Azimio la Tabora: Hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe

Azimio la Tabora: Hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe

Haters gonna hate mkuuu....But ukweli unabakia pale pale hakuna mwanasiasa mwenye akili nzuri kama Zitto Tanzania hii

Haya ndio maneno ya Zitto. Kwake kila jambo zuri ni yeye pekee analo au amefanya. Ubinafsi wa hali ya juu
 
Zitto Kabwe haaminiki tena. Hiyo ndio sababu kubwa ya kukataliwa. Tabia za usaliti, umbeya, kutaka kuishi maisha ya kifahari kwa kutegemea Hongo.
 
Nenda kwa waandishi wakusaidie hicho kitendo cha kuweka kabla hujahutubia unawasaidia waandishi kuweza fanya kazi kuchambua, kukosea na kuhariri badala akae anasikia hotuba unampa nafasi ya kuchukua habari nyingine je hotuba imewagusaaje watu na sio na yeye awe busy kusikia hotuba hiyo
 
Zitto Kabwe haaminiki tena. Hiyo ndio sababu kubwa ya kukataliwa. Tabia za usaliti, umbeya, kutaka kuishi maisha ya kifahari kwa kutegemea Hongo.

Sema simuamini, ama namkataaa.....usisemee na wengine ambao jana walijitokeza kwa wingi kumsikiliza.
 

Attachments

  • 1434270122152.jpg
    1434270122152.jpg
    69 KB · Views: 103
Mkuu salama? Kaka una shingo ngumu!! Bado tu unamhusudu huyu tapeli wa Kazuramimba na Buzebazeba?

Salama salmin mkuu Mzito Kabwela.......mkuu mimi sio fuata upepo navutiwa na itikadi ya ACT-Wazalendo.....sio lazima wote tuwe makamanda....ninachojua na kuamini kabisa ni kuwa naichukia CCM kwa dhati.
 
Last edited by a moderator:
Salama salmin mkuu Mzito Kabwela.......mkuu mimi sio fuata upepo navutiwa na itikadi ya ACT-Wazalendo.....sio lazima wote tuwe makamanda....ninachojua na kuamini kabisa ni kuwa naichukia CCM kwa dhati.

Mkuu kwahiyo ACT mkishika dola mtalifanya taifa kuwa na itikadi ya ujamaa kama azimio lenu la Tabora linavyosema?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwahiyo ACT mkishika dola mtalifanya taifa kuwa na itikadi ya ujamaa kama azimio lenu la Tabora linavyosema?

Ujamaa wa kidemokrasia.....mrengo kati kushoto...njia kuu za uchumi kumilikiwa na wananchi wenyewe....pia ujamaa huu unahusisha soko mkuu...naamini ACT wakishika dola watatekeleza hili....tofauti kati ya walionacho na wasionacho ni kubwa sana ndo maana utu na usawa vimepungua hapa nchini....ubepari unazidisha hali hii mkuu naamini hivyo.
 
Nyepesi so angejiunga CCM kabisa tukajua moja moja kuliko kuingia gharama zoote hizi za kisiasa ya kuanzisha chama kwingine ndani ya chama kile kile mambo Yale Yale maazimio Yale yale
 
Thread ipo hapa toka jana na sasa ni page ya sita tu na anayechangia sana ni mleta mada, tunajifunza nini?
Huku ndio kuchuja kwa Zitto.
 
