Ati nini?unasemaje dokta?

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Mr.marwa aliagizwa na dokta apeleke hospitali choo ndogo kwa ajili ya vipimo.Alipofika home aliandaa sampo yake ya haja ndogo kwenye kichupa kidogo,akaiweka juu ya kiti,akaingia chumbani kujiandaa kwenda hospitali.Mwanae bhoke kwa utundu wake akaigonga ile chupa,mkojo ukamwagika.Mama bhoke kuona hivyo,ili kumuepusha mwanae na kipigo kikali,akachukua kichupa,akaenda chooni,akaijaza mkojo wake mwenyewe,kisha akairudisha faster ilipokuwa.Baba bhoke alipofika hospitali,dokta alipima ile sample,akavua miwani,akamtazama vizuri mr.marwa kisha akamwambia,'MATOKEO YANAONYESHA UNA MIMBA YA MIEZI MIWILI!',tabiri kilichotokea sekunde tatu baadaye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom