Baada ya kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei kufuatia mashambulizi ya anga, uongozi mpya ulitangazwa rasmi ambapo mwanawe, Mojtaba Khamenei aliteuliwa kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, hadi sasa kiongozi huyo mpya hajaonekana hadharani, na haijulikani iwapo yuko hai, amefariki dunia au amelazwa hospitalini. Tetesi mbalimbali zinaeleza kuwa huenda alijeruhiwa katika mojawapo ya mashambulizi ya Israel.