Azam Media ongezeni kamera uwanjani

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,531
3,331
Salaam,

Naomba nianze kwa kuipongeza kampuni ya Azam kwa kuliheshimisha soka la bongo kwa kurusha LIVE matangazo ya mechi za ligi kuu ya NBC. Ombi langu kwenu AZAM MEDIA ni kuwa mtume timu ya wataalamu wenu waende uingereza,spain au ujerumani wakajifunze namna ya kurekodi na kurusha matangazo ya mpira LIVE.

Bado mnatakiwa muongeze uwekezaji katika camera zenu hususani kamera za juu na zinazochukua uwanja kwa upana,camera za offside na pia replay zenu zinatakiwa ziwe instant kuonesha matukia yaliyotokea muda mfupi uliopita hii itasaidia hata TFF nao kujiongeza kuleta technolojia ya VAR hapa nchini ili kuondoa changamoto ya waamuzi hivyo kuifanya ligi yetu kuwa bora zaidi.
 
I think ungewashauri TFF waongeze posho kwa marefa wao. Hii ndio itaondoa sintofahamu za kubebwa bebwa.

tukirudi nyuma miaka kumi hakukuwa na makamera haya yote unayoyaona na bado soka lilikuwa na kiwango kizuri

Pia katika wadhamini kuwe na fair competition, mdhamini akishaweka pesa aache kuingilia gem kufosi ushindi kwa timu aliyoidhamini.

Ni hayo
 
I think ungewashauri TFF waongeze posho kwa marefa wao. Hii ndio itaondoa sintofahamu za kubebwa bebwa...
Asante kwa mchango wako...mada yangu imejikita sana katika kusisitiza uboreshwaji wa urushaji wa matangazo...angalia jinsi DSTV wanavyorusha matangazo ya ligi ya south Africa...na jinsi inavyorushwa na Azam.

kuna tofauti kubwa sana. Ni wazi kuwa camera zinazotumika kurekodi mechi ni chache sana na wataalamu wanao operate hizi kamera na urushwaji wa matangazo ya mechi live pia ni wachache.
 
Msimu wa mwaka juzi mechi ya mbeya city vs yanga kuna goli walipewa yanga lakini kwa marudio ya tukio huwezi kuona kama mpira ulivuka mstari au haukuvuka kipindi mchezaji wa mbeya city anaokoa. Kwa kweli matukio ya kurudia mengi yanakuwa sio clear.
 
Msimu wa mwaka juzi mechi ya mbeya city vs yanga kuna goli walipewa yanga lakini kwa marudio ya tukio huwezi kuona kama mpira ulivuka mstari au haukuvuka kipindi mchezaji wa mbeya city anaokoa. Kwa kweli matukio ya kurudia mengi yanakuwa sio clear.
Hata mechi ya simba na geita utata ulisababishwa na camera za azam kuwa chache na wale waliorudia walishindwa kuonyesha replay vizuri. Camera iliyoko lango la geita ilikuwa haionyeshi contact yoyote wakati ya lango la simba ndio ilionyesha kila kitu kwa mujibu wa ufm habari
 
I think ungewashauri TFF waongeze posho kwa marefa wao. Hii ndio itaondoa sintofahamu za kubebwa bebwa...
Inawezekana kabisa wewe huwa hutazami Mpira.

Miaka ya nyuma hakukuwa na malalamiko, Una uhakika? Marefa wamepigwa sana miaka ya Nyuma. Pia hujui tabu tunayopata wakati wa kutazama Mpira, mfano mechi za Mkoani Azam nadhani wanaenda na Camera mbili tu.

Azam kuonyesha ligi Hafanyi hisani ni biashara ile, kama ambavyo yupo busy kuongeza bei za vifurushi ndio atuongezee na Camera tupate tunachostahili. Inawezekana mleta mada kabase upande wa kuclear doubts kuhusu maamuzi, ila tabu yangu mimi ni Huduma.
Iendane na 20k+ tunazompa kwa mwezi.

Naona analenga faida tu saiv, kupeleka kisimbusi chake Nje ya nchi...., anaisahau ligi iliyomuweka kwenye ramani. Azam Tv, ongezeni camera aseee.

Na kama kuna mamlaka yoyote inayosimamia hili swala ilifuatilie asee. Na kama ni TFF kwenye mkataba wao na Azam TV, ikifika mda wa kureview mkataba, wawambie watuongezee camera aseee.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana kabisa wewe huwa hutazami Mpira......
Miaka ya nyuma hakukuwa na malalamiko, Una uhakika? Marefa wamepigwa sana miaka ya Nyuma.
Pia hujui tabu tunayopata wakati wa kutazama Mpira, mfano mechi za Mkoani Azam nadhani wanaenda na Camera mbili tu.
Azam kuonyesha ligi Hafanyi hisani ni biashara ile, kama ambavyo yupo busy kuongeza bei za vifurushi ndio atuongezee na Camera tupate tunachostahili....
Inawezekana mleta mada kabase upande wa kuclear doubts kuhusu maamuzi, ila tabu yangu mimi ni Huduma.
Iendane na 20k+ tunazompa kwa mwezi.......
Naona analenga faida tu saiv, kupeleka kisimbusi chake Nje ya nchi...., anaisahau ligi iliyomuweka kwenye ramani.
Azam Tv, ongezeni camera aseee.
Na kama kuna mamlaka yoyote inayosimamia hili swala ilifuatilie asee.
Na kama ni TFF kwenye mkataba wao na Azam TV, ikifika mda wa kureview mkataba, wawambie watuongezee camera aseee.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Ni kweli inabidi waongeze camera uwanjani
 
Asante kwa mchango wako...mada yangu imejikita sana katika kusisitiza uboreshwaji wa urushaji wa matangazo...angalia jinsi DSTV wanavyorusha matangazo ya ligi ya south Africa...na jinsi inavyorushwa na Azam....kuna tofauti kubwa sana. Ni wazi kuwa camera zinazotumika kurekodi mechi ni chache sana na wataalamu wanao operate hizi kamera na urushwaji wa matangazo ya mechi live pia ni wachache.
Bila kusahau kamera moja sio chini ya dola laki mbili
 
Azam waboreshe mambo mengi kitu cha kushangaza hadi Poster zao bado zina quality mbovu kwa kituo kikubwa kama hicho.
 
Salaam, Naomba nianze kwa kuipongeza kampuni ya Azam kwa kuliheshimisha soka la bongo kwa kurusha LIVE matangazo ya mechi za ligi kuu ya NBC. Ombi langu kwenu AZAM MEDIA ni kuwa mtume timu ya wataalamu wenu waende uingereza,spain au ujerumani wakajifunze namna ya kurekodi na kurusha matangazo ya mpira LIVE.Bado mnatakiwa muongeze uwekezaji katika camera zenu hususani kamera za juu na zinazochukua uwanja kwa upana,camera za offside na pia replay zenu zinatakiwa ziwe instant kuonesha matukia yaliyotokea muda mfupi uliopita hii itasaidia hata TFF nao kujiongeza kuleta technolojia ya VAR hapa nchini ili kuondoa changamoto ya waamuzi hivyo kuifanya ligi yetu kuwa bora zaidi.
Mkuu ,Tatizo siyo camera Azam Wana camera za kutosha ambazo unazisemea ,Tatizo ni wataaalamu.Hawana wabobezi WA kuzitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom