Azim Dewji: Lissu amuombe radhi Biteko; Matamshi wanayotoa wapinzani hayapaswi kuumiza watu wengine

Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Watu wazuri hawafi
 
Nilichokielewa kikubwa kabisa ni...

Kama mh Tundu lisu siku awe kiongozi, angependa kuitwa majina ya hovyo kama anavyowaita viongozi wengine, Je angependa tumdharau kama anavyoonyesha kuwadharau viongozi wengine?

Dewj kaongea point

Point gani?

Biteko hakujua au kuona hayo ni maandamano abadili uelekeo?

Kwanza naamini angepishwa ingekuwa full aibu kwake bora walivyogoma kumpisha!
 
Dewji ni mnyaturu kumbe!! Na Rostam ni mnyamwezi, tunasubiri umeme,wengine wanasubiri sukari,wengine maji,hiyo meli sijui itafika lini,au usikute ilishazamishwa na hizbolah
Ubaguzi utakuua mbwa ww..unadhani kazaliwa mkoa gani?
 
We gabachori kaa kwa kutulia ,unajua kwamba biteko ndiyo amevunja sheria?
Huyu Azim Dewji ameitumia sana Simba kujitajirisha! Huko nyuma aliwabebesha wachezaji wa simba madawa ya kulevya bila wao kujua!!
Wakiemda kucheza mechi za nje kila mchezaji alikabidhiwa mpira uliojazwa madawa ya kulevya, akifika huko waendako, anaikusanya hiyo mipira na kutoa bidhaa zake!!
Azim kama Rostam sio wa kuwaamini. Kumbukeni Rostam ndio alikuwa architect wa kashfa ya EPA enzi ya marehemu Balali:
hawa gapacholi sio wa kuwaendekeza!
TISS hawana budi kulinda rasilimali za nchi kwa kumlinda Samia na hawa fisi wanaotaka kutumia udhaifu wake wa kutokuwa na weledi ili wafanikishe ujangili wao!
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.

Kisheria barabara ikiwa na maandamano kwa muda ule hawaruhusu magari sasa Biteko alitoka wapi ?? tatizo watu walitaka kuzua matatizo na kujaribu kumpitisha
 
kila moja awe huru kufanya yake wakati wote 🐒

..polisi na Chadema walipaswa kuzungumza kuhusu waandamanaji ku-share barabara na msafara wa Naibu Waziri Mkuu wakati wa MAANDALIZI ya maandamano.

..mimi nazipongeza pande zote kwa kutunza AMANI kwani upo uwezekano baadhi ya watu walitaka mambo yaharibike ili waanze kumshutumu upande huu au ule.
 
for sure ingeguswa gari ya waziri Mkuu au kuzuia kabisa msafara ule nadhani ingetoa picha mbaya sana kwamba waziri Mkuu anazuiwa asifanye kazi zake vip wasafirishaji, watumia barabara wengine mathalani wauuza ndizi au maji ambae nae anafanya kazi zake na haelewi wala si sehemu ya maandramano 🐒

For sure
uungwana ulotumika kuepusha shari kwa upande wa waandamanaji, polisi na msafara wa naibu waziri Mkuu ni muhimu sana kumaintain utamaduni huu wa kustahimiliana tunapofanya mambo yetu 🐒
 
..napenda kuamini kwamba Polisi waliamini maandamano ni SALAMA ndio maana wakampitisha NWM na msafara wake katikati ya waandamanaji.
 
Back
Top Bottom