AZAM TV tuwekeni sawa; Mna mpango wa kurejesha Local Channels?

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
2,023
Reaction score
2,218
Ni wakati sasa AZAM TV kutuweka sisi watumiaji wa ving'amuzi vyenu kama mnao mpango wowote wa kupata leseni ya kuonyesha local TV channels au ndio basi tena, tutafute ustaarabu mwingine?

Bado kiu yetu ya kupata Habari iko palepale licha ya kwamba yaliyotushawishi kujiunga na nyinyi yametoweka!
 
Isingekuwa kuonesha ligi yetu na ile ya Spain walahi nisingelipia! Azam wanatudhulumu sana kwa kweli
 
Inasikitisha sana...

Wenye local channels wenyewe hawana shida... shida mnaijua ipo wapi...

Cc: mahondaw
 
Kinachouma zaidi ni kuwa Azam two hata taarifa ya hanari hawaweki tena,wanatuambia kama tunataka taarifa ya hanari tukaangalie kwenye app yao!
Hapa ndio nashindwa kuwaelewa!
 
Wewe unaishi nchi gani mpaka usijue kwamba Azam hawana leseni ya kurusha hicho unachotaka?
Kiufupi hawawezi kurusha local channels walizokua wakirusha zamani maana TCRA imewapiga biti kwakua leseni zao haziruhusu, sio Azam tu hata Dstv tunaugulia maumivu hayo hayo
 
Huu uzi ni vizur umeuleta hapa ila jaribu kuedit tuweze kujua AZAM na DSTV wana mpango gan na hizo local chanel?
 
Nadhani hata wao Azam Tv hili linawaumiza kabisa kwani impact yake kimapato kwao ni negative kabisa. Nafikiria km endapo tatizo ni mkataba waliouingia awali,sasa wanapata sababu ya kukaa vzr na serikali ili waurekebishe. Kwa hali ya sasa,inamlazimu mtu km anaipenda Azam Tv basi amiliki king'amuzi kingine tena...hii haikubaliki hata kidogo. HII THREAD INAHITAJI MAJIBU YA WAHUSIKA WA AZAM TV WAJE NA MAJIBU YA NINI MIPANGO YAO.
 
Huu uzi ni vizur umeuleta hapa ila jaribu kuedit tuweze kujua AZAM na DSTV wana mpango gan na hizo local chanel?

nilisikia siku tcra wakisema wakati wanatangaza zabuni azam ilikuwa haijaanzishwa so haikushinda wala haikushiriki.

labda serekali itumie busara lasi hivyoo hizo local chanel mnaweza msizione kwa mda mrefu.

ONLY IN TANZANIA
nikuangalie TBC penda usipende.
 
Wewe unaishi nchi gani mpaka usijue kwamba Azam hawana leseni ya kurusha hicho unachotaka?
Kiufupi hawawezi kurusha local channels walizokua wakirusha zamani maana TCRA imewapiga biti kwakua leseni zao haziruhusu, sio Azam tu hata Dstv tunaugulia maumivu hayo hayo
Mkuu umenielewa au umekurupuka?Nimesema,azam tv hawarushi tena taarifa ya habari ya saa 2,wala vipindi vilivyokuwepo awali kama alasiri lounge,adhuhuri,morning trumpet NK!Ukitaka kuviona vipindi hivyo lazima udownload application ya Azam tv halafu uangalie kwa kutumia bundle!Mfano,azamu two,ukiweka asubuhi kupitia king'amuzi utakuta matamthilia ya kihindi,ila ukiweka channel hiyo hiyo kupitia application utakuta Morning trumpet!
Sasa kwanini wanatufanyia hivi?Mtu unatoa hela hata taarifa ya habari ya azam huioni mpaka ununue bundle uangalie kwa app!
 
Kama haiwezekan basi tutupe haya madude yao very stupid.
 
Mkuu umenielewa au umekurupuka?Nimesema,azam tv hawarushi tena taarifa ya habari ya saa 2,wala vipindi vilivyokuwepo awali kama alasiri lounge,adhuhuri,morning trumpet NK!Ukitaka kuviona vipindi hivyo lazima udownload application ya Azam tv halafu uangalie kwa kutumia bundle!Mfano,azamu two,ukiweka asubuhi kupitia king'amuzi utakuta matamthilia ya kihindi,ila ukiweka channel hiyo hiyo kupitia application utakuta Morning trumpet!
Sasa kwanini wanatufanyia hivi?Mtu unatoa hela hata taarifa ya habari ya azam huioni mpaka ununue bundle uangalie kwa app!
Mkuu hata mimi nashindwa kuelewa hapo. Wengi wetu huwa tunakusanyika kama familia kutazama taarifa ya habari kimazoea.

Sasa shida ni pale unapolazimika kuikusanya familia yako mmebebana kama vitunguu mnaangalia taarifa ya habari kwenye screen ya simu. Hapo bado kuna mtu anakupigia kwenye simu hiyo hiyo.

Yani utafikiri hujalipia kifurushi. Kama wameshindwa kuonesha chaneli za ndani sawa! Na sababu za kutulazimisha kuangalia taarifa ya habari kwenye app yao ni nini?

Hivi hawa watu wana mshauri wa masuala ya biashara? Dah!
 
Azam kama ingekua sio ligi kuu kuoneshwa na wao tu ingekua tushawafyekelea mbali..
 
Mkuu hata mimi nashindwa kuelewa hapo. Wengi wetu huwa tunakusanyika kama familia kutazama taarifa ya habari kimazoea.

Sasa shida ni pale unapolazimika kuikusanya familia yako mmebebana kama vitunguu mnaangalia taarifa ya habari kwenye screen ya simu. Hapo bado kuna mtu anakupigia kwenye simu hiyo hiyo.

Yani utafikiri hujalipia kifurushi. Kama wameshindwa kuonesha chaneli za ndani sawa! Na sababu za kutulazimisha kuangalia taarifa ya habari kwenye app yao ni nini?

Hivi hawa watu wana mshauri wa masuala ya biashara? Dah!
Kwakweli hata siwaelewei!Basi tu hapa nyumbani wananisumbua waangalie sinema zetu,otherwise nisingekuwa nanunua kifurushi!
Niko kwenye mpango wa kubadilisha king'amuzi!
 
Mi nafikiria kununua king'amuzi cha AZAM - Kenya. Nasikia wao bado wanarusha "Local Channels za Tanzania zote".
 
Back
Top Bottom