Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
Kwema Wakuu!
Tukiweka itikadi za Siasa pembeni, udini, na ukabila na tofauti zetu pembeni, ukweli usemwe; Watu wanajenga.
Ingawaje Mimi sina kiwanja hata cha 20*20 na pengine hata Nusu ya Pesa ya kununulia hicho kiwanja lakini ukata huo haunifanyi niwe kipofu kuona wengine wakijenga.
Kuna mmoja nilienda kumuuliza, nini kinaendelea? Ninyi Pesa za ujenzi mnazitolea wapi? Akaniambia, huu ndio muda jombaa, changamka, usipojenga sasa hesabu maumivu.
Yeye hajengi kibanda, anajenga nyumba, namaanisha nyumba hasa.
Mtaa ninaoishi na mitaa ya mbali ninayopitaga ninakuta nyumba zikivunjwa na kufanyiwa maboresho, huku vile viwanja vilivyokuwa wazi vikijengwa.
Mafundi wapo busy Mno. Nina marafiki zangu ambao tulimaliza NAO kidato cha nne, Kwa sasa ni mafundi nyumba, wako busy. Ile kawaida yetu ya kukutana kila Jumamosi na Jumapili kwenda Kula Bata ni zaidi ya Mwaka sasa imekoma. Wako busy Mno.
Rafiki yangu mmoja ambaye kiumri tunalingana kabisa, ananiambiaga wewe kalia kuandikaga Huko mitandaoni, ukija kushtuka unageuka mpangaji wangu.
Sasa Mimi Pesa nitatoa wapi? Hamtaki kunifungulia Pattern, anyway. Hongereni nyote ambao Njia zimewafungukia awamu hii.
Yote juu ya yote, Hongera serikali Kwa kuimwaga Pesa mtaani. Mwenye macho haambiwi tazama.
Najua sio wote Pesa zimewafikia(huenda hata Mimi ni mmoja wenu) lakini mwenzako akipata nawe shukuru😊😊.
Tanzania ni yetu site.
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam