TANZIA Atilio Tagalile, Mwandishi mkongwe na mdau wa JamiiForums afariki dunia

Pole kwa wafiwa.

Umenichekesha sana mkuu,

Juzi Kuna mama wa kinyakyusa nilikua nazungumza naye anilikua anaitikia tu mmh mhh ejo ejoo .
Hahahaaahahaha. Dah umenichekesha sana. Poleni wafiwa,njia yetu Ni moja
 
RIP.nakumbuka Radio Chanel afrika miaka Ile ya 90's.akiwa na wenzake akina William njelanje,Maximilian bushoke,na wengine wengi.kazi ya mungu Haina makosa.
 
View attachment 1846430

Wakuu, hizi ni taarifa mbaya.

Mwandishi wa habari mkongwe Atilio Tagalile ametutoka usiku wa kuamkia leo!

Alilazwa kwa wiki moja. Awali Hindu Mandal kisha Rugambwa hadi umauti ulipomfika saa sita ya usiku wa kuamkia leo.

Alikuwa mwandishi, mchambuzi na mkufunzi wa wengi. Aliwahi kufanya kazi Radio Channel Africa na Sauti ya Ujerumani (DW). Aidha, alifanyia kazi magazeti ya Daily News na The Citizen.

Tagalile alikuwa miongoni mwa wanachama wa JF (ambao niliwajua at a personal level).

Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani
Amin
 
Back
Top Bottom