Azam Tv na ulimbukeni wa 'replays'

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Huwa mnapoonyesha Mechi kumekuwa na timing mbovu pale mnapotaka kurudia tukio fulani kama la faulu, kosakosa ya goli, Golikipa kuokoa mpira wa hatari n.k.

Sidhani kama ni mara zote kuna ulazima wa kurudia papo hapo haswa kama kuna movement inaendelea.

Mnaweza kusubiria hata baadae mpira ukitoka au Kipa akidaka n.k...badala ya ninavyoona mara kadhaa mmekuwa mnakatisha movement na kurudia tukio bila ulazima wowote, huenda ile movement ni muhimu kuliko hicho mnacholazimisha kukirudia.

Pia pale mnapomuonyesha Mchezaji fulani, haswa kwa ukaribu (close up), muwe sensitive pale inapoonekana Mchezaji huyo anataka kupenga, au kutema basi mumuondoe pale pale baada tu ya kufanya hivyo badala ya kuacha tu Watazamaji tunaangalia.

Kutumia camera ni zaidi ya kuseti white balance, hata common sense inahitajika sana maana si kila kitu mtafundishwa darasani.
 
Kuna kipindi mpira unaendelea wanatuonyesha jamaa zao jukwaani
Ambayo sio mbaya ila tatizo ni timing...wawe wanatafuta muda muafaka kufanya hivyo sio kukatisha move.

Na move ikikatishwa ndio basi tena Watazamaji mmeikosa, maana watarudi Mpira upo goal kick na hamtajua hiyo goal kick ilikuwaje.
 
Back
Top Bottom