Heshima kwako Muhosni.
Mkuu sikutegemea kukutana na bandiko la aina hii tumezoea kusifia watu amabao hawajahi kushika nyazifa zozote za kiserekali [ hata uKatibu kata] lakini utashangaa wanavyovikwa vilemba vya ukamanda,wapiganaji wa ufisadi na nk.Kuna kipindi JF ukitaka kuparuliwa na maneno machafu mtoe kasoro mwanachama wa CHADEMA hata kwamba yaliyo wazi kabisa nakwambia utasahangaa makamanda wenye kumwaga nondo za uhakika wanaweka akili pembeni hawataki kujadili hoja.
Nirejee kwa mheshimiwa A Lyatonga Mrema mbunge wa Vunjo ana mapungufu yake mengi kama wanadamu wengine.Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema amefanya mambo mengi mazuri ambayo watanzania wa kipindi chake kamwe hawatamsahau kirahisi.
Vituo vya vidogo vya polisi ni kazi ya Lyatonga baada ya vituo vikubwa vya polisi kuzidiwa alifanya maamuzi ya kushirikisha wananchi kujenga vituo vidogo vya polisi kila sehemu vilipokuwa vikiitajika.Bahati mbaya baada ya kuondoka kwenye system hakuna aliyeendeleza kazi nzuri aliyoiacha.
Mabasi ya abiria kusafiri mchana ni ubunifu wake,wengi hawajui watu wengi walikuwa wakipoteza maisha kipindi mabasi ya abiria yakisafiri usiku.Baada ya uamuzi wake ajali zilipungua ndiyo maana uamuzi alioufanya zaidi ya miaka 18 iliyopita mpaka leo bado unaendelezwa.
A Lyatonga Mrema alimaliza mapigano ya wameru ambayo yalishamshinda Mzee A H Mwinyi kipindi hicho hali iliyosababisha amzawadie wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu.Wapo watu wanaobeza kwamba wadhifa huo haupo kikatiba lakini wanasahau jambo moja kubwa kwamba katiba ya JMT haimzui rais kufanya hivyo isitoshe Mrema ni mtanzania wa pili kushika wadhifa wa naibu waziri mkuu wa kwanza ni Dr Salimu A Salimu.
Hivi kumbe mjadala huu ni Mrema Vs Dr. Slaa!
Kwa taarifa yako tu 1995 matokeo ya NCCR:National Convention for Construction and Reform 1,406,343 21.83% wabunge 16 viti maalum 3 = 19
Kusema kwamba ni Mrema aliyesababisha haya ni dharau kwa waasisi wa mageuzi.
Kuanza 3 year sio hoja, kina Keneth Matiba wa Kenya walihitaji miaka mingapi??
mjom
https://www.jamiiforums.com
Mrema is being honour DOCTORATE by a South African University for his contribution to tanzania politics in general. he will be called Dr.Augustine Mrema
A truly living legend.......
Mwalimu aliona mbali kutuepusha na huyu baba. Sielewi kabila yake walikuwa wanajiandaa kumtumiaje. Tulioziona kampeni zake zilivyogeuka kuwa za kabila moja tuliogopa sana.
Is this true?? kindly confirm!