B boyfriend nije kukutembelea kama nani wako?

B boyfriend nije kukutembelea kama nani wako?

Ata msomane miaka yote ya maisha yenu, kama mkishindwana mnashindwana tu kwani tabia ya mtu ni maandiko isiweze badilika?
Si ndo maana yake msomane! Mkishindwana mapema sepa! Ukikubari mkafungwa pingu nakuambia hiyo pingu haina ufungua kama ya polisi! Pingu ya ndoa ufunguo ni kifo! Na hilo haijarishi ni dini gani! Tunaongelea uhalisia baada ya kufunga pingu za maisha na mtu alafu unachekelea kutengana! Angalia maisha yako baada ya kutengana na kabla ya kufunga ndoa! Unakuwa umebadilishwa kuanzia jamii ndugu marafiki kifikra economic, etc.
 
Unaweza pata kabla hujamaliza kuweka stori, wahuni wamepita na simu yako
Hii post inanikumbusha jamaa aliyeimbisha mtoto kama miezi sita. Siku ya siku muhuni yupo kwenye daladala msg inaingia. Nimekubali ombi lako, nije saa ngapi kwako tuyajenge? Jamaa akajibu njoo saa kumi jioni ntakuwepo. Basi kabla hajatuma kibaka akakwapua simu. Muhuni ilibidi atoe kichwa dirishani akamwambia we kibaka bonyeza sendi. Bonyeza sendi weweweeeeeee
 
JF is never boring
 
Huyu binti wa rafiki yangu anaitwa Shangwe. Shangwe ni binti anaevutia sana. Amemaliza kidato cha sita ingawa matokeo yake hayakuwa mazuri sana. Wakati wazazi wanafikiria cha kufamfanyia binti yao kwa maisha yake Shangwe alikutana na Dickson wakiwa kanisani. Dickson alimuelewa sana Shangwe.

Dickson alipata nafasi ya kwenda kusoma South Africa, akisomeshwa na kampuni. Baada ya kukaa miezi miwili huko Sauzi alimtumia Shangwe ticket apande pipa kwenda kuvinjari.

Shangwe alipotapa ticket alimuuliza Dickson nitawaaga wazazi wangu kuwa ninakwenda wapi na kwa nani? Mimi ninakuja kukutembelea kama nani?

Dickson alimuuliza nikituma ndugu walete barua ya posa kwenu itakuwaje?

Hivi ndivyo Shangwe alivyopata mume.
Kwa hiyo mkuu hapa moral ya hadithi yako ni nini? Ama unamwombea bi Shangwe ushauri?
 
Wasichana wasijirahisishe sana kutoa vitu vyao.
Labda wasichana wa kijijini kwenu mkuu ila Neema alimsindikiza boyfriend wa mama yake ambaye yeye alikuwa akimuita Uncle, basi siku hiyo hiyo ndo alitoa mzigo na maisha yakaendelea...hivi sasa Neema ndo mama lao na mama yake kabaki kuwa mchepuko,muhimu jamaa anatoa matunzo kwa wote na maisha yanaendelea.
 
Hizi ndoa za voda faster hata mwaka hauishi wanarudi hapa wanalia! Jamani nyie vijana mnaotaka kuoana pateni muda wa kusomana nyie pia na familia zenu kabla ndoa. Ndoa ni ngumu na nikifungo cha maisha. Ukitaka kuondoka kinakuchana personality yako hata ukijimwambafai but you will never be the same again! Don't mess up with marriage!
Ni kweli kabisa, ndoa haiitaji kukurupukia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu kwa andiko mwanana.

Hayo maswali niliwahi kuwatandika 'wakwilima' kupelekea kuwalamba 'masumule'(fine).

'Process' za ndoa za kiAfrika na kibantu ni mvulana kumpenda msichana na kutangaza nia yake kwa mlengwa, akiisha kubaliwa hutuma mshenga akiwa na barua ya posa.

Posa likishakupokelewa, taratibu za mahari na kutangaza ndoa kunafuata, baadaye harusi.
Hakuna muda wa kusubiri tena kwa kisingizio chochote.

Haya mambo ya uzungu kwenda kutambulishana ukweni, yatupasa kujiuliza yafuayayo:

Mlienda ukweni mkiwa kama nani?

Maana cheo cha uchumba huanza baada ya mahari kupokelewa na harakati za harusi kuanza.

Maana ni marufuku kwa wachumba kusogeleana kwa vyovyote hadi ndoa!

Mkifika huko mnalala wapi kwanza, separated rooms au mlala pa1?

