severinembena
JF-Expert Member
- Jun 2, 2018
- 2,435
- 2,404
Yaani siku hizi ni uongo uongo tu kwenye hii wanaita industry ya Muziki. Utasikia Madee amnunulia dogo janja gari la mil. 18, Mara harmonize ampa shilole gari la mil. 20 kwenye birthday yake, Mara ney Wa mitego anamiliki gari za kifahari 4 na mijengo 7 ya hatari hapa jijini Dar es salaam. Hapo ulipo jaribu tu kuandika kwenye Google nyumba ya Ali Kiba au harmonize uone mijengo utayoletewa ili hali wahusika wenyewe wanaishi kwenye nyumba za kupanga na wazazi wao wanaishi kwenye nyumba za kawaida tu saa myingine hata kukarabati mziki. Sasa unajiuliza huyu mtu ana uwezo Wa kumpa mil 20 mtu kama zawadi lakini home kwa wazaz ni ungaunga. Sasa sijui ndio kukua kwa Muziki wenyewe ndio maana na uongo unakua!?