Azam Ukwaju wanautoa wapi?

Huo ndiyo ukweli. Hakuna cha ukwaju halisi hapo. Vinywaji vingi wanavyodai ni matunda halisi siyo kweli Bali ni flavour tu ya tunda husika
 
Inawezekana ikawa inatokana na hii miti ya ukwaju inayojiotea sana maporini. Mwaka 2011 nilikuw naona watu wakiiangusha sana hii miti ili mradi wapate hayo matunda yake kwa wingi. Walikuwa wanajaza hata fuso.
 
Mzee baba alichofanya ni kuipa thamani, ila juice za ukwaju tumekunywa sana tandare kwa tumbo na huku vingunguti kabla ya hizo ukwaju zake.
 
Naomba kufahamu Azam ukwaju wanaotumia kutengenezea juice ya ukwaju (ukwaju halisi)wanapata wapi?hili zao inalimwa wapi kwa uwingi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukwaju ni matunda pori kama ilivyo kwa mbuyu ,pia ukihitaji kuotesha waweza otesha na kuupanda, unamea kama maharage kipindi kifupi cha siku14 na unaanza kuzaa matunda baada ya miaka5.

Miti hiyo inapenda na kustawi sana maeneo yenye ukame.

Nenda mkoa wa Simiyu na Shinyanga utaamini ninachoandika.

Inachofanya kampuni ya Azamu ni kukusanya kwa mawakala waliopo mikoa hiyo ya Simiyu Shinyanga na Tabora, kisha husafirsha kuleta Dar kiwandani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa scale ya production ya hiyo azam ukwaju, juice na ice cream, siamini kwamba ukwaju kama tunda unatosheleza mahitaji ya kiwanda, ni lazima kutakuwa na means nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa scale ya production ya hiyo azam ukwaju, juice na ice cream, siamini kwamba ukwaju kama tunda unatosheleza mahitaji ya kiwanda, ni lazima kutakuwa na means nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu sifahamu content katika utengenezaji wake, hilo sifahamu.
Lakini mwaka huu 'ajenti' wa Azamu walikuwa wananunua ukwaju ghafi kwa bei nzuri sana tu, waliwapiku hata wafanyabiashara wa sokoni.

Mikoa hasa ya Simiyu ukwaju unapatikana kwa ma tani.

Kule mikwaju inavyostawi, mti mmoja unavunwa hadi gunia5.

Kumbuka na Wachina nao wananunua kupeleka kwao kama malighafi ya vipodozi.
Ukwaju sasa hivi ni mali dhahiri, hasa baada ya Azamu kuupromot ukwaju na kufanya kuwa bidhaa yenye wateja kibao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mimi huwa ndio namuuzia,misukule yangu ndio inaupanda huo ukwaju,ukiwa tayari kuvunwa,unavunwa na anapelekewa azam
 
Sio maziwa ya ng'ombe hata label wameandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…