Ujue thamani ya binti ni kutoguswa kwa vyovyote na huyo mchumbaake, akishatumika kutathiminiana huanza kichwani mwao hasa kikubwa ni madhaifu ya kitanda na la pili kupimana maongezi!

Ugumu wa msichana kutochezewa kwa ulaghai wwoote toka kwa mchumba, humpandisha thamani, pia huongeza 'muhu' wa mwanaume kutolala usingizi akiwaza kummiliki huyo ampendaye kwa dhati.

Mvulana(mchumba) huyo hujinyima hata saazingine kulala na njaa ili aweze kutimiza tu lengo lake hilo la kuoa.

Msichana ukiisha kujigawa kiurahisirahisi kwa mwananaume mwenye malengo na wewe, basi automatic 'kani' ya lengo hupungua na kulifanya jambo hilo kuwa la kawaida sana na lisilokuwa na uharaka wowote katika utekelezaji wake.

Hata muoaji speed ya kuoa hupungua kwani anapata vyote anavyohitaji kutoka kwa binti. Wengine wanafua, kupiga pasi, kupika na kusafisha nyumba.

Ukishamfanyia mwanaume haya yote unamuweka kwenye comfort zone.
 
Hizi ndoa za voda faster hata mwaka hauishi wanarudi hapa wanalia! Jamani nyie vijana mnaotaka kuoana pateni muda wa kusomana nyie pia na familia zenu kabla ndoa. Ndoa ni ngumu na nikifungo cha maisha. Ukitaka kuondoka kinakuchana personality yako hata ukijimwambafai but you will never be the same again! Don't mess up with marriage!
Marriage is the most legally significant thing you will ever do apart from death.

Vijana tuache ujinga.

Usioe kizembe.
 
Hata muoaji speed ya kuoa hupungua kwani anapata vyote anavyohitaji kutoka kwa binti. Wengine wanafua, kupiga pasi, kupika na kusafisha nyumba.

Ukishamfanyia mwanaume haya yote unamuweka kwenye comfort zone.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji106][emoji106][emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata muoaji speed ya kuoa hupungua kwani anapata vyote anavyohitaji kutoka kwa binti. Wengine wanafua, kupiga pasi, kupika na kusafisha nyumba.

Ukishamfanyia mwanaume haya yote unamuweka kwenye comfort zone.
La muhimu zaidi 'usimpe'.

Hapo ndipo utakapozielewa mbivu na mbichi, lengo la kweli hapo ndiyo hujionesha dhahiri.

Me mwenyewe nilifanyiwa hivyo.
Pamoja na ujanja wangu na mbinu zangu zaidi ya 100 za kulaghai na kunasa mabinti, lakini nilikwamishwa kishenzi na wakwe.

Baada ya uchumba nikatumia mbinu ya kwenda kwa wazazi kumuomba nimchukue kwenda naye mjini kumnunulia zawadi na mahitaji mbalimbali mchumba wangu.

Ebanaeeh! Ile familia juwaji wacha!

Huo mchezo ulinitia hasara kwenye bajeti zangu bila kufanikisha nilichokilenga.

Nilipofika kutoa ombi hilo nikaelezwa na baba mkwe: 'baba tunakukabidhi binti yetu mwende naye kama ulivyoomba, lakini usirogwe kumfanyia kinyume chochote cha maadili.

Kitendo hicho kitavuruga ndoto yako uliyoidhamiria na gharama za mahari utakuwa umeitupa bure, hakuna atakaye kufidia.

Maelezo yalikuwa ni mengi mno, pia katika msafara huo akachomekwa na kaka mtu tuambatane naye safari yetu yote.

Hila yangu ikantia hasara, maana nikajifaragua kununua zawadi, ikaenda bure kitendo!

Mwewe kukosa mawindo na kushindwa kuambulia hata majani, kulinipa mori ya kumuoa huyo binti hata kwa dharula sasa, huku nikijiapiza moyoni....' ndhza! Akiyamungu siku yaarusi ntamkeshea niuone ujanja wao, yaani mimi wa kunidhibiti kwa mchumba wangu niliyemtolea na mahari, wewe ngojaaa!'.....

Nikawa nimejifunza ambavyo mwanaume ukichekewa, wazazi wa msichana 'wataambulia mabua'.

Kwenye 'season' ya uchumba mwanaume hatakiwi kupewa huduma yoyote toka kwa msichana kama ulivyosema sky, ikiwezekana hata tabasamu anyimwe ili aharakishe mipango yake, kama cheko na tabasamu akavipate hukohuko mbele kwa mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom