The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo wa Iran na Israel, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Picha za runinga ya serikali zilimuonyesha akiwasalimia waumini kwenye msikiti siku ya Jumamosi kabla ya tamasha la waumini wa Kishia linalofahamika kama Ashura.
Mara ya mwisho Khamenei kuoneka ilikuwa katika hotuba iliyorekodiwa wakati wa mzozo na Israel, ulioanza tarehe 13 Juni na wakati ambapo makamanda wakuu wa Iran na wanasayansi wa nyuklia waliuawa.
Israel ilifanya mashambulizi ya kushtukiza katika maeneo ya nyuklia na ya kijeshi nchimi Iran. Hatua ilisababisha makabiliano makali baada ya Iran kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya angani yaliyolenga Israel.
Wakati wa vita vya siku 12 na Israel, Khamenei alionekana kwenye TV katika ujumbe wa video na kulikuwa na uvumi kwamba alikuwa amejificha kwenye chumba chini ya ardhi.
Siku ya Jumamosi matangazo ya vyombo vya habari vya Iran yalitawaliwa na mwonekano wa Khamenei, huku wafuasi wakionyesha kufurahia kumuona kwenye televisheni.
Khamenei anaonekana akimgeukia kasisi mkuu Mahmoud Karimi, akimhimiza "kuimba wimbo wa taifa, O Iran".
Wimbo huo wa uzalendo ulipata umaarufu mkubwa wakati wa mzozo wa hivi majuzi na Israel.