumbo wa ng'ombe zilizomwagika barabarani!"
 

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,030
dah! nilijuwa ni baada ya ajali kule visiOne umekuja na kinachoendelea! Ok, napita.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom