Aua naye kauawa

Aua naye kauawa

Kibwagizo

Senior Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
130
Reaction score
8
mtu anayesadikika kuwa mweu amemuua kijana kwa kumchoma visu mjini Mwanza jirani na msikiti wa Ijumaa,kutokana na hasira za nzengo naye kapigwa mpaka kauawa.Tuki hili limetokea majira ya saa 9:15

Source:mimi mwenyewe
 
Mwee! huyo chizi akifika akhera akapimwe akili!
 
duh.. mi naogopaga sana nikikutana na kichaa barabarani maana huwezi jua siku hiyo kaamka vipi, sema ndio vile kwa sababu nao ni binadamu hatuwatengi na jamii ila ni hatari sana
 
pole kwa kushuhidia vifo. taarifa zaidi kuhusu marehemu hao chanzo cha vifo hivyo ni nini? kulikuwa na ugomvi wowote kati yao ?
 
duh.. mi naogopaga sana nikikutana na kichaa barabarani maana huwezi jua siku hiyo kaamka vipi, sema ndio vile kwa sababu nao ni binadamu hatuwatengi na jamii ila ni hatari sana
Duh? Mkuu umenikumbusha majuzi (J/pili) nilipishana na chizi akiwa anavuja damu mdomoni, tulipo karibiana ghafta akaanza kukunja ngumi nami nikakunja nikawa namfuata ili nimuwahi kabla ya yeye kuniwahi (ugomvi kuwahiana) Ghafra akilizangu zikabadilka nakunituma nitoke nduki na kweli nilikimbia nakumuacha amefura kwa hasira huku matusi yakimtoka. Nilivyo fika mbali nikawa najiuliza, Ivii kama wangetokea watu nakuona napigana na chizi tena akiwa anavujwa na damu wangenichukulia hatuagani? Ivii kama angeniwahi yeye (sijui kama alikua na siraha) ingekuaje? nilijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu la maana. Nishukuru usafi niliokua nao siku hiyo ndio ulio niokoa maana nilihofia asije kuni chafua.
 
pole kwa kushuhidia vifo. taarifa zaidi kuhusu marehemu hao chanzo cha vifo hivyo ni nini? kulikuwa na ugomvi wowote kati yao ?

Inasemekana kijana amekuwa muhudumu katika mgahawa maeneo yale. mahuti yamemkuta nje ya mgahawa akiwa kwenye shughuli yake ya kusambaza chai kwa wateja wa nje na mgahawa gafra akakutana na huyo chizi ameshikilia kisu ndipo akaanza kumchoma visu sehemu mbali mbali za mwili wake.
 
Inatisha,wana jamii hii taarifa mbichi na hata mimi niko eneo la tukio nafuatilia ni kwa nini jamaa aliamua kuua kabla na yeye kuawa..
 
Duh? Mkuu umenikumbusha majuzi (J/pili) nilipishana na chizi akiwa anavuja damu mdomoni, tulipo karibiana ghafta akaanza kukunja ngumi nami nikakunja nikawa namfuata ili nimuwahi kabla ya yeye kuniwahi (ugomvi kuwahiana) Ghafra akilizangu zikabadilka nakunituma nitoke nduki na kweli nilikimbia nakumuacha amefura kwa hasira huku matusi yakimtoka. Nilivyo fika mbali nikawa najiuliza, Ivii kama wangetokea watu nakuona napigana na chizi tena akiwa anavujwa na damu wangenichukulia hatuagani? Ivii kama angeniwahi yeye (sijui kama alikua na siraha) ingekuaje? nilijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu la maana. Nishukuru usafi niliokua nao siku hiyo ndio ulio niokoa maana nilihofia asije kuni chafua.

hahahAa Hahahaaha hahahahH Hahaaha We jamaa.yaelekea mtata sana.
 
Imenikumbusha kuna chizi mmoja alikua na njaa, akaenda kwenye mgahawa na kusimama katikati ya mlango mkono mmoja kakamata panga na mkono mwengine kakaamata rungu, kisha akasema 'sijui nile kwanza au niue Kwanza' ama watu wote ndani walitoka mbio waliompenya, waliomsukuma.
Kumbe jamaa alikua na shida na chakula tu kuona watu washatoka akatafuta meza 1 akakaa akapiga msosi then akaondoka zake.

BTW, rip marehemu
 
hahahAa Hahahaaha hahahahH Hahaaha We jamaa.yaelekea mtata sana.
Mkuu, me nimtu mstaarabu sana ispokua sipendi kuletewa za kinyonge (kionewa) nikotayari kuzichapa hata mbele ya familia yangu (mke na watoto)
 
WAKUU!!Habarini za mchana?.

Taarifa zilizonifikia muda mfupi uliopita kutoka mwanza zinaeleza kwamba mtu mmoja amekufa maeneo ya Msikiti wa Ijumaa Mwanza asubuhi ya Leo baada ya kuchomwa na kisu.

Baada ya kuchomwa kisu alianguka na kufa papo hapo kisha aliyehusika na tukio akakimbia lakini wananchi wakamkimbiza wakamkata Ngwala na kuanza kumshambulia kwa mawe na kumponda ponda vibaya naye akafa hapo hapo.

Mwisho wa siku aliyeua naye kauawa!hii ndiyo Dunia yetu ilipofikia!

Picha zitawajia baada ya muda mfupi kadri nitakavyokuwa nazipokea,wenzetu wa Mwanza wakina Pwaaaa,Thinker,na wengineo wengi wa huko wekeni hali halisi ilivyokuwa.
 
aliyemchoma kisu mwenzake alikuwa kada wa ccm,na aliuwawa hapohapo!
 
vizia vizia utupe hata store kutoka kijiwen ni ugoni au siasa zimewauwa hawa jamaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom