mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,548
Mnamo 26 Januari 1967 saa tano na robo asubuhi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa chama cha TANU alifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho. Mkutano huu ndio uliozaa Azimio la Arusha lililoiweka nchi kwenye reli ya kujenga Taifa la kijamaa, lenye usawa na lisilo la kinyonyaji. Katika hotuba yake ya ufunguzi Mwalimu Nyerere alisema
.. Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ulikuwa umepangwa ufanyike mjini Tabora
. Kama Mwenyekiti, naomba radhi viongozi pamoja na wanachama wa Tabora kwa vile mkutano huu haukufanyika mjini Tabora kama ilivyokusudiwa hapo mwanzoni.
Kumbukumbu za mkutano huo zinaendelea kumnukuu Mwalimu Nyerere akisema Mnamo mwaka 1958, mwezi January kama huu, Chama chetu kilifanya mkutano mkubwa mjini Tabora. Kusema kweli, kama Mkutano huu ungefanywa tena pale, Tabora ingekuwa na Historia kubwa sana. Ilikuwa mwezi wa January 1958, baada ya kuendelea na Chama chetu kwa muda wa miaka mine tuliona ni heri kutoa tamshi la kutikisa nchi.
Leo tupo Tabora kurejesha nafasi ya Tabora katika historia ya nchi yetu. Leo tunazindua Azimio la Tabora kama ilivyokuwa imekusudiwa hapo awali. Leo tunahuisha Azimio la Arusha kwa kufuata nyayo za maamuzi ya busara ya Tabora ya mwaka 1958. Leo tunatoa tamshi la kutikisa nchi. Tunataka kurudi kwenye Ujamaa.
Wananchi wa Tabora, ndugu Watanzania nchi yetu inakabiliana na changamoto kubwa nne;
Uchumi usiozalisha ajira na kutoondoa umasikini
Huduma duni za jamii hususan Elimu, Afya na Maji
Rushwa na Ufisadi
Nyufa katika Taifa kutokana na hisia za udini na ukabila kuanza kushamiri
Mwaka 1967 nchi yetu ilikuwa inakabiliwa na changamoto hizi hizi isipokuwa changamoto ya rushwa na ufisadi ilikuwa ndio imeanza kuchomoza. Waasisi walianzisha Azimio la Arusha ili kwanza kuwa na mwongozo wa kutekeleza shabaha ya kujenga Taifa lisilo la kinyonyaji na pili kuweka itikadi ya kitaifa ili kujenga Taifa moja lisilo na itikadi za kidini na kikabila. Tamko la Arusha na Azimio la Arusha (ambavyo tumekuwa tukiita vyote AZIMIO) liliweka Miiko ya Viongozi ili kukabiliana na Ufisadi. Ndio maana kipindi chote cha uhai wa Azimio la Arusha hapakuwa na ufisadi. Rushwa ilikuwapo, ilidhibitiwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali. Ulimbikizaji wa mali unaotokana na ufisadi haikuwezekana wakati huo kwa sababu Miiko ilikuwa ni kizuizi kikubwa.
Kwa takribani miaka 25 nchi yetu ilitekeleza Azimio la Arusha. Nchi yetu ilianza kujenga uchumi wa kijamaa na kujenga Taifa lenye usawa na lisilo la kinyonyaji, Taifa lisilo na ubaguzi wa aina yeyote. Taifa lililopiga vita udini na ukabila. Ili kumilikisha uchumi kwa wananchi, Serikali ilitaifisha mabenki, migodi, kampuni za bima na biashara nyingine mbalimbali za ndani na biashara ya nje. Katika kipindi hiki pia Serikali ilijenga viwanda mbalimbali hususan viwanda vya kuongeza thamani ya Mazao yetu kilimo kama vile viwanda vya nguo ikiwemo viwanda vya kuchambua pamba, viwanda vya nyuzi na nguo. Jumla ya viwanda 12 vya nguo vilijengwa nchini na kuzalisha maelfu ya ajira kwa wananchi. Serikali pia ilianzisha viwanda vya ngozi, vya kubangua korosho, vya kuzalisha sukari, vya kubangua na kusaga kahawa, vya kamba za katani na magunia ya katani na kadhalika. Serikali pia ilijenga viwanda vikubwa 2 vya kutengeneza vipuri. Kimsingi mpaka mwaka 1978, kabla tu ya vita vya Kagera, nchi yetu ilikuwa katika hatua ya take-off kama wachumi tunavyoita. Waasisi wetu wa Taifa walitaka kuondokana na uchumi wa kuzalisha malighafi tu.
