Maji ya Kibada Kigamboni na hekaya za CCM

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,904
Usiku wa deni ni mfupi sana! Kesho ndio kesho ndio kesho siku tuliyoahidiwa umeme wa uhakika na mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano! SIMLAUMU kwa asilimia kadhaa maana naye alihakikishiwa na wateule wake! Akaridhika na hakikisho akasahau kukumbushana! Mambo ni mengi ni vigumu kukumbuka yote

Tanesco ni fupa gumu lililomshinda hata fisi. Kuna fupa lingine la SGR..! halitafuniki, halimezeki, halitemeki kufa halifi, kuishi haliishi.. Lipo tu hapo lilipo kama zezeta..! Mama hajui alifanyeje..!

Nusu ya pili ya mwaka jana 2023 kulitokea tatizo kubwa la maji jijini Dsm! Kelele zikawa nyingi mno.. Mama kuhoji wakamyingiza kingi cha maana! Haraka haraka likatengenezwa tukio la kuzindua kisima kikubwa cha maji kilichopo Kibada Kigamboni.. Na ahadi ya kwamba maji yake yatafika jijini ndani ya wiki mbili na tatizo la maji kuwa historia..!
Wananchi wakaamini kwa asilimia 100 na kwa shangwe kubwa.. Lakini huo ulikuwa uongo mkubwa maana mpaka January hii 2024 yale maji yalikuwa hayajavuka hata bahari!

Marehemu Edward Lowassa kwenye sekeseke la umeme wa Richmond aliwahi kusema.... tukileta siasa kwenye umeme, tatizo la umeme halitaa liishe

Edward Lowassa aliponzwa na kupush mambo yaende haraka! Serikali ya CCM haijazoea kupush mambo mpaka kuwe na maslahi binafsi hasa ya rushwa na 10%

Hakuna watendaji wabovu, wavivu, wasiofuatilia na goigoi kama watendaji wa serikali ya CCM... Sehemu pekee ambayo wako makini nayo sana ni sehemu ya shekeli hasa kama kuna maslahi binafsi
Tofauti na hapo ni business as usual
Kufuatwa na gari nyumbani
Kupelekwa kazini
Kujifungia ofisini
Kusoma magazeti
Kupata chai
Kupitia ripoti juujuu na kuzisaini
Kupokea wageni
Kupata lunch
Kuchat
Kumaliza siku
Kuondoka ofisini

Ufuatiliaji zero.. Wanategemea ripoti za wasaidizi
Wasaidizi nao wanategemea ripoti za mainjinia
Mainjinia nao wanategemea ripoti za wakandarasi
Mkandarasi yeye naye hutoa ripoti kulingana na joto lililopo.. Kwa sehemu kubwa HUDANGANYA!

WAtendaji na wataalam waendao site kwa sehemu kubwa hudanganywa na wakandarasi na hawafuatilii sana kwakuwa nguvu ya kufuatilia humalizwa na bahasha walizoandaliwa!

Tushishangae sana ya umeme kuna ya SGR na kuna ya maji ya Kigamboni na mengine mengi!
Mvua zilizinyesha mfululizo December na January
Zimeokoa mengi
Zimeficha mengi
Zimesingiziwa mengi

Je mama anakumbuka maji ya Kigamboni hayajafika huku mjini!?

Watendaji wa serikali ya CCM ni tatizo donda ndugu! Halina tiba..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mtu ni mwanajeshi mwenye nguvu hivi unampigaje Mzee kama Yule ,Una nguvu Kwa nini usimwambie Kwa kumshika mkono ,weeee Mzee sogea pale !!! halafu kwani marehemu lowasa angeguswa angefufuka?wanajeshi ambao mipaka Yao inalindwa na waarabu huku wao wapo busy ni wake zao pumbavuuuu
 
Mungu mwenyewe ameshachoka.
Mungu wa kuchoka sio Mungu! Most likely itakuwa kaweka uso wake mbali nasi; katupa kisogo!

Mfalme ajishushe, ajikane, ararue mavazi yake ya dhahabu, avae magunia, ajipake majivu, atuongoze kuutafuta uso wa BWANA nchi ipate kupona.

Historia imeonesha hivyo; nchi zilipona kwa namna hiyo. Mkishupaza shingo mmekwisha! "Wamedi" watatwaa nchi yenu na mahali penu na kizazi chenu.
 
Umemaliza kila kitu.
Kusema ukweli hawa watawala wanatukosea sana sisi wananchi, ......yaani hawajali kitu ....bize wanapambana kuhakikisha wanabaki madarakani na kujikusanyia mihela kwa njia yoyote ile.
 
