Auawa kwa wivu wa mapenzi

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
MWANAMKE Sharuna Gimon (30) ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kutokana na wivu wa kimapenzi wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Advocate
Nyombi alisema kuwa tukio hilo ni la Machi 19 mwaka huu, saa 4 asubuhi katika kijiji cha Ndaga Wilayani Rungwe.

Aidha alieleza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mwanamke huyo kufumaniwa na dereva na mkazi wa kijiji cha Ndaga, Yohana Mwazanga (35) ambaye pia alipata majeraha na amelazwa katika hospitali ya Igogwe kwa matibabu.

Kwa mujibu wa Kamanda Nyombi polisi inawashikilia watu wawili kuhusu tukio hilo na
upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Bahati Musa (35) na Jofrey Hezron (21) wote wakazi wa kijiji cha Ndaga wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Dah mbombo ngafu...................
 
Back
Top Bottom