Ntozi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 226
- 299
Bila kupepesa macho,na bila kuhangaika na itikadi za vyama,na pia ukiachana na uchambuzi wa kitaalamu,awamu ya Mzee Mwinyi na awamu ya kikwete,ndizo awamu ambazo mwananchi wa kawaida alifurahia maisha.
Pamoja na mapungufu ya kiutawala yanayoongelewa katika awamu hizo,lakini pesa ilipatikana kirahisi, mahitaji muhimu yalipatikana Kwa bei ya kumudu,ajira zilikuwepo muda wote nk
Nyerere kipindi chake, changamoto zilitokana na uchanga wa nchi baada ya Uhuru,wasomi walikuwa wachache,Sera ya ujamaa na Vita vya kagera.Changamoto hizo,zilipelekea wananchi kuishi maisha magumu yasiyoelezeka.sabuni,Colgate,sukari na mahitaji mengine yaligeuka kuwa anasa,kiasi kuwa kukutwa navyo ilikuwa ni tayari uhujumu uchumi.Hivyo Mwinyi alipoingia aliamua kuachana na Sera mbovu za awamu illiyopita na kuruhusu biashara huria.Mzee anapendwa hadi Leo.
Mkapa alikuja na Sera yake ya kubana matumizi,na kulipa madeni ya nje.Awamu ikaitwa ukapa.Mzunguko wa hela ukawa mgumu kwelikweli.
Kikwete alipoingia mambo yakafunguka tena,kazi na bata, siasa zikafanyika.wenye kusema wakasema,wakulaumu wakalaumu.Baada ya hapo ni historia. Awamu ya tano ilikuja na imepita, Watu Kwa sasa wanaiangalia awamu ya 6.Mama anaongea vizuri Sana,Kwa sauti ya matumaini,Kwa lugha ya staha na upole,hivyo wananchi wanasubiri matendo sasa.
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app