MAMLAKA ya Udhibiti wa Uthibitiwa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini nchini (Sumatra) imesema kuwa kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu mabasi ndogo yanayobeba abiri chini ya 25, maarufu kama 'vipanya', hayataruhusiwa kutoa huduma jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Sumatra, mabasi yanayota usafiri jijini Dar es Salaam (daladala), yatakayoruhusiwa ni yale yanabeba abiria zaidi ya 25 ili kupungunguza msongamano wa magari jijini.
Sambamba na hatua hiyo, Sumatra imeagiza kuwa mabasi yatayasajiliwa kutoa huduma hizo lazima yawe mapya au yaliyotumika si zaidi ya miaka mitano tangu yalipotengezwa, kwa lengo la kulinda usalama wa wasafiri na kupunguza ajali.
Katika kuboresha na kudhibiti usafiri jijini, mamlaka hiyo pia imesema daldala zitakazopewa leseini, wamailikiwa wake watalazimika kuunda kampuni ambazo ndizo zitajulikana kisheria kuwa ndizo zinazotoa huduma hiyo jijini badala ya kila mtu kuwa na basi lake kama ilivyo sasa.
Licha ya agizo hilo kutokuwa jipya, tunaipongeza Sumatra kwa kuweka tarehe maalumu ya kuanza kuteleza ilichokuwa ikisema kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, kama kweli wamedhamira kufanya hivyo na kuhakikisha kuwa walichopanga kinatekelezwa.
Lego la kuhibiti msongamano wa magari jijini ni hatua muhimu katika jijini la Dar es Salaam kwa sasa, kutokana na kuongezeka kwa magari katika barabara nyembamba zilizojengwa miaka mingi iliyopita.
Ni dhahiri kwamba, kuwepo kwa vipanya jijini, licha ya kuawasidia wananchi, vimekuwa vikisabisha msongamano wa magari usio wa lazima kutokana na wingi, pamoja na mchezo mbaya wa madereva kutumia njia za mkato kuyapita magari mengine (kuchomekea).
Si hivyo tu, hatua ya kuwataka wamailiki wa daladala kuungana na kuunda kamapuni za usafirishaji, inasaidai kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa sheria za barabarani na utovu wa nidhamu unaofanywa na baadhi ya madereva na makondakta wa daladala dhidi ya wasafiri na hasa wanafunzi.
Kuna baada madereva ambao wanasababisha ajali kwa makusudi, kutokana na tabia zao za kuchomekea na wengine kuwanyanyasa na kuwadhalilisha abiria, kisha hukimbia namabasi yao.
Hivyo tunaamini kuwa mabasi hayo yakisajailiwa chini ya kampuni vitendo hivyo, vitakuwa rahisi na usafiri utapatikana kwa urahisi na hadhi inayotakiwa, kama ilivyo katika nyingi duniani.
Tunaamini kuwa kama usafiri wa daladala utaimarishwa na kufikia viwango bora, watu wengi na hata wanaomiliki magari madogo watalazimika kutumia usafiri huo, ili kupunguza msongamano zaidi jijini, kwa sababu mazingira hayo yanaweza kuwezesha kuwepo kwa mabasi makubwa yaendayo kasi.
Hata hivyo tunaishauri Sumatra ihakikishe kwamba hatua hiyo inaanza kufanya kazi kukiwa na mabasi ya kutosha, ili sije ikasababisha kero kubwa kwa wananchi na wanaafunzi wanaokwenda kazini na shukeni.
Pamoja na hayo, tunaomba kuanzia sasa Sumatra na mamlaka zote zinazohusika yafanyike maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza utekelezi wa amri hiyo kwa haki na kutoa upendeleo kwa baadhi ya wamiliki a mambasi hiyo.