Avunjika MIGUU akipandisha bendera ya CUF

Avunjika MIGUU akipandisha bendera ya CUF

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=3][/h]



​

Akizungumza akiwa kitanda namba 4 katika wodi namba nne ya majeruhi ya wanaume katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine alisema


MKAZI wa Mtaa wa Mwenge Manispaa ya Lindi, Abdulahmadi Rashid amenusurika kufa baada ya kuanguka kutoka mwenye mlingoti wa kupeperushia bendera na kuvunjika miguu yote wakati alipokuwa anafunga bendera ya Chama cha Wananchi (CUF).

Tukio hilo lilitokea saa 12:00 asubuhi siku ya Desemba 9, mwaka huu katika Tawi la CUF lililopo Kituo cha Mabasi ya mkoa katika Manispaa ya Lindi.Akizungumza akiwa kitanda namba 4 katika wodi namba nne ya majeruhi ya wanaume katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine alisema anamshukuru Mungu kwa kumnusuru na kifo kwani hakutegemea kama atakuwa salama kutokana na ajali hiyo.

Alisema kuwa mlingoti alikuwa amepanda una urefu wa zaidi ya futi 18 na kwamba alikuwa anakwenda kubadilisha bendera ya chama chake ambayo ilikuwa imechakaa kwa kuwa ilikuwa ya muda mrefu.

Alisema wakati akifunga bendera hiyo ghafla mlingoti huo ulikatika katikati na kumsababishia kuanguka na kupoteza fahamu huku akiwa amevunjika katikati ya vifundo vya miguu yake yote miwili.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CUF mkoa wa Lindi ambaye ni mbuge wa Jimbo la hilo Salamu Baruani alikiri kuwapo kwa tukio na kueleza kuwa chama kinamuhudumia kwa kumpatia mahitaji yote tangu akutwe na tatizo hilo.

Baruani alisema kuwa wamelipokea tatizo hilo kama la chama kwa kuwa kijana huyo ni miongoni mwa wananacha ambao wanakitumikia chama kwa vitendo bila ya kujali hali ya kiuchumi ya chama.

Aliwaomba wanachama wengi ne kumsaidia kijana kwa kutoa kila walichonacho ili apate na atibiwe ili aweze kuruhusiwa akaendelee na kazi za chama



MWANACHI
 
Pole ndugu yangu kwa kuumia sana na kuvunjika miguu.

Mungu mkuu wa Israel akuponye na kukulinda. Amen
 
Katiba mpya ikataze huu ujinga wa kuwa na Bendera na Nguo za vyama vya siasa.
 
Pandisha ya CHADEMA tu, hata Mungu atakubariki,
maana hizo zingine tangu wamefunga ndoa na kushirikiana kuwakandamiza wananchi masikini, Mungu amewalaani .

Sasa akipandisha ya CHADEMA atakua anakaribisha Sodoma na Gomora maana Cameroon, David ndiye mfadhili wao! Hapo vipi wajner??
 
Sasa akipandisha ya CHADEMA atakua anakaribisha Sodoma na Gomora maana Cameroon, David ndiye mfadhili wao! Hapo vipi wajner??
Huyo David Cameroon alishakuja Tanzania mara ngapi? na mara zote alipokelewa na alifanya mazungumzo na nani?
 
vyama vingine nuksi.kwani ni lazima wamwage damu kila mara?Bendera gani inahitaji mtu kupanda juu hivyo.Hawajui hata nani kawalaani hawa wana wa shetani.
 
Bendera inapandishwa au kubadilishwa kwa kukwea mlingoti au unasimama tu chini, pemben ya mlingoti na kupandisha kwa kuvuta kamba??? Pole kaka ila hapo kuna element ya uzembe!!!
 
mh pole yake, atakua na maumivu ila hii habari ilivyo anvekua hajaumia ningecheka sana it sounds funny
 
Huyo David Cameroon alishakuja Tanzania mara ngapi? na mara zote alipokelewa na alifanya mazungumzo na nani?.......

Kwani ili uwe mfadhili au muwekezaji kuna ulazima wa kukanyaga ardhi ya hao unaowafadhili? Kila siku munalalamika Kikwete huenda atakatika miguu kwa kutembeza bakuli nchi za mbali, je nchi zote anazotembeza sinia wao wameshakuja hapo kwenu?
 
Back
Top Bottom