Azam TV na "Hekaya za Abunuasi" wapoteza mvuto kwa watazamaji kwa kwa kujiingiza katika "siasa"

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Nilikuwa natazama taarifa ya habari ya Azam saa mbili za usiku huu na katika habari za leo kuna habari mbili zilizopelekea mimi kuandika makala hii fupi ambayo ntaawachieni nyie kama wasomaji mfanye tathimini yenu.

Habari ya kwanza (a) kampuni ya Azam kupitia Mkurugenzi wake (mmiliki) ametoa Kiasi cha shilingi Millioni 100 kuchangia ujenzi wa ofisi mpya ya CCM inayojengwa huko Pwani katika “’fund raising’’ iliyosimamiwa na Makamu wa Rais Pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri JK leo huko Pwani.

Kwangu mie hiyo haikuwa ‘’issue” kubwa kwa yeye kutoa mchango huo kwani sio mbaya ila tatizo langu ni kwamba ameutoa kwa wakati gani na kwa nia gani. Habari nilizo nazo (za uhakika) Kampuni ya Azam wanataka kujenga kiwanda kikubwa cha kubangua korosho Pwani na tayari wameomba na kuidhinishiwa Mkopo kutoka Benki ya Kilimo (Benki ya Kisiasa ya serikali TADB) ya kiasi cha... (nisikitaje kwa sasa) Ila ni kikubwa saana na wanapewa mwaka huu.

Kwa akili ya kawaida hiyo milioni 100 ni kama shukrani kwa mkopo kwani kwa akili ya kawaida mtu anayeweza kutoa sadaka ya zaidi ya Milioni mia kama mchango ni mtu aliye na uwezo wa hali ya juu hata pengine asingehitaji huo mkopo. Ilo halikunistua saana hili la pili ninalo taka kulileta kwenu ndo limeniistua saana

Habari ya Pili..’”Magereza na Chadema wapishana kauli kwa tukio lilotokea jana wakati akitolewa gerezani Mweneyekiti wao. Hakuna shaka kwamba mpaka sasa kila Mtanzania anaelewa ‘”kipondo” walichopewa wanaChadema waliojitokeza jana kutaka kumpokea mwenyekiti wao mintarafu kwa maagizo kutoka juu.

Tatizo hapa ni kwamba katika habari ya usiku huu, kichwa cha habarii na taarifa nzima kuhusu tukio hilo iliyoonyeshwa na kituo hiki cha TV ni “’Paka na Panya”. Kichwa cha habari kinasema Chadema na Magereza wapishana lakini habari nzima iliyoonyeshwa na kurudiwa rudiwa mara nyingi ni ya Msemaji wa Magereza tu huku akiwalaumu Chadema eti walileta taaharuki katika maeneo ya Gereza, jambo ambalo lingehatarisha amani na utulivu kwenye maeneo ya gereza na hakuna kiongozi wa Chadema au mwanachama aliyeonyeshwa akihojiwa na Azam kuthibitisha au kukana kulingana kichwa cha habari kilivyokuwa kimeeleza.

Mimi dukuduku langu ni kwamba pamoja na msaada wanaopata AZAM, kampuni kupitia taasisi mbali mbali za Serikali nachelea kusema kuwa wanatupotosha na bahati mbaya hatujapata mbadala wa chombo kingine cha habari hapa nchini kama ilivyokuwa ITV kabla nayo kuvamiwa na CCM baada ya uchaguzi wa 2015.Japo mie nafamilia yangu tunaangalia na kuamini DSTV siku hizi, AZAM tunayo basi tu, ila ningewaomba Watanzania tutumie wakati huu kuwaoyesha Azam kuwa hawatakiwa kuchanganya upenzi wao kisiasa na kazi ya umma.

Nimesikitishwa saana leo taarifa ya habari ya AZAM na kwa mara ya kwanza nimezimia kwamba sintolipia tena kifurushi cha AZAM kwa msimu huu uliobaki (mwaka huu woote) hadi uishe kwani nilikuwa naangalia AZAM kwa ajili ya ligi ya TZ na taarifa ya habari ya saa mbili usiku tu.

Kwa upande wa taarifa ya habari wameniangusha "big time", kwa upande wa mpira tayari timu yangu ya Simba ni mabingwa na wameshacheza mechi zote na watani kwa hiyo sioni sababu ya kuendelea kulipia AZAM na hivi uchaguzi unakuja labda mwakani wakijirekejibisha pengine tutakuwa na serikali mpya huwezi jua.
 
Siku hizi hakuna taarifa za habari hapa, bora hata utazame taarifa za habari za tv za CAR, DRC, GAMBIA, unaweza ukaona uhalisia wa kinachoendelea kwenye mataifa hayo, japo hayakuhusu!!!
 
Back
Top Bottom