Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Atheists tulionekana wa ajabu sana!

Mara kwa mara huwa nasema kuwa suala la mungu ni la imani,lakini huwa hamnielewi mnasema imani sio tatizo.

Lakini kama imani isingekuwa tatizo kwenu usingesema et kama mungu angekuwepo(suala la imani) kusingekuwepo nadharia za kuwa hakuna mungu,yani ulitaka suala la imani ya mungu liwe sawa na mtu aseme kuwa anaamini kuwa rais wa Tz ni Magufuli.

Watu kuamini au kutoamini mungu isikuchanganye maana hili ni jambo la imani,kinachotakiwa ni kwani unaamini au kwanini hauamini.
Hivyo wewe kutoamini mungu sikwamba una akili sana.
Hapa ni jukwaa la Intelligence ndio maana tunataka kuelewa na siyo kuamini......Kama unataka kuamini, nenda jukwaa la Dini/Imani.
 
......MUNGU hakumuumba shetani ili autese ulimwengu bali ni baada ya shetani kuasi ndipo laana ya MUNGU ikashuka juu yake,
Kumbuka uharibifu wa kwanza ulianzia mbinguni na hii ni baada ya Shetani kuasi.
Mbona kila siku tunaipangua hoja yenu lakini hamelewi?.......Kama Mungu alijua Shetani atakuja kuasi,...kwanini alimuumba?
 
Hapa ni jukwaa la Intelligence ndio maana tunataka kuelewa na siyo kuamini......Kama unataka kuamini, nenda jukwaa la Dini/Imani.
Basi wewe ambaye hutaki kuamini imekuaje unabishania jambo la imani wakati wewe hutaki kuamini?

Hebu nieleweshe(usiniaminishe) kuwa hakuna mungu.
 
Basi wewe ambaye hutaki kuamini imekuaje unabishania jambo la imani wakati wewe hutaki kuamini?

Hebu nieleweshe(usiniaminishe) kuwa hakuna mungu.
Ilikuelewa kitu inabidi tutumie milango mitano ya fahamu.....sasa Mungu hafit hapo.
 
kata tiketi ya ndege, mkiruka mkiwa juu kabisa, halafu itokee hitilaf kidogo.... chungulia dirishani.... hali izidi kuwa mbaya ... ukiwa huna matumaini tena..... utajikuta unatamani kuwa karibu na huyo unaejidanganya hayupo.. utajikuta unatoa matamshi ya sauti na kimoyomoyo ya kumuomba akuokoe.

nnachojaribu kukuambia ni kwamba hata kama utapenda iwe hivyo,binadamu hayuko huru ,amefungwa na matakwa ya Muumba wake. ruka ruka wee na hako kaubongo ulikojikuta tu unako, utarudi tu kwake.
God is Real.
Yaani wewe bwana... unawaza kitoto... ni wa ngapi katika mazingira hayo wametaka kuwa karibu nae. But they are gone..... una maana ukiamini Mungu ndio haufi??? au... there is no difference or favour katika nature....yakikukuta hayana msalie mtume its either u believe or u dont believe...
 
......MUNGU hakumuumba shetani ili autese ulimwengu bali ni baada ya shetani kuasi ndipo laana ya MUNGU ikashuka juu yake,
Kumbuka uharibifu wa kwanza ulianzia mbinguni na hii ni baada ya Shetani kuasi.
What is the conclusion... Mungu ameshindwa kupambana nae. Kama shetani alikuwa na ugomvi yeye mbona katuletea sisi. Si angemalizana nae??? Mbona anamlea hivi mpka anakuwa na kiburi??
 
Ilikuelewa kitu inabidi tutumie milango mitano ya fahamu.....sasa Mungu hafit hapo.
Kumbuka kuna Agnostic,sasa wewe atheist unayetaka watu waelewe kuwa hakuna mungu je,ni mlango gani wa fahamu ambao unatumika kuelewa kuwa hakuna mungu?
 
