Azam TV yapewa leseni ya kurusha chaneli za ndani

Azam TV yapewa leseni ya kurusha chaneli za ndani

Ni kweli startimes, nilinunua cha 140,000 mwaka wa pili huu napata local channel
 
Unapata Chanel ngapi za FTA?
Wapuuzi hawa walinishangaza uti kupwatwa na msiba wakatuzibia AFCON.... Basi channel yao ikaacha kurusha ila wakaona haitoshi mpaka KBC wakawa wanaizima wakati wa mpira.

Hawaoni thamani ya pesa yetu tuliyolipa, wapuuzi wa karne.

Ng'amuzi lao meligeuza nalitumia kwa dish kubwa FTA.
 
View attachment 1097798View attachment 1097798

Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amelieleza Bunge leo Jumanne Mei 14, 2019 kuwa kituo cha televisheni cha Azam jana Jumatatu kimepokea leseni ya kuonyesha chaneli za ndani bure.

Pia, Nditiye amesema katika kipindi cha miezi saba watajenga mfumo wa kurusha chaneli hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuvuta subira.

Naibu waziri ametoa kauli hiyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Mlalo Mkoani Tanga (CCM), Rashid Shangazi aliyehoji Ni kwa nini Azam wananyimwa haki ya kuonyesha channel za ndani bure.

"Je, Serikali haioni kuwanyima haki hiyo wakati wengine wamepewa ni kukiuka ibara ya 18 ya katiba ambayo inatoa haki ya kupata habari, lakini hata Rais wetu anatumia Azam kurusha matangazo yake hivyo tungejitangaza hadi nje," ameuliza Shangazi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula, aliuliza Serikali iwapo haioni kupitia TCRA kuwafungia local channels (chanel za ndani) baadhi ya ving'amuzi ikiwamo Azam TV, DSTV na vingine imewanyima wananchi fursa ya kupata habari..

Naibu waziri amesema Serikali inatambua umuhimu wa wananchi kujua mambo yanayoendelea, hivyo imetoa leseni zenye masharti tofauti.

Amesema kwa sasa matangazo ya umma yanarushwa na TBC1 na TBC3 maarufu safari channel.
Kwa mujibu wa Nditiye, kampuni zinazomiliki ving’amuzi vya DSTV, Zuku na Azam hayakustahiki kutoa huduma ya kubeba chaneli za ndani zisizolipiwa kutokana na masharti ya leseni zao.

Amesema Serikali imefanya jitihada ya kukaribisha maombi ya leseni ya kubeba maudhui ya chaneli za ndani kutoka kwa wanaohitaji kutoa huduma ikiwamo
upuuz mtupu.
 
Iko hivu leseni ya kulipia kama dstv zuku azam, hutumi satellite tu hada leseni yake ni bei ndogo, leseni yenye local ni bei kubwa shart lazima ujenge mitambo ya ardhini ili wenye antenna wakupate kma star times kuna antenna na dish ndio sheria inataka azama kabadiri leseni iwe kama star times kwahio wakishajenga tu free Chanel tano za ndani
Sasa Mkuu,wewe umenielewesha vizuri
 
Back
Top Bottom