Awamu ya Tano fitna kama alizofanyiwa Lowasa hazina nafasi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,095
164,438
Imejidhihirisha ktk awamu ya tano fitna za kisiasa na makandokando yake havina nafasi tena.Zamu hii ikiundwa tume ni lazima ifanye kazi kwa weledi na haki kwa pande zote izingatiwe likiwemo swala zima la haki ya asili.Kwa kuzingatia hilo hata ilipozuka figisu ya mchanga wa madini, baada ya JPM kuzungumza ilbimbidi Spika Ndugai kutia timu "mwenyewe" bandarini akiambatana na kamati ya madini.Halikadhalika Waziri Mkuu akatimba "mwenyewe" huko buzwagi kuutafuta ukweli.Hii inaonyesha ktk awamu ya 5 hakuna kiongozi aliye tayari kuingizwa chaka kwa maslahi ya kisiasa ya kundi fulani.Nadhani report ya Richmond Vs report ya Nape/Clouds zimewafungua macho viongozi.Yule aliyesema "kisheria" haikuwa lazima kumhoji mtuhumiwa ili kutimiza takwa la natural justice mnamo 2008 ndio HUYOHUYO leo anasema ni lazima kisheria kumhoji mtuhumiwa ili kutimiza takwa la haki ya asili, then watanzania tunapiga makofi.Siasa hizi za kimkakati sio za kuziendekeza zina madhara mapana kwa jamii.Hongera JPM hongereni pia Ndugai na Majaliwa kwa utendaji na umakini wenu!
 
Back
Top Bottom