Awamu ya matamko, maandamano na Intelijensia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Awamu ya matamko, maandamano na Intelijensia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by We can, Jan 23, 2011.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Upepo wa maandamano. Unaandamana na ma Tamko. Na kabla ya Tamko kuna habari za kiintelijensia. Wanaotoa taarifa za kiintelijensia kwa sasa ni Polisi...Who cares.

  Nimeuona upepo huu ukitokea Afrika ya Kaskazini, walao kwa mwaka huu. Watu wanaandamana (Tunisia, Algeria) na kuna dalili kama hizo Sudan na Ivory Coast...Who cares.

  Wana CCM na wana CHADEMA wanatoa ma TAMKO. Mimi najiuliza, je, ma TAMKO yatatusaidia? Je, maandamano yatajenga nchi? Who cares.

  Nilikuwa napata hofu zamani kuwa Mwl Nyerere akifariki, nani atakuwa Rais...kumbe ikawezekana. Nilimwamini sana. Na onyo lake leo juu ya kuvunja muungano ninalizingatia; kwamba mkivunja mwungano hamtaishia hapo....mtasema sisi ni wazanzibara,....lakini wanasayansi nao wanatuambia, haya mabara tuliyonayo leo, yamepitia historia ndefu; kuna wakati yalikuwa pamoja (kama PANGEA), baadaye yakaachana na kuungana kule na kuachana huku, nk. kumbe kuungana na kutengana ni jambo la kawaida...Who cares.

  Hofu yangu mimi, ni pale Polisi watakapoandamana kama ilivyotokea Afrika kusini; je, itatokea nini? Mimi sitaki kuongelea nini kitatokea, lakini niongelee INTELIJENSIA. Je, nani atatupatia taarifa za kiintelijensia? Wo cares?

  Mimi natoa TAMKO, maana ni mwaka wa ma TAMKO, kwamba wanaosababisha uchungu wa maisha hadi watu waandamane, tunataka WAJIUZURU MARA MOJA. Je, wasipojiuzuru? Who cares!
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Why should we care? who cares?
  Sisi watz tunaishi kwa tamaa kuwa iko siku mambo yatakuwa sawa ,bila ya kuwekwa sawa.
  Tunaishi kwa tamaa kuwa iko siku na sisi tutapata nafasi ya kuingia katika exclusive club na tutapata fursa ya kuvuna shamba la bibi.
  Tuna nidhamu ya woga.
  Lakini zaidi ya yote, sisi tunaringia amani na utulivu wetu...tunasubiri wito wa matembezi ya mshikamano!.... who cares?
  Sisi tumeridhika na kula takwimu za uchumi unakua na unaboreka...lakini aalaaas! Mifuko imetoboka... who cares?

  Habari za kiinteligensia zinasema uchumi umekuwa, unapaa lakini maisha ya mlalahoi yanazidi kuwa magumu...tutatoa tamko hivi karibuni kuhusiana na mkanganyiko huu.
  Kabla ya watu kuandamana wasubiri Tamko...tamko litatoka baada ya tume kutoa mapendekezo yake...tume itaundwa mwakani mwezi wa pili...wananchi tuwe na subira.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  WHO CARES?kama hatuonyesh kuwa twachukizwa na madhambi ya watawala we2
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Who cares: if what you care is your own maslahi; uchungu wa watu wako is tatizo bali tatizo ni maandamano ambayo unajua hayakuwa ya fujo...who cares about your lame questions if you choose to call truth a lie and a lie to be truth maana polisi ndio wanaoleta fujo wakati watu wanaandama kwa amani; who cares if you think maandamano ya amani ni bora kuliko vita...kwamba watu wanapoandamana wanataka ku-raise issues/challenges...ambazo ni reality yao...who cares about aperson who doesn't care
   
 5. W

  We can JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Oo yes... upepo huu wa matamko, maandamano na taarifa za kiintelijensia unavuma kwa kasi, kisha naambiwa kuna watu wameagizwa kuuzuia kwa kutumia rungu, je, inawezekana? Berlin nao walijaribu kuzuia mitazamo ya itikadi kwa kujenga ukuta mkuubwa, hatimaye umebaki kuwa ni ukuta wa kitaliii.

  Ndugu wapendwa mnaohusika: Ukiamua kumziba mtu mdomo kwa kutumpiga hadi kumjeruhi, utasababisha watu wajikusanye na kumpeleka hospitali, je, huo siyo mkusanyiko mwingine? Ukipiga risasi watu wakafa, watu wataandamana kwenda kuwazika, je, hayo siyo maandamano makali zaid? Ni makali kuliko upepo....Who cares!

  Huko Tunisia askari polisi nao ni kama vile wameandamana kuwaunga mkono wananchi mitaani-upepo gani huo....Who cares!
   
Loading...