Awamu ya Sita Watu wanajenga, mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni

Mtihan san!! Swal liko open kbs.. sema awamu ya tano kulikua na moja mbili tatu ndio maan watu hata kujenga walishindwa pia awamu ya sita ipo moja mbili tatu ndio maan watu wanajenga kila uchao!! Mbona simple? Mna nn nyie uvccm lkn?

Hapo ndio unakwama. Kudhani kila mtanzania ni CCM au chadema.
Au Mkristo au muislam.
Siku mkijua kuwa kuna zaidi ya uchama na udini ndio nchi Hii itaendelea
 
Mimi huwa naamini sana kwenye storage ukitaka kupiga pesa kwenye kilimo

Storage ni changamoto kwa wakulima wengi wanashindwa kuhifadhi mazao yao mpaka bei zinapopanda na kuwa na faida maradufu

Wengi huuza mazao yao wakati wa mavuno hapo bei lazima ziwe chini ila mavuno yakipita baada ya miezi kadhaa bei hupanda hapo ndipo pesa ilipo

Mazao ya chakula ni kucheza tu na wakati unapiga hela vizuri tu

Kumbe hiyo ni fursa Kwa Vijana wenye mitaji
 
Hapa Dar kuna baadhi ya wafanyabiashara wanadai eti awamu hii mzunguko wa pesa umepungua ikilinganishwa na awamu ya JPM.

Hawawezi kukosekana.
Ila ukweli ni kuwa nenda Sinza, Kinondoni, mwenge, Tabata, Tegeta Angalia Fremu zilizokuwa zimefungwa sasa hivi zinafunguliwa.

Kipindi cha awamu ya tano serikali ilikuwaa Pesa lakini awamu hii kuna uwiano mzuri baina ya serikali na watu.
Serikali inamwaga mapesa
 
Umeeleweka well, turudi kweny swal langu la msingi kwaajil ya faida ya wana jamvi. Ahsnt

Vizuri.
Kipindi cha awamu ya tano serikali ilitumia mfumo wa kutaka kuendesha karibu kila kitu, yaani ilitaka kujiingiza katika biashara kwa kile kilichoitwa kubana matumizi.

Hapakuwa na semina na kama zilikuwepo basi zilidhibitiwa zisihusiane na swkta binafsi, mfano kutokuchua Hoteli kwaajili ya semina.

Semina ni pesa. Mbali na mafunzo.
Kutokuongeza Mishahara na kuajiri watumishi wapya pia ilichangia mzunguko wa Pesa kuwa Mdogo.

Kuzuia mikutano ya kisiasa ambayo pia ni sehemu ya chanzo cha Ajira Kwa vyama vya upinzani, pia ni sehemu ya kuifinya Pesa.

Uhuru wa vyombo vya habari, na Uhuru WA Maoni kulizuia mzunguko wa Pesa.
Lakini sasa hivi kila MTU yupo huru, kupitia Uhuru ni rahisi kufanya biashara, kwani biashara ni Uhuru.
 
Ni kweli kabisa awamu hii ukiamua kukaza hata kwenye biashara unatoboa hela ipo wasioamini waache wabishe .
 
Ni kweli Mtibeli ,awamu ya "MAZA" watu wanajenga sana! Yaani kama kipindi cha JAH-CAR-HIRE.
 
Wanaachaje kujenga wakati watumishi wote wenye haki ya kupandishwa madaraja wamepandishwa,leo kila Idara hakuna anaestahili kupanda cheo hajapandishwa,ukioanda cheo hela inaongezeka,unaenda Bank kuikope hnajenga vyumba viwili na sebule unaachana na maisha ya kupanga.

Baa na Clabu za usiku zinafurika watu wanaofanya matumizi.

Matajiri sasa wanafanya biashara bila bughudha na mitutu ya bunduki.

Yaani utawala wa Mama tutaukumbuka siku akina Dikteta mwingine kuitawala nchi yetu.
 
Wengi wanajenga maeneo ambayo hayajapimwa,that's 80% ya miji yetu ni squatter no planning
 
Kwanza hakuna mahala ambako Serikali haina mradi na haya Sasa ndio matokeo ya tozo unaokoteza mia mia ila inaenda kusaidia wengi na Kwa vitu vya msingi.

Ujenzi uko kuanzia kwenye Halmashauri Hadi kwenye skimu za Umwagiliaji.

Mfano mwaka huu pekee Serikali inaenda kujenga nyumba za Maafisa ugani zaidi ya 4500 Nchi nzima.na hii ni Wizara Moja tuu ya Kilimo Bado elsewhere.

Kiufupi 70% ya Bajeti ya Serikali inaenda kwenye ujenzi.
Ila bado kuna watu wanakwambia serikali haifanyi kitu
 
Back
Top Bottom