Auondoe ule utamu, hili janga litakuwa limekwisha. Hivi bwana yule anasubiri nini?

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Vilio Ni vingi!
Ooh ni viiingi saana!
Hawa wameuana kwa wivu wa mapenzi, huyu amejinyonga, yule anakonda amesalitiwa, mmh makubwa haya!

Kwenye nyumba ile, wazazi hawana amani juu ya watoto wao wa kike! Vischana vimepevuka, vifua vimetuna, vitako vimebinuka tayari. Kwanini Sasa wazazi, hawana amani juu ya maendeleo ya watoto wao wenyewe?

Shuleni Kuna migogoro mikubwa!
Waalimu dhidi ya mienendo ya wasichana. Wazazi wa wanafunzi wa kike dhidi ya waalimu marijali, duuh!

Serikali hazitulii, zinaumiza kichwa namna ya kudhibiti wimbi la ushoga, ulawiti, ubakaji, na madanguro. Na vipi itafanya kuondosha maradhi mabaya ya zinaa ulimwenguni!

Ohoo, niliwahi kusoma kwenye kitabu Fulani Cha dini, kuwa hapo kale ziliwekwa amri kumi Kali Sana, ila ya sita ndio ilizua taharuki na gumzo kubwa ulimwenguni? Hoja Ilikuwa hivi Nani ataweza ishika kwa uadilifu kabisa kabisa? Wakati bado watu wanajiuliza, wakakumbuka taarifa kuwa Sodoma na Gomora ziliteketea kwa Moto kutoka juu, daah!

Sheria hio namba sita bado ipo, na imeongezewa nguvu na sheria Kali za serikali, lakini jinamizi linazidi kushika Kasi nyumba kwa nyumba!

Hivi kwanini Bwana yule asiutoe huu UTAMU usio na tija aliotuwekea kwenye viungo vyetu!

Hivi kweli watu tunaojua umuhimu wa familia tungeshindwa kuamua kuzaa bila huu utamu? Kweli?

Bwana yule anasemwa kuwa ni muweza wa yote, kwanini asiweke utamu huu kwenye ndoa tu, na hivyo akaweka sehemu hiyohiyo uchungu, nje ya ndoa?

Inasemekana kuwa anaudhika saana na haya maovu. Iweje yuko tayari kuishi kwa stress siku zote akishuhudia mabalaa haya yanayomuudhi ilihali anaweza kutengua maamuzi yake kwa sekunde tu?

Hebu atusaidie kwenye hili dogo bhana, ili kuondoa mabalaa haya!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
🤣🤣🤣🤣🤣we jamaaa utamu usitolewe sema magonjwa yafutwe tu paaah UKIMWI, gono, na mengn.... Ndoa ifutwe yaan tukikutana tu ni mwendo wa 🎶kamata chini
Kamatia chini🎶
 
Ya kaisari mpe kaisari ya Mungu mpe Mungu. Ameweka utamu ili mpate kuzaana ninyi wanadamu mnapakatana mtaachaje kufa na magonjwa? mtaachaje kufa na magomvi ya wivu wenu? ndioooo! lazima mfe kwa dhambi zenu. Chochote alichokiumba Mungu, chochote alichokiandika Mungu ukienda kinyume chake unakufaaa!
 
Umepewa chaguo daima hakikisha kuwa kichwa cha chini kinasikiliza amri ya kichwa cha juu,, usipouanika utautwanga mbichi,,
 
Vilio Ni vingi!
Ooh ni viiingi saana!
Hawa wameuana kwa wivu wa mapenzi, huyu amejinyonga, yule anakonda amesalitiwa, mmh makubwa haya!

Kwenye nyumba ile, wazazi hawana amani juu ya watoto wao wa kike! Vischana vimepevuka, vifua vimetuna, vitako vimebinuka tayari. Kwanini Sasa wazazi, hawana amani juu ya maendeleo ya watoto wao wenyewe?

Shuleni Kuna migogoro mikubwa!
Waalimu dhidi ya mienendo ya wasichana. Wazazi wa wanafunzi wa kike dhidi ya waalimu marijali, duuh!

Serikali hazitulii, zinaumiza kichwa namna ya kudhibiti wimbi la ushoga, ulawiti, ubakaji, na madanguro. Na vipi itafanya kuondosha maradhi mabaya ya zinaa ulimwenguni!

Ohoo, niliwahi kusoma kwenye kitabu Fulani Cha dini, kuwa hapo kale ziliwekwa amri kumi Kali Sana, ila ya sita ndio ilizua taharuki na gumzo kubwa ulimwenguni? Hoja Ilikuwa hivi Nani ataweza ishika kwa uadilifu kabisa kabisa? Wakati bado watu wanajiuliza, wakakumbuka taarifa kuwa Sodoma na Gomora ziliteketea kwa Moto kutoka juu, daah!

Sheria hio namba sita bado ipo, na imeongezewa nguvu na sheria Kali za serikali, lakini jinamizi linazidi kushika Kasi nyumba kwa nyumba!

Hivi kwanini Bwana yule asiutoe huu UTAMU usio na tija aliotuwekea kwenye viungo vyetu!

Hivi kweli watu tunaojua umuhimu wa familia tungeshindwa kuamua kuzaa bila huu utamu? Kweli?

Bwana yule anasemwa kuwa ni muweza wa yote, kwanini asiweke utamu huu kwenye ndoa tu, na hivyo akaweka sehemu hiyohiyo uchungu, nje ya ndoa?

Inasemekana kuwa anaudhika saana na haya maovu. Iweje yuko tayari kuishi kwa stress siku zote akishuhudia mabalaa haya yanayomuudhi ilihali anaweza kutengua maamuzi yake kwa sekunde tu?

Hebu atusaidie kwenye hili dogo bhana, ili kuondoa mabalaa haya!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Hawa walimu wa kiswahili wanawadanganya sana, sijui unaficha fasihi simulizi, yani ujinga ujinga, tu.
 
Kwenye suala la ngono tungekuwa kama wanyama tu,yani tunasex pale jike likiwa tayari kubeba mimba,
 
Ngono ni Mindset ni kujiendekeza au kuendeshwa na mihemko...Ukiweza kudhibiti mihemmko umetoboa....Hivi kuna Utamu zaidi ya Kiepe Yai ,Kwio na Pepsi? Au ugali dona na mdudu?
 
Ya kaisari mpe kaisari ya Mungu mpe Mungu. Ameweka utamu ili mpate kuzaana ninyi wanadamu mnapakatana mtaachaje kufa na magonjwa? mtaachaje kufa na magomvi ya wivu wenu? ndioooo! lazima mfe kwa dhambi zenu. Chochote alichokiumba Mungu, chochote alichokiandika Mungu ukienda kinyume chake unakufaaa!
Mungu sio mbabe Kama ulivyoandika hapa!
Kukubali mwanae afe msalabani ni ushahidi tosha kuwa anatupigania tusipotee maovuni!

Tuungane tumuombe kutuondolea huu UTAMU wenye hasara zaidi kwetu kuliko faida!

Back
Top Bottom