Wakuu salama, Kwanza kabisa nianze kwa kusema Elimu pekee ndio itakayomkomboa Mwanadamu katika sayari hii, Uwezo wa kutatua changamoto upo ndani yake mwenyewe, Hakuna Msaada wowote utakaotokea anga za juu kuja kusaidia hapa Dunia Hivyo Binadamu ni Mungu tosha kabisa ni Maarifa na yanazidi kupanuka na kukiweka Huru kiumbe Hichi, Miaka kadhaa nyuma Baadhi ya sisi atheists humu tulionekana watu wa ajabu kwa imani Yetu kuwa Hakuna Mungu, Mkuu Kiranga ana thread moja imefikisha almost 3K Comments za Believers wakimshambuliwa kwa matusi nae akiwajibu kwa hoja.

Taswira ya Jf sasa iko tofauti kabisa Watu kiukweli wametoka kwenye vifungo na kwa sasa wengi ni Free thinker ata kama Anaamini katika Mungu ila yuko tayari kusikiliza sera za wasio amini na kuchambua kidogo.

Tuliwahi ongea apa kwamba Mungu huyu tunaemsoma makanisani au Misikitini Hawezi kuwepo hata kwa bahati mbaya mana sifa tunazomjaza hayuko nazo hata punje .NakaribiSha mijadal zaidi.

Cc Free ideas Doyi Kiranga nusuhela @Areta ludovick Kifyatu
Mimi nitakubaliana na kuwepo na Energy fulani ambayo hata kwenye Geo wanaisema kama Aliens sababu kuna structures ambazo kwa akili ya binadamu unajiuliza walizijengaje na wakati huo wa primitive age? Imani za kuwa kuna jua linachomoza na utakuta kuna imani nyingi za kuiabudu jua hivyo there is something there. Kuna hii ya watu kutokewa na Mama Bikra Maria je mama hawezi kuwa kati ya Aliens? What is aliens? Wagerumani yaani nazis wanadai wenyewe wametokana na huo uzao as well as the top class ya wahindi na wahindi wana history ndefu ambayo imeandikwa. Je yawezekana wapo hawa watu?
Koo za Wahima na wahabeshi wanadaiwa wanauhusihano na hawa viumbe na ndo waliwaweka watutawale. Ukisoma mapokeo ya watu wa far East na hata middle east kabla ya kristo. Hivyo kuna nguvu na nguvu hizi zinatuyumbisha na wanadai zinatumia uranium kusafiri. Tuwaulize waliofanya utafiti wa Kabba je lile jiwe jeusi limetokana na nini? Nijibu kwa utafiti siyo mihemko ya dini sababu mimi siyo mdini.
 
Mimi hata grup langu la chuo wananiona wa ajabu hasa pale ninapo wapinga live kuhusu huyo mungu.
Lkn kwasasa naona kuna baadhi wamebadilika na kuwa open mind.

Mwanzon unaonekana km jiti lililokosa adabu, lihuni lkn kadri unavyowatemea facts wakaanza kunielewaa.

Sasa tunaheshimiana na wengi kwasasa hawajishughulishi na mambo ya imani km zaman


Usijidanganye Mkuu, kitu ushindwacho kukithibitisha haimaanishi hakipo bali upeo wako mdogo ndio umeshindwa kutambua uwepo wa kitu hicho.
 
Kuvaa nguo na kuonesha staha hakika ni kusonga mbele, je kuletewa dini ambayo baadaye ilitumika kama kigezo cha kupitisha ukoloni ni kusonga mbele?
Hiyo pia ni moja wapo ya maendeleo. Karibu Nchi zote duniani zimewahi kutawaliwa. Na hivi leo nchi ambazo zimeshawahi kutawaliwa ndio zipo top katika maendeleo. Nchi chache sana ambazo hazijatawaliwa na ndizo zipo chini sana kimaendeleo.
 
Mungu hakuletwa kama usemavyo, Mungu alikuwepo katika kila jamii, lugha, jamaa, taifa na dunia kwa ujumla.
Unachojaribu kueleza ni kuwa watu walichanganya utamaduni na ubinafsi katika Kumtafuta na kumuabudu huyu Mungu.

Pia jamii moja kutaka kujitofautisha na jamii nyingi kulingana na mazingira na maumbile ndivyo vilivyopelekea Mungu aonekane kagawanyika.

Ukweli ni kwamba Mungu ni yule wa wote mwenye uweza japokuwa jamii zimemmilikisha Fulani zimemmilikisha na baadhi ya mataifa kumtaifisha huku baadhi ya watu kumbinafsisha. Jambo hili limefanya jamii nyingi kuchanganyikiwa.