Chadema kina miaka thelasini na zaidi tangu kianzishwe, mpaka leo hawana ofisi ya makao makuu, wanapanga tu
 
Bila ccm kufa, ama kupata KATIBA MPYA yenye maslahi kwa nchi na wananchi...
Tutabaki hapahapa miaka nenda rudi.
Kukichwa kutapambazuka
20240216_055516.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku wa deni ni mfupi sana! Kesho ndio kesho ndio kesho siku tuliyoahidiwa umeme wa uhakika na mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano! SIMLAUMU kwa asilimia kadhaa maana naye alihakikishiwa na wateule wake! Akaridhika na hakikisho akasahau kukumbushana! Mambo ni mengi ni vigumu kukumbuka yote

Tanesco ni fupa gumu lililomshinda hata fisi. Kuna fupa lingine la SGR..! halitafuniki, halimezeki, halitemeki kufa halifi, kuishi haliishi.. Lipo tu hapo lilipo kama zezeta..! Mama hajui alifanyeje..!

Nusu ya pili ya mwaka jana 2023 kulitokea tatizo kubwa la maji jijini Dsm! Kelele zikawa nyingi mno.. Mama kuhoji wakamyingiza kingi cha maana! Haraka haraka likatengenezwa tukio la kuzindua kisima kikubwa cha maji kilichopo Kibada Kigamboni.. Na ahadi ya kwamba maji yake yatafika jijini ndani ya wiki mbili na tatizo la maji kuwa historia..!
Wananchi wakaamini kwa asilimia 100 na kwa shangwe kubwa.. Lakini huo ulikuwa uongo mkubwa maana mpaka January hii 2024 yale maji yalikuwa hayajavuka hata bahari!

Marehemu Edward Lowassa kwenye sekeseke la umeme wa Richmond aliwahi kusema.... tukileta siasa kwenye umeme, tatizo la umeme halitaa liishe

Edward Lowassa aliponzwa na kupush mambo yaende haraka! Serikali ya CCM haijazoea kupush mambo mpaka kuwe na maslahi binafsi hasa ya rushwa na 10%

Hakuna watendaji wabovu, wavivu, wasiofuatilia na goigoi kama watendaji wa serikali ya CCM... Sehemu pekee ambayo wako makini nayo sana ni sehemu ya shekeli hasa kama kuna maslahi binafsi
Tofauti na hapo ni business as usual
Kufuatwa na gari nyumbani
Kupelekwa kazini
Kujifungia ofisini
Kusoma magazeti
Kupata chai
Kupitia ripoti juujuu na kuzisaini
Kupokea wageni
Kupata lunch
Kuchat
Kumaliza siku
Kuondoka ofisini

Ufuatiliaji zero.. Wanategemea ripoti za wasaidizi
Wasaidizi nao wanategemea ripoti za mainjinia
Mainjinia nao wanategemea ripoti za wakandarasi
Mkandarasi yeye naye hutoa ripoti kulingana na joto lililopo.. Kwa sehemu kubwa HUDANGANYA!

WAtendaji na wataalam waendao site kwa sehemu kubwa hudanganywa na wakandarasi na hawafuatilii sana kwakuwa nguvu ya kufuatilia humalizwa na bahasha walizoandaliwa!

Tushishangae sana ya umeme kuna ya SGR na kuna ya maji ya Kigamboni na mengine mengi!
Mvua zilizinyesha mfululizo December na January
Zimeokoa mengi
Zimeficha mengi
Zimesingiziwa mengi

Je mama anakumbuka maji ya Kigamboni hayajafika huku mjini!?

Watendaji wa serikali ya CCM ni tatizo donda ndugu! Halina tiba..!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ziara za Makonda zinadhihirisha uozo huu; japo hazina suluhisho la kudumu!
 
Chadema kina miaka thelasini na zaidi tangu kianzishwe, mpaka leo hawana ofisi ya makao makuu, wanapanga tu
Kwahiyo ofisi ya Chadema ndo italeta maji na umeme we chawa promax? CCM wana ofisi mpaka nyumbani kwa mabalozi. Niambie zinaleta maji na umeme. Ndugu yangu kama huna kitu cha kuandika is better ukae kimya kuficha ujinga wako. Watu wanaongelea mambo muhimu ya umeme na maji wewe unaongelea ofisi za chama cha upinzani ambacho hata kodi hakikusanyi. Ndugu akili unaachaga wapi kabla ya kupost?
 
Una akili zako timamu kabisa au zimefyatuka mkuu ? Inaweza kuwa chadema ni wapuuz pia ila wanahusikaje hapa ? kila siku huwa nawauliza watu kwanini watu wa ccm wanapenda kulinganisha upumbavu wanaofanya wao na upumbavu wa chadema ? Yan mnashindana kwenye ujinga, yan kujua nan mjinga zaidi ? Why ?
 
Kwahiyo ofisi ya Chadema ndo italeta maji na umeme we chawa promax? CCM wana ofisi mpaka nyumbani kwa mabalozi. Niambie zinaleta maji na umeme. Ndugu yangu kama huna kitu cha kuandika is better ukae kimya kuficha ujinga wako. Watu wanaongelea mambo muhimu ya umeme na maji wewe unaongelea ofisi za chama cha upinzani ambacho hata kodi hakikusanyi. Ndugu akili unaachaga wapi kabla ya kupost?
Lipopoma hilo jamaa
 
Back
Top Bottom