Hoja ya ko ya msingi ya kuwabarasa ndugu zako ili uishi na mke ni nzuri, japo inategemeana sana kati ya mtu na mtu...Lakini pia inatokana na sababu zilizomfanya huyo anayeishi hapo aje hapo!...Kuna ndugu wengine ambao tunakaa nao haiwezekani kumwambia aondoke, au kumpeleka kwa jamaa!...Wengine ni Yatima!...Lakini pia kama mtu niliekuwa naishi nae kabla ya kuoa ni mstaarabu, kuna shida gani kuendelea kuwapo pale kwangu?....Tuangalie na upande wa pili kwamba ndoa isilete mvunjiko wa mahusiano na jamaa zetu, maana ni kitu chema!...Kama kuwatoa nduguzo nyumbani ni shinikizo la huyo mke, basi ujue pia kuwa familia hiyo mpya haitaonja amani!