yaani Tz kila kitu karaha hata fedha zako mwenyewe! Ila mashine za kuweka fedha kaka italuwa ngumu kwa hali hii ya wahusika wa wizara ya fedha kupenda 10% katika uchapishaji wa fedha! Kama unakumbuka kipindi cha Mramba kuna hela zilichapwa na kabla ya hapo maelezo yalikuwa kemkem ati hela zitakuwa si rahisi kughushi mara ohoo kipofu ataweza tambua sijui nini sijui kile sijui hiki! zilipotoka Lahaula hata miezi miwili haikuchukua choka mbivu zimechakaa!
mashine za kuwekea pesa nchi za nje ndo hizo hizo atm za kuchukulia pesa........pia huduma nyengine kama kubadili pesa kuwa za kigeni, ku transfer money into an account in a different bank, kulipa bills kwenye account
na kila kitu kinafanyika automatic.......
Tanzania pia kunatakiwa hizo mashine za automatic, sio akae mtu ndani kupokea kibahasha. kwa kuanzia wanaweza kufanya mashine zilizoko sasa zikaweza pia kupokea pesa
mkuu....atm za kuweka hela ziko aina nyingi,nyingine wakati wa kuweka inatoa bahasha ambayo unajaza details zako na kiasi cha fedha then unaweka hela zako ndani ya bahasha kisha unatumbukiza bahasha kwenye mashine.huko ndani[bank] mtu anafanya process yote ya confirmation,tatizo la hii ni kuwa kama bank haina watu waaminifu kama wabongo wateja watadhulumiwa kwa kuambiwa waliweka hela pungufu au bandia.....mimi nishawahi kuweka hela kupitia hii mashine nikasahau sifuri moja yaani badala ya 300 nikaweka 30,bank walinipigia simu kuniuliza uliweka kiasi gani nikawaambia amount wakaniambia nilipokosea wakasort,sasa pata picha kosa hilo umefanya CRDB/NMB etc....
mie najua atm za kupokea na kuweka pesa ni automatic hakuna mtu wa kupokea wala kuweka ...........
labda sikukuelewa hapo kwenye maandishi ya red na blue ..............fahamisha tafadhali
anhaaa...................hiyo nchi uliyoko imenishangaza kwa kweli huo mfumo wao
nizijuazo mimi ziko hivi sasa
unaingiza cash card............select deposi.........una enter amount........ panafunguka ki-draw..... unaweka hela yako, mashine inazihesabu kabla hakijajifunga hicho ki-draw, inakuambia umeweka pesa sawa na uloandika if not inakwambia ingiza zaidi au anza mwanzo kama umekosea.
ukimaliza hapo inatoka risiti ambayo inakwambia umeweka pesa ngapi na kwenye account therefore zimekuwa pesa ngapi.
ukipenda una update kitabu chako unaondoka
hakuna uwezekano wa kuandika pesa nyengine na ku deposit nyengine .....................hiyo ndo niliyo iita mimi full automatic
mie najua atm za kupokea na kuweka pesa ni automatic hakuna mtu wa kupokea wala kuweka ...........
labda sikukuelewa hapo kwenye maandishi ya red na blue ..............fahamisha tafadhali
Lol...haya mambo ya kuiga haya!! Hivi hizi ATM zimekuja lini Tanzania? Maana naona zinaleta mushkili sana kwa watu....