AUNT EZEKIEL ACHEZEWA MAKALiO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AUNT EZEKIEL ACHEZEWA MAKALiO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, May 15, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  auntezekiel.jpg
  Na Musa Mateja
  Kitendo cha njemba ambaye jina lake halikunaswa mara moja cha kumchezea makalio staa wa Kiwanda cha Muvi Bongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa', kimezua mtiti wa haja na kusababisha mastaa kutandikana barabara, Risasi Jumamosi lina fulu data.

  Tukio hilo lililofukizwa ubani na ‘mashambenga' wenye majina kunako fani tofauti Bongo na kushuhudiwa na macho na masikio ya gazeti hili, lilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Club Bilicanas, Posta, jijini Dar Jumatano wiki hii ambapo Bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa ikisugua visigino pande hizo.

  Ishu nzima ilikuwa hivi; Aunt na mastaa wenzake wa filamu, Vicent Kigosi ‘Ray', Jacob Steven ‘JB', Hisani Muya ‘Tino', Nice Chande, Juma Chikoka na wengine, wakiwa ndani ya klabu hiyo muda mfupi baada ya Twanga Pepeta kumaliza shoo, alitokea jamaa mmoja ambaye alimsogelea mrembo huyo na kuanza kumchezea makalio.

  Kitendo hicho kilimkasirisha Aunt ambapo aligeuka mbogo mwenye hasira na kumwagia jamaa huyo mvua ya matusi ya nguoni yasiyochoreka gazetini.

  Wakati Aunt akiendeleza libeneke la matusi, ghafla Ray aliyekuwa ‘vere klozi' aliinunua kesi hiyo na kuanza kutiririsha mvua ya maji machafu iliyojaa matusi ya mjini na kwa mbali yale ya kijijini yaliyoambatana na kipigo kikali kwa njemba huyo aliyekuwa akizubaa eneo hilo.

  Jamaa alipoona kipigo kinapelekea kusitisha mkataba wa uhai wake kufuatia chupa kusambaa zikitumika kumtandika kutoka kwa wasanii hao, alichoropoka na kwenda kujichimbia ‘kaunta' ya juu ambapo msanii Tino akiambatana na yule baunsa wa Twanga Pepeta, John Cena walimfuata kisha kumshusha chini.

  Baada ya kufikishwa chini, njemba huyo alifanikiwa kuuona mlango wa nyuma ‘imejensi doo' ambapo mabaunsa walitanda na kuwazuia wasanii hao kuendelea kumfanyizia.

  Katika varangati hilo, Mwana Hip Hop kiraka Bongo, Karama Masoud ‘Kala Pina' alilazimika kutaka kulinunua soo hilo huku akisikika akisema: "Haiwezekani mastaa wangu mkafanyiwa fujo na mimi nipo, itakuwa ni aibu na watu watashangaa kusikia kuwa nilikuwepo."

  Kwa bahati, mabaunsa wa ukumbi huo walifanikiwa kumtorosha ‘mtuhumiwa' eneo hilo na kutokomea kusikojulikana huku akina Ray wakitimka makwao.

  Tukio lingine lililochukua nafasi usiku huo ni lile la kunusurika kuungua kwa Klabu hiyo ya mastaa ambapo kulitokea ‘shoti' ya umeme na kuunguza moja ya televisheni ukumbini humo.

  Shoti hiyo ilisababisha watu kukimbia huku na huko ndani ya ukumbi huo huku wengine wakikimbilia mlangoni, hali iliyosababisha watu kukanyagana na kupoteza vitu vyao, ingawa hakuna aliyeumia.

  Juhudi za polisi wa kikosi cha zima moto ndizo zilizofanikisha kuondoa hofu hiyo baada ya kutia miguu eneo hilo na kuweka mambo sawa ambapo burudani iliendelea kama ‘kawa'.
   
 2. M

  Mkono JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamaa kashindwa kujizuia kama alikuwa anaonekana kama hiyo picha inavyoonekana ! ni sawa tu hata ww inaweza kukutokea.
   
Loading...