Atlas Primary School - Madale, Dar

Msikivu umesema.. ni nani asiyemjua..mtu anayetukana wazazi parent day... ndo unamwita msikivu huyo..


Pole sana kama alikutukana. Mimi alinisikiliza vizuri sana na kwa adabu kabisa . Nakushauri umripoti Polisi kuwa amekutukana ili sheria ifuate mkondo wake.
 
Msikivu umesema.. ni nani asiyemjua..mtu anayetukana wazazi parent day... ndo unamwita msikivu huyo..

Naomba mumpeleke kwenye vyombo vya sheria. Kutukana ni kosa la jinai na kuto kumshitaki ni kuzuia sheria isifanye kazi yake.
 
Msaada wa kimawazo khs kumuhamisha Mwanangu atlas ya madale kutokana na changamoto za hostel zao,na kuna mwenye kufahamu iwapo naweza kupata uhamisho wa mtoto wa std 7?
Unaweza kumwamisha.. bado hawajasajiliwa kwa ajili ya mtihani wa la 7
 
Usiseme "Sitaki kuja kulia kutokana na Ujeuri wao...."... Sema " Sitaki kuja kulia kutokana na Upumbavu wao...!". Wanachofanya na Upumbavu na Ujinga, Mkuu![emoji34][emoji34]
 
Jamani Mie naishi Sinza,
Natafuta shule maeneo ya Karibu, yaani Sinza, Kijitonyama, Makumbusho, Ubungo, Mwenge, Magomeni, Kinondoni, etc,
Mtoto anaingia Darasa la Kwanza Mwakani,
Shuleiwe vizuri Kitaaluma, Ada na Usafiri iwe reasonable angalau isifike au kuzidi 1,800,000/= ndio uwezo wangu,
Kwa Mzazi mwenye kujua shule ya aina hii msaada please
 
Hivi ni kweli Atlas ilifutiwa matokeo na wanafunzi darasa la saba kufanya mtihani mwingine kwa jina la shule nyingine. Ina maana watoto kuamshwa alfajiri saa kumi baada ya kunguni kuwatafuna na kulazimishwa kuingia prep ya alfajiri walikuwa wana fanya mapitio ya paper. Kama hivyo ndivyo adhabu gani wamepewa waliovujisha hizo paper. Inamaana jeuri ya Rugambwa inatokana na imani kuwa atapitisha wanafunzi wote kwa alama A na kuendelea kujaza watoto chumba kimoja cha darasa watoto mia na hamsini. Watoto wana kula nje iwe jua iwe mvua yeye anajali kuongeza madarasa na idadi kubwa ya kupokea wanafunzi. Sasa imefungiwa miaka mitano ni wazi atatumia jina lingine kuandikisha wanafunzi. Baadhi ya walimu wanalia kuto lipwa mishahara miezi kadhaa. Nashauri utawala wa shule ufanye mabadiliko makubwa. Wizara ichunguze nini na nani walisababisha shule kupata paper zote ili wawajibishwe.
Sipendi wanafunzi waliobaki waathirike na ubazazi wa watu wapigaji.
 
Sunrise hapo mikocheni, ni mzur sana pia.
 
Ni kweli ilifutiwa matokeo wakarudia mitihan yao shule ingine,
Na wamefungiwa kama kituo cha mitihan kwa muda usiojulikana mpaka hapo Serikali itakaporidhika na mwenendo wake.
Hili Mmiliki hawezi kuwatangazia wanafunzi au kuliweka wazi maana litamuharibia biashara. Ndio maana hata kwenye matokeo ya Darasa la Saba hawapo hawa jamaa.
 
Ndalichako Aione Hii Habari
Wizara ya Elimu ibashughulika Na usafiri wa Mabasi? Hilo swala la mabasi pelekeni wizara ya uchukuzi wizara ya Elimu haina mainjinia wa kujua basi la shule Zima au bovu
 
vip kwa sasa jamani bado wapo hivo hivo au washabadilika ....mana nshalipa pesa ya semister moja juz tu kwa ajili ya mtoto wa nurser ndo nakutana na hii taarifa humu
 
Vipi kuhusu kufutiwa matokeo kwa mtihani wa utimilifu darasa LA 7 mwaka huu 2018???
Au bado umebakia na wanafanya vizuri sana kitaaluma????
Kuna mtu katuroga sio bule
 
My dear mtoto anakaa kwa azizi ali unamleta madale? Mbona mbali sana si angeenda hata ya ubungo?
Huyu sijui anamkomoa Huyo mtoto??? Kwa azizi Ali temeke mpaka atlas madale???!
Labda kama anasoma bure ila kama na ada unalipa kama inavyotakiwa tatizo sio madereva tatizo ni wewe na wanafanya makusudi ili umuamishe mwanao maana yawezekana anatoka saa 10/alfajili kumfuata mtoto mmoja kwa Aziz Ali then anavuka bugurun na mwanao pekee akifika maeneo ya tabata ndio anaanza kuwaokota
 
Grade 3 na grade 1 kwa watoto ni suala LA wiki 1 zimezid sana 2 atakuwa kundini acheni kukariri wakuu.
Kutoka kwa Aziz Ali mpaka atlas madale??? Bora apate changamoto ya kwenza mazingira mapya unless mtese mtoto kwa miaka 7 ???????!!!!!!!!!!
Siyo lazima ila kuna madhara anayopata mtoto kuhama shule moja kwenda nyingine. Loosing friends na kwenda ku adapt mazingira Maya. Nadhani unalitambua hilo
 
Yaani utoe mtoto mdogo Ubungo kumpeleka Madale, hiyo shule wanapandikiza ubongo mpya kuliko aliozaliwa nao? Wakati mwingine sisi wazazi tunahangaika na upuuzi!
 
Hata kama anasoma bure, simpeleki mwanangu shule ya mbali kiasi hicho. Ni ujinga wala sio maarifa...
 
Hii ni zaidi ya undezi, eti mfumo wao wa elimu ni mzuri, mzuri kumshinda mwanangu na uhai wake? Kuna watu wana watoto lakini hawakufaa kuwa wazazi. Wangu alisoma hapo std 1 na 2, na alianza hapo baada ya mamake kushauriwa na rafiki zake. Mie nilikuwa nje kwa kipindi kirefu so masuala ya shule mamaa ndo alikuwa mfuatiliaji. Mwaka wa pili nilishuhudia hayo magari yao na pale shuleni kwao nikajiongeza taratiibu! Nipo kibamba na mwanangu anasoma kiluvya kwa komba. Amekua sana ki taaluma kwani no stress za usafiri. Na ikitokea hitilafu ya usafiri muda ukapita wa kurudi nyumbani wazazi mnapewa taarifa kwa baba na mama/mlezi kwa pamoja, lengo ni taarifa ipatikane kwa wakati keupusha mtafaruku. Mazingira ya shule+ mfumo ni mzuri pasi na kifani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…