sidhani kama hii peke yake inatosha kuwa sababu; maana tukifuata yanayofanywa na nchi nyingine "zinazokwenda na wakati" tunaweza kufuata mambo mengi kweli. Kuna mambo ambayo sisi wenyewe ni lazima tuyafikiri na kuyaamua kwa nia yetu sisi wenyewe.
Lakini kwenye suala la UN2 hatuwezi tu kutoka na kusema every one go!! hakuna sehemu duniani ambao wamefanya hivyo, kila watu wana utaratibu wao na sababu zao. Sisi wa kwetu uweje? hilo ndilo swali au hutaki hata tufikirie tufanye vipi turuhusu tu alimradi tumeruhusu bila kufikilia masuala mbalimbali?
sidhani kama hii peke yake inatosha kuwa sababu; maana tukifuata yanayofanywa na nchi nyingine "zinazokwenda na wakati" tunaweza kufuata mambo mengi kweli. Kuna mambo ambayo sisi wenyewe ni lazima tuyafikiri na kuyaamua kwa nia yetu sisi wenyewe.
Lakini kwenye suala la UN2 hatuwezi tu kutoka na kusema every one go!! hakuna sehemu duniani ambao wamefanya hivyo, kila watu wana utaratibu wao na sababu zao. Sisi wa kwetu uweje? hilo ndilo swali au hutaki hata tufikirie tufanye vipi turuhusu tu alimradi tumeruhusu bila kufikilia masuala mbalimbali?
Nyie mnashangaa hili
Mbona tuna waziri wa Fedha ambaye ana degree feki?
sasa ipi sensitive btn the two?
Duh! Bubu nchi ulizozitaja walikua na sababu zao za kuruhusu. TZ kwa sasa hatuna sababu izo.Nchi aiendeshwi kwa kufanya kila jambo linalofanywa na jirani.Nina wasiwasi utakuja sema Rwanda, Burundi, Uganda walishapigana wao kwa wao sijui TZ tunangoja nini!
Anakuja lini, tarehe kama unafahamu?Membe atakuwa London kwenye mkutano wa diaspora wiki chahce zijazo.Nadhani itakuwa fursa nzuri akiulizwa kuhusu huo mchakato usio na mwisho about dual citizenship.
Sawa lakini hao si "Halali" Kisheria,si raia wa Tanzania.
Ni kwa sababu ya Tanzania kutokua na data base ya wananchi wake! Najua hili si tatizo la Tanzania peke yake, lipo na nchi zingine, lakini haina maana kuwa ni sawa.
Serikali ingeweza kuanza tu kwa kuingiza kwenye data base wananchi wote wenye hati za kusafiria na hiyo data base iwe updated mara kwa mara (si kama website zao!)
Basi tunaonekana wajiiinga! Aibu!
Marehemu Barbara Johansson aliwahi kuwa balozi wetu Sweden/Mbunge wa kuteuliwa wakati akiwa Mswidi/Mtanzania
Huyo mama alikuwa lini balozi wetu Stockholm? Hii hapa orodha ya waliowahi kuwa mabalozi Stockholm. Tuoneane huruma wakati mwingine.
Amandla.........
- Vacant Oct. 2008- Todate
- H.E. Dr. Ben Moses2005-2008
- H.E. James L. Kateka 1998-2005
- H.E. Wilson K. Tibaijuka 1994-1998
- H.E. Mohamed Ramia Abdiwawa 1990-1994
- H.E. Daniel N. Mloka1983-1989
- H.E. J.F. Edward Mhina 1977-1983
- H.E. Chief Michael Lukumbuzya 1969-1977
- H.E. Philemon Muro 1964-1969
Julius.. usielewe vibaya mkuu. Binafsi sina tatizo kabisa na kuruhusu Watanzania kuweza kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja (sielewi kwanini lazima uwe wa nchi mbili tu!) lakini kama unavyosema lazima tuweke wazi exceptions kwa sababu.. nakumbuka Fujimori kilipomuungulia kule Peru akakimbia nchi ya asili ya wazazi wake (Japani!) akidai uraia wa kule.
Sheria ipi ambayo wewe unasema? Mbona wanaingia Tanzania na kutoka bila kuchukuliwa hatua kama watanzania? Hizi sheria ambazo hazifanyi kazi ndio unazipigia debe? Sheria ambayo haifanyi kazi ina maana gani?
Wala sio mmoja tu. Tunao wengi tu. Na wabunge ndio usiseme kabisa. Na huko kwenye taasisi zingine ndio wamejaa kibao. Ukweli ni kwamba hakuna cha kushangaza hapa.
Naamini wote (kwa kiasi kikubwa) tunakubaliana kuwa kuruhusu wananchi kuwa na uwezekano wa uraia zaidi ya mmoja siyo jambo baya kwa kipimo chochote. Naamini mgogoro unakuja kwenye kanuni za kuruhusu jambo hilo. Kusema tu kuwa kutakufa na faida za kiuchumi kama wengi wanavyojenga hoja sidhani kama inatosha.