Mfano wa watu waliojaribu kumbinafsisha Mungu ni pamoja na Waisrael ambao kupitia kitabu cha historia yao ambacho wengi hukiita kitabu kitakatifu "BIBLIA". Husema;
Mungu wa Ibrahimu, Isaka na yako, huku ni kumbinafsisha Mungu wa wote. Na ikiwa Mungu angekuwa wa Mtu mmoja mmoja basi ni wazi asingeweza kuwa wa Ulimwengu mzima.

Vitabu vya Biblia hasa Agano la kale, viliandikwa kiokombozi zaidi. Ukombozi pekee uliokusudiwa ulikuwa ni ukombozi wa taifa la Israel katika dunia hii. Hata alieandika vitabu vya mwanzoni kabisa alikuwa ni Mwanamapinduzi au Mkombozi wa awali wa taifa hilo. Mwanamapinduzi huyo na mwanaharakati ambaye aliitwa Nabii ili kwa malengo mahususi ndiye aliyeanzisha Vuguvugu kwa taifa hili ambalo lipo katika msuguano mpaka leo.

Nabii Musa mwanamapinduzi ndiye aliyeandika vitabu vitano vya awali katika biblia, aliandika vitabu hivyo kwa mtindo wa ubinafsi kwa taifa lake.
Nasema kwa Ubinafsi nikiwa namaanisha kabisa kutokana na baadhi ya visa vilivyomo katika vitabu vyake.

Aidha kuna kisa cha Yakobo na Esau ambacho kinaonyesha dhahiri lengo la mwandishi wa vitabu hivyo. Yakobo ambaye ndiye Israel aliutwaa ukubwa kwa Esau ambaye ni Baba wa waEdomu. Kisa hicho cha kusisimua kinaonyesha lengo kamili la mwandishi ambalo ni ubinafsi kwani Yakobo hakuwa na khaki yoyote ya kupata baraka ama kurithi katika familia ya Isaka. Musa akiwa mwanzilishi wa Kitabu cha Biblia kwa maandishi yake ndiye mtu aliyeleta mgogoro wa Uwapo wa Mungu.

Mfano wa Pili ni Wa Isaka na Ishimael.
Ubinafsi wa mwandishi katika kutetea asili ya mababu yake aliweza kuudhihirisha. Kisheria Mtoto wa kwanza hasa wakiume ndie anayetakiwa kuwa mrithi wa Mali.

Mtunzi Musa alijua kabisa Ishmael sio wa Taifa lake hivyo kumtukuza lilikuwa ni jambo baya sana kwake. Ukisoma kwa makini aya za kisa kile unaona jinsi Mungu alivyokuwa upande wa Ishmael.

Kama mtoto wa nje yaani wa mtumwa hajri hawezi kuwa Mrithi ilikuwaje kwa Yakobo na Wake zake wanne ambao kila mmoja alipata gawio katika nchi ya Kanani.

Biblia inasema kuwa Ibrahimu atabarikiwa na kuwa taifa kubwa lakini mtoto wake mmoja ambaye ni Ishmael ambaye ni wakwanza anafichwa kabisa pamoja na watoto zake wengine kwa mkewe Ketura. Watoto hawa wa ibrahimu Historia yao inawekwa kapuni na mwandishi Wa kitabu cha Mwanzo katika Biblia. Huku watoto wa Yakobo(Israel) wakiibuka kidedea katika historia. Moja ya sababu kubwa ni kuwa Mwandishi Musa alitoka katika moja ya makabila ya Israel hivyo huenda aliandika kwa ubinafsi au kwa kutojua ama kufuatilia vizuri historia ya vizazi vingine vya Ibrahimu.

Jambo jingine ambalo Musa alililenga si kumtangaza Mungu kama baadhi ya watu wadhaniavyo. Musa alishindwa kuandika mambo ya Msingi ikiwemo Asili ya mwanadamu. Ameelezea juu juu chimbuko la mwanadamu kana kwamba hakuona umuhimu wake. Pengine tusimlaumu kwa kutoelezea chimbuko lake kwani huenda hata yeye hakujua au hakuwa na taarifa muhimu zenye manufaa.
Musa alishindwa kuelezea Kwa kivipi Watoto Wa Adamu walivyopata wake zao.
Pia watu wengine walitoka wapi ambao Kaini aliogopa wasije wakamuua.

Mwandishi huyu pia alitumia lugha ambayo kimsingi huweza kumletea utata mtu mwenye akili ndogo au kubwa. Kwa mfano kitendo cha kusema Nyoka akamdanganya Hawa bado kinautelezi katika fikra za watu wengi.
Iweje nyoka amdanganye hawa wakati hakupewa uwezo kama binadamu aliye mfano wa Mungu.

Lugha ya mafumbo ya kitabu cha Mwanzo huwagawa watu katika makundi mbalimbali. Wapo wanaoachwa solemba kwa akili ndogo na wapo wanaotoa tafsiri kulingana nauwezo mkubwa wa akili zao.

Kwa mfano ikiwa wapo wanaofikiria kuwa nyoka alikuwa ni Shetani huku wakijiona wapo sawa basi hata wale wanaoona Tunda lilikuwa ni uchi au sex huenda nao wakawa sawa.

Musa hamtaji Shetani Mara kwa Mara jambo ambalo linazua utata. Mara nyingi hutumia watu Kama wachawi, waganga, wanajimu n.k. Jambo ambalo hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa huu ni Uchawi au ni muujiza. Na upi ni Mungu na upi ni washetani. Kwa bahati mbaya wote husema wanamtumia Mungu. Hivyo kila upande humwona mwenzake ni Mchawi atumiwaye na Shetani.

Musa alijikita kuelezea Historia ya taifa lake na kusahau historia ya mwanadamu. Ndio maana naweza kusema Musa alisahau iwe kwa kujua au laa kusimulia habari muhimu za asili ya mwanadamu.

Dunia ipo hivi Leo kwasababu ya Musa, japokuwa kuna Imani nyingi lakini nyingi zinaamini kulikuwa na Adamu na Hawa.

Historia ya mwanadamu ikiwekwa sawa ndio ukweli kuhusu Mungu kuwepo haitakuwa na Mashaka.

Mungu yupo sema waandishi ndio huongozwa na athari mbalimbali katika kumwelezea hivyo hujikuta wakiacha maswali mengi kwa kuacha kusimulia baadhi ya matukio ya Msingi.

Musa alikuwa na athari ya elimu za kimisri hivyo lazima umakini uwepo katika kusoma habari zake na lengo lake na nafasi yake.
 
Mbona kila siku tunaipangua hoja yenu lakini hamelewi?.......Kama Mungu alijua Shetani atakuja kuasi,...kwanini alimuumba?
........alimuumba ili kuthibitisha uweza, nguvu, na mamlaka yake kwa mwanadamu
 
Hiyo pia ni moja wapo ya maendeleo. Karibu Nchi zote duniani zimewahi kutawaliwa. Na hivi leo nchi ambazo zimeshawahi kutawaliwa ndio zipo top katika maendeleo. Nchi chache sana ambazo hazijatawaliwa na ndizo zipo chini sana kimaendeleo.
Hakuna nchi itakayoendelea kwa kutegemea mawazo ya kutoka nje, tamaduni za nje, hata teknolojia za nje. Nchi huendelea kwa kukuza, kulinda na kuheshimu tamaduni zake hapo tunakuta lugha na teknolojia ya eneo husika hii inamaanisha hata kuasili lugha ngeni kinaweza kua kikwazo cha maendeleo.

Hizo nchi zilizoendelea hebu angalia kiwango chao cha kuona ikiwa Mungu yupo au hayupo mfano nchi za Scandinavia.
 
Kumbuka kuna Agnostic,sasa wewe atheist unayetaka watu waelewe kuwa hakuna mungu je,ni mlango gani wa fahamu ambao unatumika kuelewa kuwa hakuna mungu?
It's either black or white! there is no something intermediate like gray!......You are either Atheist or Theist.
 
What is the conclusion... Mungu ameshindwa kupambana nae. Kama shetani alikuwa na ugomvi yeye mbona katuletea sisi. Si angemalizana nae??? Mbona anamlea hivi mpka anakuwa na kiburi??
.........To prove his existence almighty God allowed Satan to destroy your mind so as atheist would accept Existence of God through your Delivery..
 
Back
Top Bottom