Yote haya tuliyafanya kwa pamoja kama Taifa ama kwa kutumia fedha zetu wenyewe za kodi au kwa kutumia mikopo na misaada kutoka nje. Hata hivyo, baada ya vita vya Kagera uchumi wetu ulianza kuporomoka na nchi yetu kulazimishwa kufuata masharti ya Shirika la Fedha la Dunia (IMF) na Benki ya Dunia.
Mwaka 1750 mchumi wa kijerumani Johann Heinrich Gottob von Justi aliandika nchi zote zinazolazimishwa kuzalisha malighafi tu zitaelewa kuwa zilikuwa zinawekwa kwenye umasikini wa kudumu. Wakati shabaha ya Azimio la Arusha ilikuwa ni kuodokana na onyo hili la mchumi Gottob von Justi, kuanzia mwaka 1992 Tanzania ilianza kuvunjavunja misingi ya Azimio la Arusha na kurudi miaka 25 nyuma. Kimsingi uvunjaji ulianza kidogo kidogo kuanzia mwaka 1986 na ndio maana mwaka 1987 hapakuwa na tathmini iliyowazi ya Azimio kama ilivyokuwa mwaka 1977. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mwaka 2017 tunaadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha kwa kufanya tathmini ya miaka 25 ya utekelezaji wa Azimio na Miaka 25 ya kutupwa kwa Azimio. Chama cha ACT Wazalendo kinaanza mchakato huo sasa kwa kutangaza Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha.
Kuanzia mwaka 1996 tulianza kuona viwanda vyote tulivyojenga kwa pamoja vikibinafsishwa na kupewa watu wachache na wengi wageni. Tulianza kuona mabenki tuliyomiliki wote kama Taifa yakiuzwa kwa bei ya kutupwa. Kimsingi ubinafsishaji sio tu ulikuwa ni ugenishaji wa uchumi wetu bali ulikuwa ni deindustrialisation. Leo hii hakuna hata kiwanda kimoja cha Korosho kinafanya kazi licha ya kubinafsishwa, lakini Watanzania wote bado wanalipa madeni ya kujenga viwanda hivyo maana tulijenga kwa mikopo. Hali ni kama hiyo kwa viwanda vya nguo ikiwemo ginneries mbalimbali. Badala ya kufanya vile mataifa mengine yalifanya ili kupata maendeleo, sisi tuliamua kufanya tunachoambiwa kufanya. Tulisahau msemo wa kizungu Dont do as the English tell you to do, do as the English did. Ni watu wachache wanajua kuwa nchi kama Norway ilipiga marufuku nguo kutoka nje mpaka miaka ya mwisho ya hamsini. Hata kuagiza gari binafsi ilikuwa ni mafuruku nchini Norway katika hatua zake za mwanzo za kujenga uchumi wao. Leo Norway ni nchi ya kupigiwa mfano kutokana na usimamizi wa rasilimali zao. Tufanye walivyofanya, tusifanye tunavyoambiwa tufanye.
Wananchi, tulijaribu Azimio kwa miaka 25 na kufanikiwa kujenga Taifa moja lenye viwanda licha ya changamoto za ki uendeshaji tulizokumbana nazo. Tumejaribu sera za kiliberali kwa takribani miaka hiyo hiyo na kufanikiwa kujenga Taifa lenye nyufa nyingi na matabaka ya walionacho na wasio nacho. Sasa ni wakati wa kurudi kwenye misingi kwa kurekebisha makosa ya miaka 25 ya Ujamaa na kuchukua mafanikio ya miaka 23 ya uliberali na demokrasia na hivyo kuanza mchakato wa kujenga Taifa la Ujamaa wa KiDemokrasia. Tabora ndio kitovu cha historia ya nchi yetu na ndio maana tuliamua kuja Tabora kufanya kazi hii ya kihistoria. Lazima kufanya maamuzi ya busara.
