Azim Dewji: Magufuli alikuwa na Nia yake, Wewe (Samia) Wasikufitinishe

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,194


Azim Dewji amemwambia Rais Samia: Rais Wetu Aliyepita(John Magufuli) Alikuwa na Nia Yake na Wewe (Samia Suluhu) Una Yako, Wasikufitinishe

Source : JamiiForums

========

Azim Dewji: Mama kila kitu inategemea kwenye nia, Rais wetu mpendwa aliepita alikuwa na nia yake na wewe sasa hivi una nia yako, wasikufitinishe wala wasikusumbue. Hawa wakorofi utatuachia sisi watu wa madhehebu tutawaombea na Mungu atawaangamiza alivyomuangamiza Firaun.

Tabia moja ya binadamu, sisi ni wasahaulifu sana na Mungu analijua hilo. Inasikitisha kuona kwamba sisi tunasahau mazuri yaliyofanywa na hayati Magufuli, kuna mambo mengi amefanya lakini mimi nitagusia moja.

Alisumbuka tangu uwaziri wake kujenga barabara kwenye nchi hii lakini wapo wanasiasa wamepauka au wamefilisika kisiasa wanakuja kusema barabara inasaidia nini!

Wanasahau kwenye nchi yetu moja tulitaka kwenda Bukoba ilibidi twende Kenya, tupite Uganda halafu ndio tufike Bukoba, ni miaka 10 tu kabla tulikuwa tunashindwa kwenda.

Kwenye miaka mitano ya Rais Magufuli sisi watu wa Dar es Salaam hatujawahi kusikia mlio wa bunduki, hatujawahi kupata shida ya umeme, siku hizi watu wameacha kuuza majenereta.
 
Mdogo wake alitekwa ili asaini nyaraka muhimu na mpaka leo ile bilioni aliyotoa haijapata muokotaji. Yani hawa walamba viatu sijui tutawamaliza lini! Shina limekatwa ila bado wanaleta ngebe!
 
KUNA MTU ANAJUA UHUSIANO WA KINDUGU KATI YA Azim Dewji NA Gulam Dewji; baba Yake Mo Dewji?
 
Jamaa kiroho safi anamwagia sifa mwendazake bila kinyongo
Nikikumbuka yule mlinzi alivyokua anapiga mkono wake asigusane na hayati daah
 
Back
Top Bottom