Fanya ufanyavyo, sema uonavyo, danganya uwezavyo lakini siku moja tutakubaliana kwamba muungano huu una kasoro nyingi.
Ukiishaungana hasa kwa style hii ya muungano wetu lazima kuwepo na chain of command inayo usisha pande zote za muungano, kwa mfano mawaziri wa wizara zilizo kwenye muungano wanaripoti kwa marais wote wawili au wanaripoti kwa rais wa muungano tu?
Kama hivyo ndivyo basi rais wa Zanzibar atakuwa hajatendewa haki. Kuna serikali mbili ndani ya muungano wa nchi mbili, eti moja ni serikali ya muungano yenyewe(maana serikali ya tanganyika haipo) na serikali ya Zanzibar, sasa hii confusion yote ni ya nini?
Halafu kuna shida gani ya kuunganisha wizara zote? Ili tuwe na serikali moja? Mimi bado sana huu muungano unanipa shida kuuelewa maana naona kama ni wizara fulani zimeunganishwa na ni heri serikali ya Zanzibar iwe inapewa nafasi ya kuteua mawaziri wa wizara zilizounganishwa.