Wananchi, Wazee wetu walikutana katika ukumbi tuliokutana sisi leo mwaka 1958 ili kufanya maamuzi kuhusu hatma ya uhuru wa nchi yetu. Wakati huo uhuru uliokuwa unatafutwa ni uhuru wa kisiasa. Walifanya Uamuzi wa Busara. Uamuzi wa Busara wa Tabora wa TANU wa mwaka 1958 ulijibu changamoto ya kuharakisha Uhuru wa Tanganyika kwa kukubali uchaguzi wa kura tatu. Uamuzi wa Busara wa Tabora wa mwaka 2015 unataka kujibu changamoto ya kurudisha utaifa wetu kwa kuhuisha Azimio la Arusha na hivyo kushawishi kubadili sera zetu za kiuchumi kwa shabaha ya kumilikisha uchumi kwa wananchi wenyewe.
Tumeeleza hapo awali kuhusu changamoto za nchi yetu. Kwanza hatuna budi kuhuisha Azimio la Arusha ili kurejesha itikadi moja ya kitaifa inayotuunganisha na kuziba nyufa za udini na ukabila ambazo zinashamiri katika nchi yetu hivi sasa. Tunaanza kuona viongozi wa dini wakichukua nafasi kubwa kwenye siasa hivi sasa kwa sababu hakuna itikadi ya kitaifa. Kuna ombwe na asili haipendi ombwe ( nature abhors vacuum). ACT Wazelendo ina imani kwamba lazima kurudi kwenye misingi ili kuepusha nchi kusambaratika. Udini na Ukabila utafutika kutokana na kuwapo kwa Itikadi ya kitaifa kwani Udini ni itikadi na Ukabila ni itikadi.
Pili, tuna uchumi unaojenga Matabaka. Hivi sasa uchumi wetu umeshikwa na watu wachache hususan wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao. Azimio la Tabora linahuisha Azimio la Arusha kwa kurudi kwenye uchumi wa Ujamaa wa kisasa utakaojikita katika kuongeza uzalishaji mali na ugawaji sawa wa keki ya Taifa na hivyo kupunguza matabaka nchini kwetu.
Tatu, tuna changamoto ya huduma za kijamii hasa afya na elimu ambapo hivi sasa huduma hizi zimekuwa kwa matabaka. Wenye uwezo kifedha wana shule zao na hospitali zao na masikini wana shule zao dhaifu na hospitali duni. Tunahuisha Azimio la Arusha ili kurejesha muundo wa utoaji huduma muhimu kama Afya na Elimu kwa kuhakikisha kuwa shule za umma na hospitali za umma zinakuwa ni bora zaidi.
Nne, tuna kansa ya ufisadi ambapo watu hutumia nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali. Ufisadi ni tatizo zaidi la viongozi walioshika madaraka ya umma. Tunahuisha Azimio kwa lengo la kusimika miiko ya Uongozi wa Umma ambayo itakuwa msingi mkuu wa mapambano dhidi ya ufisadi.
Wananchi, leo tunafanya yale waasisi wa Taifa letu walitaka tufanye ya kuhakikisha misingi ya nchi yetu inarejeshwa. Leo tunaanza kazi hiyo ambayo inaweza kuchukua muda mrefu kufikia malengo yetu. Inawezekana malengo yakafikiwa na watoto wetu au wajukuu zetu lakini ni lazima kazi hii ifanyike. Ndio maana tumekuja kuanzia Tabora, mahala ambapo wazee wetu waliamua kuharakisha Uhuru wa nchi yetu. Uamuzi wa Busara wa Tabora ni nguzo ya Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha. Tunaanzia hapa kuirudisha nchi yetu kwenye misingi na kumilikisha uchumi kwa wananchi.
Chanzo: Zitto Kabwe (FB page)