Zitto Kabwe
# AzimioLaTabora Hotuba yangu leo
Mnamo 26 Januari 1967 saa tano na robo
asubuhi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais
wa chama cha TANU alifungua mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Mkutano huu ndio uliozaa Azimio la Arusha
lililoiweka nchi kwenye reli ya kujenga Taifa la
kijamaa, lenye usawa na lisilo la kinyonyaji.
Katika hotuba yake ya ufunguzi Mwalimu Nyerere
alisema “….. Mkutano wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ulikuwa umepangwa ufanyike mjini Tabora
…. Kama Mwenyekiti, naomba radhi viongozi
pamoja na wanachama wa Tabora kwa vile
mkutano huu haukufanyika mjini Tabora kama
ilivyokusudiwa hapo mwanzoni”.
Kumbukumbu za mkutano huo zinaendelea
kumnukuu Mwalimu Nyerere akisema “ Mnamo
mwaka 1958, mwezi January kama huu, Chama
chetu kilifanya mkutano mkubwa mjini Tabora.
Kusema kweli, kama Mkutano huu ungefanywa
tena pale, Tabora ingekuwa na Historia kubwa
sana. Ilikuwa mwezi wa January 1958, baada ya
kuendelea na Chama chetu kwa muda wa miaka
mine tuliona ni heri kutoa tamshi la kutikisa
nchi”.
Leo tupo Tabora kurejesha nafasi ya Tabora
katika historia ya nchi yetu. Leo tunazindua
Azimio la Tabora kama ilivyokuwa imekusudiwa
hapo awali. Leo tunahuisha Azimio la Arusha kwa
kufuata nyayo za maamuzi ya busara ya Tabora
ya mwaka 1958. Leo tunatoa tamshi la kutikisa
nchi. Tunataka kurudi kwenye Ujamaa.
Wananchi wa Tabora, ndugu Watanzania nchi
yetu inakabiliana na changamoto kubwa nne;
Uchumi usiozalisha ajira na kutoondoa umasikini
Huduma duni za jamii hususan Elimu, Afya na
Maji
Rushwa na Ufisadi
Nyufa katika Taifa kutokana na hisia za udini na
ukabila kuanza kushamiri
Mwaka 1967 nchi yetu ilikuwa inakabiliwa na
changamoto hizi hizi isipokuwa changamoto ya
rushwa na ufisadi ilikuwa ndio imeanza
kuchomoza. Waasisi walianzisha Azimio la Arusha
ili kwanza kuwa na mwongozo wa kutekeleza
shabaha ya kujenga Taifa lisilo la kinyonyaji na
pili kuweka itikadi ya kitaifa ili kujenga Taifa moja
lisilo na itikadi za kidini na kikabila. Tamko la
Arusha na Azimio la Arusha (ambavyo tumekuwa
tukiita vyote AZIMIO) liliweka Miiko ya Viongozi ili
kukabiliana na Ufisadi. Ndio maana kipindi chote
cha uhai wa Azimio la Arusha hapakuwa na
ufisadi. Rushwa ilikuwapo, ilidhibitiwa kwa mujibu
wa sheria mbalimbali. Ulimbikizaji wa mali
unaotokana na ufisadi haikuwezekana wakati huo
kwa sababu Miiko ilikuwa ni kizuizi kikubwa.
Kwa takribani miaka 25 nchi yetu ilitekeleza
Azimio la Arusha. Nchi yetu ilianza kujenga
uchumi wa kijamaa na kujenga Taifa lenye usawa
na lisilo la kinyonyaji, Taifa lisilo na ubaguzi wa
aina yeyote. Taifa lililopiga vita udini na ukabila.
Ili kumilikisha uchumi kwa wananchi, Serikali
ilitaifisha mabenki, migodi, kampuni za bima na
biashara nyingine mbalimbali za ndani na
biashara ya nje. Katika kipindi hiki pia Serikali
ilijenga viwanda mbalimbali hususan viwanda vya
kuongeza thamani ya Mazao yetu kilimo kama
vile viwanda vya nguo ikiwemo viwanda vya
kuchambua pamba, viwanda vya nyuzi na nguo.
Jumla ya viwanda 12 vya nguo vilijengwa nchini
na kuzalisha maelfu ya ajira kwa wananchi.
Serikali pia ilianzisha viwanda vya ngozi, vya
kubangua korosho, vya kuzalisha sukari, vya
kubangua na kusaga kahawa, vya kamba za
