Azam tv mnachokifanya hakivumiliki

Azam tv mnachokifanya hakivumiliki

ecolizer baba

Member
Joined
Sep 29, 2010
Posts
88
Reaction score
310
Azam Tv hiki mnachofanya hakivumiliki.

Wananchi tulianza kuwaamini sana kwa huduma zenu za matangazo ya televisheni. Taarifa zenu za habari na hasa Campaigns zilikuwa balanced kwa vyama vyote vikubwa vya siasa na hasa CHADEMA/UKAWA kwa upande mmoja na CCM kwa upande mwingine zilikuwa balanced bila bias yoyote.

Lakini kwa takribani wiki mbili zilizopita tunaona tofauti kubwa sana na hasa kwa upande wa mgombea urais wa,CHADEMA/UKAWA Mh. Edward Lowassa. Taarifa za mikutano yake hamzioneshi vizuri siku hizi na hata kama mtaonesha huwa camera zenu zinawakwepa umati wa wahudhuriaje ambao huwa ni wengi na badala yake mnaishia kuonesha high table tu.

Na kwa siku ya leo ndio mmetia fora kabisa. Licha ya kuacha kuonyesha mikutano ya Lowassa huko kanda ya ziwa lakini pia mmetunyima kusikia alichosema Mh. Freeman Aikael Mbowe juu ya Msiba wa M/kiti mwenza wa UKAWA Dr. Emmanuel Makaidi. Wakati mtangazaji anatangaza hiyo habari sauti ilikuwa inatoka lakini Mh. Mbowe alipoonyeshwa akitoa tamko la UKAWA kuhusu kifo cha Mh. Makaidi sauti ikakata. Ilipoisha habari ya Mbowe sauti ikarudi. Kwa kweli wana-UKAWA wameumia sana kwa hiki mlichotufanyia leo. Na hata hamkuomba radhi.!!!

Am sure Ndg. Tido Mhando ni mtu ambaye ni smart sana na huenda hajui hiki kinachotokea. Huenda anahujumiwa na mafundi mitambo na watangazaji wa Azam.

Azam tv kumbukeni kuwa mna wateja toka vyama vyote na wote wanalipa gharama sawa kila mwezi. Hivyo acheni kutakatisha tamaa wateja wenu. Kama imekuwa ikitokea kwa,bahati mbaya basi ni busara muwe mnaomba radhi.

MODS NAOMBENI MSIUFUTE UZI HUU KWANI TUNA HAKI YA KUONYESHA MASIKITIKO YETU KWA JF IS WHERE WE DARE TO TALK OPENLY.
 
hawawezi kuonesha umati wa watu unaowadai wewe inasemekana picha ni za kuunganisha ambalo ni kosa la jinai
 
Mwaka huu lazima mnye mezani tena kwa shuruti, mnalalamika sana na mbowe ndo alipochemka, kawajenga bavicha ktk msingi wa kulalamika tu, hawana solutions! mnakimbia hadi vivuli vyenu!
 
Tunashukuru Mungu kuwa ITV ndiyo inayotazamwa na watu wengi sababu iko kny kila king'amuzi, hao azam anayewaona ni yule mwenye king'amuzi chao tu.
 
100% kesho nilikuwa nika nunuwe kingamuzi chao kwaiyo nibora niache maana watu waliwasifia siku mwanzo mwa kampeni asnte bora pesa yangu nile kwa furaha 25 na 26 na 27oct maana lazima lowassa ashinde
 
jamani tido mhando nae kawa mbaya?.....


ndo maana nikasema ukawa ni walalamishi sana,,,,,na hawachelewi kubadilika kama kinyonga...
 
Watanzania kwa sasa ni watu wa kulalamika kwa kila kitu.
Uzuri uko na options tune to other TV ndo uone kuwa mbona hawa wana afadhdali
 
jamani tido mhando nae kawa mbaya?.....


ndo maana nikasema ukawa ni walalamishi sana,,,,,na hawachelewi kubadilika kama kinyonga...

Tatizo unakurupuka. Rudi soma tena alichoandika
 
nyie nao kila kituo cha habari mnaugonvi nacho kila siku mnaongoza idadi ya maadui tu sijui mkoje
 
Hawa mods wamekuwa wanabebelezwa kila siku wasifute posti za watu hapa kwa nini msiondoke na ki forum chenu hiki!? Imefikia hatua kila anayeleta habari anakuwa na wasiwasi wa uwepo wa habari yake hapa jf. Futeni na hii posti yangu.
 
Back
Top Bottom