Atheism: Imani nusu na robo

Sasa kinashindikana nini kufanya hayo mazuri ya dini nje ya dini?
 
Lipi baya ambalo linafanywa na wenye kuamini dini tu?
 
Hakika Mkuu.

Kama yupo kweli basi ana roho mbaya sana na hana upendo na watu wake.

Mfano tetemeko lililotokea bukoba angezuia lisitokee kwa sababu anajua kila kitu.

Lakini kuwaokoa watu wake lakini amewaacha wameumia sana.
Hivyo ndivyo ambavyo umelitafsiri wewe tukio la tetemeko la ardhi,lakini kwa wanaoamini mungu wanalitafsiri vyengine.
 
Post ya kawaida kabisa hii imegeuka mtifuano mkali kati ya imani mbili waamini na wasioamini
 
Mabaya gani ambayo watu hutumia vitabu vya dini kuyafanya?
 
Acha mawazo mgando wewe. Wazee wako wa kale mbona walikuwa na sheria kali dhidi ya uzinzi licha ya kuwa walikuwa hawamjui huyu mungu na sheria zake?
Hizo sheria Kali zimewekwa endapo utakiuka utaadhibiwa,sasa ikiwa kwenye dini unajua hakuna mungu kipi kitakuogopesha kuacha kuzini au kuiba au hata kuuwa?

Hata mimi huwa nawaza along the same lines...
 
Hizo sheria Kali zimewekwa endapo utakiuka utaadhibiwa,sasa ikiwa kwenye dini unajua hakuna mungu kipi kitakuogopesha kuacha kuzini au kuiba au hata kuuwa?
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?

Hujajibu hili swali.
 
Hvi ww huoni aibu kuendelea kuandika huu upumbav mwenzio anakwambi vtu vya maana ww unaandika ujinga na upumbav
Neno la msalaba kwao wapoteao ni upumbavu bali kwetu sisi tunaoamini ni nguvu kubwa iletayo wokovu. So sioni shida kwa comment yako hii. Barikiwa.
 
Hizo sheria Kali zimewekwa endapo utakiuka utaadhibiwa,sasa ikiwa kwenye dini unajua hakuna mungu kipi kitakuogopesha kuacha kuzini au kuiba au hata kuuwa?
Ukiona huwezi kuacha maovu au mabaya kwa sababu ya kukosa vitisho au thawabu basi ujue wewe bado hujakua kifikra na hauna tofauti na mtoto mdogo. Grow up.
 
Hakuna baya lolote unaloweza kulifikiria ambalo mtu hwezi kutumia kitabu cha dini kulifanya.
Nitajie wewe hilo baya japo moja ambalo mtu anaweza kutumia kitabu cha kufanya baya hilo.
 
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?

Hujajibu hili swali.
Sijajibu kvp?
 
Ukiona huwezi kuacha maovu au mabaya kwa sababu ya kukosa vitisho au thawabu basi ujue wewe bado hujakua kifikra na hauna tofauti na mtoto mdogo. Grow up.
Hakuna sehemu ambayo hakuna sheria na adhabu kwa ataekiuka sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…