katani na magunia ya katani na kadhalika.
Serikali pia ilijenga viwanda vikubwa 2 vya
kutengeneza vipuri. Kimsingi mpaka mwaka 1978,
kabla tu ya vita vya Kagera, nchi yetu ilikuwa
katika hatua ya ‘take-off’ kama wachumi
tunavyoita. Waasisi wetu wa Taifa walitaka
kuondokana na uchumi wa kuzalisha malighafi tu.
Yote haya tuliyafanya kwa pamoja kama Taifa
ama kwa kutumia fedha zetu wenyewe za kodi au
kwa kutumia mikopo na misaada kutoka nje. Hata
hivyo, baada ya vita vya Kagera uchumi wetu
ulianza kuporomoka na nchi yetu kulazimishwa
kufuata masharti ya Shirika la Fedha la Dunia
(IMF) na Benki ya Dunia.
Mwaka 1750 mchumi wa kijerumani Johann
Heinrich Gottob von Justi aliandika “ nchi zote
zinazolazimishwa kuzalisha malighafi tu zitaelewa
kuwa zilikuwa zinawekwa kwenye umasikini wa
kudumu”. Wakati shabaha ya Azimio la Arusha
ilikuwa ni kuodokana na onyo hili la mchumi
Gottob von Justi, kuanzia mwaka 1992 Tanzania
ilianza kuvunjavunja misingi ya Azimio la Arusha
na kurudi miaka 25 nyuma. Kimsingi uvunjaji
ulianza kidogo kidogo kuanzia mwaka 1986 na
ndio maana mwaka 1987 hapakuwa na tathmini
iliyowazi ya Azimio kama ilivyokuwa mwaka
1977. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mwaka
2017 tunaadhimisha miaka 50 ya Azimio la
Arusha kwa kufanya tathmini ya miaka 25 ya
utekelezaji wa Azimio na Miaka 25 ya kutupwa
kwa Azimio. Chama cha ACT Wazalendo kinaanza
mchakato huo sasa kwa kutangaza Azimio la
Tabora linalohuisha Azimio la Arusha.
Kuanzia mwaka 1996 tulianza kuona viwanda
vyote tulivyojenga kwa pamoja vikibinafsishwa na
kupewa watu wachache na wengi wageni.
Tulianza kuona mabenki tuliyomiliki wote kama
Taifa yakiuzwa kwa bei ya kutupwa. Kimsingi
ubinafsishaji sio tu ulikuwa ni ugenishaji wa
uchumi wetu bali ulikuwa ni ‘deindustrialisation’.
Leo hii hakuna hata kiwanda kimoja cha Korosho
kinafanya kazi licha ya kubinafsishwa, lakini
Watanzania wote bado wanalipa madeni ya
kujenga viwanda hivyo maana tulijenga kwa
mikopo. Hali ni kama hiyo kwa viwanda vya nguo
ikiwemo ‘ginneries’ mbalimbali. Badala ya
kufanya vile mataifa mengine yalifanya ili kupata
maendeleo, sisi tuliamua kufanya tunachoambiwa
kufanya. Tulisahau msemo wa kizungu “ Don’t do
as the English tell you to do, do as the English
did”. Ni watu wachache wanajua kuwa nchi kama
Norway ilipiga marufuku nguo kutoka nje mpaka
miaka ya mwisho ya hamsini. Hata kuagiza gari
binafsi ilikuwa ni mafuruku nchini Norway katika
hatua zake za mwanzo za kujenga uchumi wao.
Leo Norway ni nchi ya kupigiwa mfano kutokana
na usimamizi wa rasilimali zao. Tufanye
walivyofanya, tusifanye tunavyoambiwa tufanye.
Wananchi, tulijaribu Azimio kwa miaka 25 na
kufanikiwa kujenga Taifa moja lenye viwanda
licha ya changamoto za ki uendeshaji
tulizokumbana nazo. Tumejaribu sera za kiliberali
kwa takribani miaka hiyo hiyo na kufanikiwa
kujenga Taifa lenye nyufa nyingi na matabaka ya
walionacho na wasio nacho. Sasa ni wakati wa
kurudi kwenye misingi kwa kurekebisha makosa
ya miaka 25 ya Ujamaa na kuchukua mafanikio
ya miaka 23 ya uliberali na demokrasia na hivyo
kuanza mchakato wa kujenga Taifa la Ujamaa wa
KiDemokrasia. Tabora ndio kitovu cha historia ya
nchi yetu na ndio maana tuliamua kuja Tabora
kufanya kazi hii ya kihistoria. Lazima kufanya
maamuzi ya busara.
