Azama na kufa katika maji,jijini Tanga

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,149
6,989
Kufuatia mvua kubwa zinazonyesha jijini Tanga,mtu mmoja asiyefahamika,amezama na gari yake,maeneo ya Makorora,makaburi ya Maftahaa,karibu na hospital ya Makorora.
Wasamaria wema walizama ndani ya maji,na kuutoa mwili wa marehemu,tukio hilo limetokea mchana huu.
Sikuweka picha ya marehemu,kwa kulinda heshima ya marehemu.
 
Ndo wapi huko?
Kulikuwa na mafuriko

Hata ivo Mungu awe faraja ndugu wote na jamaa wa karibu wa marehemu
 
Ndo wapi huko?
Kulikuwa na mafuriko

Hata ivo Mungu awe faraja ndugu wote na jamaa wa karibu wa marehemu
Ni jijini Tanga,Somaiya Road,mvua zinazonyesha zimejaza maji katika barabara hii ya lami nzuri,na ukiiona sawa na mpya.Dereva wa hii gari,nafikiri alifikiri maji sio mengi,lakini kumbe ni mengi,na kuizamisha Landcriser yake.
 
Kufuatia mvua kubwa zinazonyesha jijini Tanga,mtu mmoja asiyefahamika,amezama na gari yake,maeneo ya Makorora,makaburi ya Maftahaa,karibu na hospital ya Makorora.
Wasamaria wema walizama ndani ya maji,na kuutoa mwili wa marehemu,tukio hilo limetokea mchana huu.
Sikuweka picha ya marehemu,kwa kulinda heshima ya marehemu.
Poleni sana wafiwa, gari limezama mtoni? au baharini? Nafikiria mazingira ya mjini kuwe na bwawa au mfereji wa kuzamisha gari hadi lipotee kabisa.
 
tanga tuna mfeleji mkubwa sana unaotoa maji katika maeneo mbalimbali ya mji kupeleka baharini kwa hiyo usi shangae hilo muhimu kujua tu ilikuaje na kumuombea kheri marehemu
 
Gari lilitumbukia kwenye maji au ilikuwaje hebu tulia uandike taratibu
Huyu Dereva wa gari alikuwa atokea maeneo ya GBP petrol station,kwa kupitia Somaiya Road,alipofika maeneo ya makaburi ya Maftahaa,maji mengi yalikuwa yamejaa barabarani,wapo wasamariya wema,walimuonyesha ishara ya kusimama,lakini hakusimama,akataka kupita,nafikiri gari ikamzimikia,baada ya kuzibwa na maji.Na wakati huo huo,pembeni kulikuwa na la gari la Tank ya mafuta,limezima,linalokwenda kuchukuwa mafuta bandarini.
Huwenda hakuona haya maji kwa kuzibwa na gari kubwa la tank ya mafuta.
 
Kwa wanatokea Makorora hospital,jijini Tanga,na wanatokea GBP petrol station kwa Somaiya Road,wajuwe kuna maji yaliyojaa maeneo ya makaburi ya Maftahaa,bora kukatiza Barabara ya kanisani kutokea shule ya Usagara secondary.
 
Siku yake ilifika. Watu wamemtahadharisha hakuwafuatilia, ana landcruiser, pia halikufua dafu!
 
Back
Top Bottom