B Dozen conflict of interest

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Habari comrades.

Conflict of interest ni tukio ambolo taasisi ya jamii inapotumiwa kwa manufaa binafsi ya mwajiriwa wake. Kwenye hii mada taasisi ya jamii nayolenga ni kituo cha Radio Clouds FM na mwajiriwa wake anayeleta shida ni B Dozen al maruufu B Twangala, Hamisi Mandi na mengineyo. Hichi kituo cha radio kimekuwa pendwa kutokana na kuburudisha kutoka kwa burudani za wazawa na kuwa wabunifu katika vipindi vyake suala ambalo linakufanya unase na vipindi vyake ushindwe kujinasua kutokana na umahiri wa watangazaji wake. Mimi nimenaswa na kipindi cha XXL tokea miaka ya 2006 na rafiki zangu walinaswa na Loveness Love – Diva. Sasa kadiri miaka inavyoenda na mabadiliko yanatokea katika sekta ya mawasiliano nimeshudia rafu zikichezwa sasa haina budi niziseme.

XXL , kubwa kuliko ni kipindi maarufu kwa tasnia ya bongo flavor utaona jinsi wahisani walivyorundikana inaongozwa na B twelve ambako husindikizwa na watangazaji wenzake kennedy, Adam Mchomvu, Mamy Baby kwa sasa. Conflict of interest nazoziona kwa Mandi ni hizi

CLOUDS NA DOZEN SELECTION

Hapa bwana Mandi anacheza rafuu sana, kwanza huwa ana tabia ya kupandikiza story kutoka wa watangazaji wenzake ambako mwisho wa siku wakati unasubiri story imaliziwe utasika nenda kaingie Dozen Selection kwa story nzima, why yaani unaachwa juu juu kabla story haijafika mshindo sasa kama Clouds inavyojidai kwamba ni redio ya burudani ina jukumu la kutoa burudani hizi bure kwa sisi ndugu wasikilizaji. Mfano halisi ni hapa juzi tuu Ijumaa ambako kulikuwa na story juu ya Mabeste na mkewe kuachana ikaishia juju baada ya Dozen kusema story ipo kwenye YouTube channel yake ya Dozen Selection. Na nyingi tuu ameminya huyu mshikaji.

CLOUDS NA ADAMU MCHOMVU

Hii redio ilipaswa itoe chance kwa mziki bomba uweze pata airtime, na hiki kilio kinasikika sana kwa ngoma za Hip Hop. Lakini sasa bwana Mandi amekuwa na boriti jichoni mwake kwa kumbeba kulikopitiliza mshikaji wake, mtangazaji mwenzake bwana Adamu Mchomvu. Huyu jamaa kesi yake naweza sema ni special case kwani hii ni conflict of interest within conflict of interest ipo hivi.

Conflict within conflict of interest – hii kwanza ndani yupo adamu mchomvu mtangazaji mahiri mweje kipaji cha kuburidisha na kufurahisha kwa maneno yake. Sasa shida ni kamba bwana Adamu anatumia madaraka yake vibaya kama mtangazaji kwa kutangaza nyimbo zake na project zake, raia wanataka mziki mzuri na siyo nani kaimba.

Critic ya nyimbo za Adamu Mchomvu

Kwanza kwenye HIP HOP kitu kinachomata ni flow of rhyme tumesikia mc kibao wakijinadi they have sick flow lakini kwa ndugu yetu Adamu Mchonvu hana flow kabisa kama wajua rap waweza LIA MACHOZI kwa kumsikiliza Adamu akiwa anarapu ni anaongea kabisa yaani na miaka yote ambayo amekuwa aki-practise bado.

Hajaweza kabisa kuflow. Ni jambo LA KUSIKITISHA SANA. Na nadhani hii shida ni kutokana na kusoma vi-quote vya Instagram pasipo kumalizia sentence yote kwamba follow dreams. Na katka watu ninaohisi wana stress, huyu mwana ni mmoja wapo, kwani anaimba madudu kabisa nadhani ata rohoni kwake atakuwa anajua.

Haki ya nani nyani haoni kundule. Ndugu Adamu Ijumaa hii ya tar 17 mwezi Januari anajisifu kwa kufanya ndani ya siku track yake. It very depressing na kumbe wameshakubaliana na bwana Mandi kwamba mwaka mzima kila mwezi anadodosha ngoma yaani .

Kwa utumbo anaoimba na very very bad flow anataka kila mwezi kutuhuzunisha Zaidi wapenzi wa rap . Waweza sema anatumwa na watu kutunyanyasa burudani huyu mwana.

Adamu acha kuimba unabomoa badala ya kujenga na kama ulibahatika kusikiliza XXL ya Ijumaa DIVA akampiga dongo kwamba siyo wote waimbe, wengine wawezeshe nyimbo kali zifanyike (DIVA ana bonge la ngoma ali-introduce feature Brick n Lace na dogo mmoja wa King Music. Lakini ajabu naye Diva kamuiba dogo kwa King Music bila maafikiano mazuri, sijui wana nini hawa watu wa Clouds.

Bwana mandi anaingia kwenye hii conflict kutokana na konekana wazi anampendelea mwenzake kwa kumpatia muda bwana mchomvu mandi acha mchezo wako huu. Mchovu akilalamika mwambie hana reiver nzuri ya kupokea mistari kwenzi aache watu natural wafanye mambo ya maana kama kina Ngwair.

Simamia burudani kwani kwa maaisha ya sasa ndio kitu pekee kilichobaki kwa wananchi ingawa njia nyingi zinafungwa za wananchi kupata burudani (VIBANDO VYA GHARAMA) simamia burudani ili wanainch wapooze moyo kwa kuvumilia mengi yanayoendelea sasa na kama kwenye burudani mkaharibu itatia huruma sana hata wa-South Africa waliachiwa mziki mzuri kipindi cha ubaguzi.

B Dozen SOMA HIYOOO!
 
Na ndio maana watangazaji wa Clouds huwa nawaona kama wana amani na furaha sana kufanya kazi pale tofauti na media zingine.

Kila mtangazaji utakuta ana promote brand au biashara yake kupitia hiyo platform.
 
Umejuaje afanyi kazi? Na vp kama anafanyakazi na kazi yake inamruhusu kusikiliza redio? Acha ushamba kufanyakazi hakuhusiani na kusikiliza redio, Nandugu yangu Dr na kazini kwake anaredio anasikiliza kila siku.
Inaonekana huna kazi ya kufanya zaidi ya kusikiliza radio tu. Fanyeni kazi vijana radio uwe unasikiliza kama bahati mbaya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....radio za burudani zipo kibao, ukikelwa na radio hi..una tune nyngn kiroho xf (hamna kutexeka)
 
Inaonekana huna kazi ya kufanya zaidi ya kusikiliza radio tu. Fanyeni kazi vijana radio uwe unasikiliza kama bahati mbaya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo starehe yake, au wewe inakukera!? Hivi mfano, mimi ni muuza duka, kuna tatizo nikisikiliza redio wakati niko kazini wakati kazi yangu inaniruhusu kufanya hivyo!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom