Atheism ni nini?

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,646
Reaction score
9,619
Ipo mijadala humu jukwaani kuhusu Atheism! Kwa bahati mbaya nimejaaribu kuifuatilia bila kufata maana halisi! Kwanza wachangiaji wanatumia kiingereza kigumu sana na wengi ni walewale.

Ukweli ni kuwa tupo wengi tusioelewa, Ombi langu kama nitaweza kupata maelezo ya undani kwa kiingereza rahisi kama sio kiswahili!
 
 
 

weka kichwa chako huru kisha soma hapa: Atheism - Wikipedia, the free encyclopedia utapata idea.
ukirahisisha ni kama unawatu wawili, unamuuliza wa kwanza, "unaamini kuna mungu?", akijibu ndiyo inamaana ni theist, anaimani kwamba kuna mungu. wa pili unamuuliza vilevile akijibu "hapana, siamini kama kuna mungu" huyo ni atheist, a non-believer, haamini kama kuna mungu. nadhani umepata picha.
 
Hapo nimepata mwanga maana nilinisumbua sana! MaAtheist maarufu ni akina nani?
 
Hapo nimepata mwanga maana nilinisumbua sana! MaAtheist maarufu ni akina nani?

Atheist maarufu ninaowafahamu mpaka sasa ni hawa

1. Richard Dawkins- huyu ni mwanabaolojia kwa kiasi kikubwa ni muumini wa evolution ya Darwin. Kaabdndika machapisho na vitabu vingi huku kitabu cha God Dellusion kikimpa umaarufu kwa kuuza mamilion ya kopi! Ana documentary nyingi you tube!!

2. Lawrence Kraus-Huyu naye ni mwanasayansi ambaye ameandika kitabu kinachoitwa "Something from nothing"...katika kitabu hiki anajaribu kuelezea chanzo cha ulimwengu pasipo kumuhitaji mungu...kuna conversation yake na Dawkins Youtube..utajifunza mengi!! Kraus kashafanya midahalo mingi sana na theists kuanzia US, UK mpaka Australia...na karibia midahalo yote amekuwa akiwashinda opponents wake!!

3. Kiranga- Huyu amejipambanua humu Jf kama mtu anayepinga nadharia ya mungu bila uoga wowote, licha ya kejeli anazokumbana nazo bado amekuwa abadili msimamo, na kikubwa anachoitaji ni uthibitisho wa madai ya theists ambayo mpaka leo wameshindwa kuyathibitisha!
 
Last edited by a moderator:

Uungu wa Mungu umejithibitisha kwenye hayo maneno bila wao kujua hasa kwenye hayo maneno 'magically' na 'rearranged itself' hakuna kitu kinachofanyika chenyewe bila nguvu fulani! ni kushindwa kubaya sana huko kwa kusema vilitokea na kujipanga vyenyewe ukisoma BIBLIA takatifu inakupa mwanga kuhusu hilo hasa kwenye kitabu cha mwanzo mstari wa kwanza....Hapo mwanzo alikuwepo neno(conscious energy) naye neno alikuwepo kwa Mungu(conscious mind) naye neno alikuwa Mungu(conscios energy + conscious mind = conscious soul) na huu ndio utatu mtakatifu usiofahamika hata na wasomi mahiri wa elimu zote
 

Umeongea maneno yenye uzito sana. Mwenye ufahamu na afahamu
 
I think it is wrong ku-argue na atheist ukianzia katika msingi, wao ni God-haters. Na ndio maana mijadala huwa haiishi.

Kwanini nasema hivyo, mfano: I hate Nigerian movies mie kuhate Nigerian movies does not mean hazipo, zipo ila sizipendi.

So ukisema atheist ni God-haters hiyo ina maanisha jamaa hawa wanajua kuwa Mungu yupo ila wanamchukia au hawamtaki, hiyo sio sahihi.

Atheist wao wanajua kuwa Jamaa hayupo na ukija ukamwambia yupo basi njoo na uthibitisho.

Kwahiyo basi, ni muhimu sana uje na uthibitisho kuwa mwenyezi yupo na sio maelezo ya kumsuuza roho asiwe hater awe lover…

Hiyo ndio namna yak u-argue nao ni kuwapa uthibitsho uliosimama kweli kweli.
 
Hoja mbili kubwa ndizo zinatupelekea sisi kuamini uwepo Mwenyezi Mungu.
1.Asili ya ulimwengu...wote tunakubaliana na msingi wa out of nothing, nothing come...ma-atheist wanasema ulimwengu haujatokana na kitu chochote.lakini haiwezekani ulimwengu huu na hali yote hii ijitokee tu.
2.suluhisho la moral objective value...theism ina msingi mzuri wa morality kama love your neighbor as yourself katika msingi huu unapata ukarimu, upendo...lakini atheist wanasema sisi ni mashine tuliotokana na DNA ..!! Wao ni very confusion...mfano.simba akimrarua swala anakuwa na hatia..hivyo hivyo ngombe dume akimrukia jike anaambia amebaka kwa hiyo human being tuna utaratibu na suluhisho la kiulimwengu ni kumuamini uwepo Mungu wa Ibrahim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…