Wananchi, Wazee wetu walikutana katika ukumbi
tuliokutana sisi leo mwaka 1958 ili kufanya
maamuzi kuhusu hatma ya uhuru wa nchi yetu.
Wakati huo uhuru uliokuwa unatafutwa ni uhuru
wa kisiasa. Walifanya Uamuzi wa Busara. Uamuzi
wa Busara wa Tabora wa TANU wa mwaka 1958
ulijibu changamoto ya kuharakisha Uhuru wa
Tanganyika kwa kukubali uchaguzi wa kura tatu.
Uamuzi wa Busara wa Tabora wa mwaka 2015
unataka kujibu changamoto ya kurudisha utaifa
wetu kwa kuhuisha Azimio la Arusha na hivyo
kushawishi kubadili sera zetu za kiuchumi kwa
shabaha ya kumilikisha uchumi kwa wananchi
wenyewe.
Tumeeleza hapo awali kuhusu changamoto za
nchi yetu. Kwanza hatuna budi kuhuisha Azimio la
Arusha ili kurejesha itikadi moja ya kitaifa
inayotuunganisha na kuziba nyufa za udini na
ukabila ambazo zinashamiri katika nchi yetu hivi
sasa. Tunaanza kuona viongozi wa dini
wakichukua nafasi kubwa kwenye siasa hivi sasa
kwa sababu hakuna itikadi ya kitaifa. Kuna
ombwe na asili haipendi ombwe ( nature abhors
vacuum). ACT Wazelendo ina imani kwamba
lazima kurudi kwenye misingi ili kuepusha nchi
kusambaratika. Udini na Ukabila utafutika
kutokana na kuwapo kwa Itikadi ya kitaifa kwani
Udini ni itikadi na Ukabila ni itikadi.
Pili, tuna uchumi unaojenga Matabaka. Hivi sasa
uchumi wetu umeshikwa na watu wachache
hususan wafanyabiashara ambao pia wameshika
siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja
kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea
maslahi yao. Azimio la Tabora linahuisha Azimio
la Arusha kwa kurudi kwenye uchumi wa Ujamaa
wa kisasa utakaojikita katika kuongeza uzalishaji
mali na ugawaji sawa wa keki ya Taifa na hivyo
kupunguza matabaka nchini kwetu.
Tatu, tuna changamoto ya huduma za kijamii
hasa afya na elimu ambapo hivi sasa huduma hizi
zimekuwa kwa matabaka. Wenye uwezo kifedha
wana shule zao na hospitali zao na masikini wana
shule zao dhaifu na hospitali duni. Tunahuisha
Azimio la Arusha ili kurejesha muundo wa utoaji
huduma muhimu kama Afya na Elimu kwa
kuhakikisha kuwa shule za umma na hospitali za
umma zinakuwa ni bora zaidi.
Nne, tuna kansa ya ufisadi ambapo watu hutumia
nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali. Ufisadi
ni tatizo zaidi la viongozi walioshika madaraka ya
umma. Tunahuisha Azimio kwa lengo la kusimika
miiko ya Uongozi wa Umma ambayo itakuwa
msingi mkuu wa mapambano dhidi ya ufisadi.
Wananchi, leo tunafanya yale waasisi wa Taifa
letu walitaka tufanye ya kuhakikisha misingi ya
nchi yetu inarejeshwa. Leo tunaanza kazi hiyo
ambayo inaweza kuchukua muda mrefu kufikia
malengo yetu. Inawezekana malengo yakafikiwa
na watoto wetu au wajukuu zetu lakini ni lazima
kazi hii ifanyike. Ndio maana tumekuja kuanzia
Tabora, mahala ambapo wazee wetu waliamua
kuharakisha Uhuru wa nchi yetu. Uamuzi wa
Busara wa Tabora ni nguzo ya Azimio la Tabora
linalohuisha Azimio la Arusha. Tunaanzia hapa
kuirudisha nchi yetu kwenye misingi na
kumilikisha uchumi kwa wananchi.
 
ZZK amejifanya kuleta ubunifu mpya kwa kutofautiana na wengine cha ajabu amejikuta kituko, ametaka kutofautiana na wengine na amejikuta hata yeye mwenyewe ni msaliti kwani maneno na matendo yake yanaonesha utofauti mkubwa
 
Unatujazia uchafu, mod please destiny this to the garbage bin
 
Back
Top Bottom