Athari za TFF kutoa ruhusa klabu za Ligi Kuu Kusajili Wachezaji 12 wa kigeni

kwa hatua hii bila shaka itauwa vipaji vya soka la vijana wetu kwani ni wazi sasa vilabu havitakuwa tena na mda wa kupoteza wa kulea vijana ili hali kuna soko tayari nje nje la vijana kutoka nje waliolelewa vizuri na wapo tayari kutoa matokeo mazuri (ikumbukwe lengo kuu la wamiliki wa vilabu vikubwa vilivyochangia sana sana kupitishwa kwa kanuni hii ya wachezaji 12 yaani SImba na Yanga wao wanaangalia zaidi katika kutengeneza faida zaidi na kurudisha pesa yao i,e MO & GSM.

Kanachoshikitisha ni kwamba TFF ya sasa inaongozwa na watu wasio na uwezo wa kudadavuo mambo kwa manufaa ya Taifa mbele (namzungumzia Rais wa sasa wa TFF) mungu wangu! "Kitumbo" sijui hata elimu yake ni kiasi gani lakini hata ukimsikia anavyoongea ni mtu asiyejua nini anachoongea basi tu kwa kuwa aliwekwa pale na ""usalama" basi yeye amakuwepo pale akisikiliza matakwa ya wakubwa waliomuweka pale kumpeleka peleka.

Hitimisho ni kwamba ligi yetu itaonekana bora Afrika kwa mda kwa sababu ya "influx" ya wachezaji wa nje lakini soka letu la bongo litaendelea kudidimia mpaka atapotokea Waziri wa michezo mwenye akili na sio huyu wa sasa "mnyambo" mwenye akili "kamasi" anayepelekwa pelekwa kwa kila jambo.
Wewe unataka tukumbatie wachezaji wa ndani tuendelee kukaa tulipokuwa? Mbona klabu ni nyingi watapata nafasi na wakipandishwa klabu kubwa wajitume zaidi.
 
Soko ya Tanzania ilikufa alipoondoka Marcio maximo enzi hizo zambia ilisawazisha mchezo ukawa droo ikawa kama wameshinda Kwenye michezo ya caf .

Sasa hivi imebaki biashara kati ya Tff na vilabu .
Italy kiwango cha wachezaji wa kigeni ni 7 kwenye timu moja
 
Nakupongeza kwa maoni na mtazamo wako, tofauti ya wachezaji wawili kwa msimu ujao ndio utawezesha hilo?10 players tulishindwa nini? Wachezaji wa kigeni ni hasara kwa taifa hili, kwanza hao makocha wana mkakati wamepewa wa kuwanoa wazawa na sharti la kuwapa namba au wako huru kuamua wapangeje first eleven zao, mapato na matumizi ya hao wachezaji wa kigeni uwiano ukoje? mfano mauzo ya jezi OG wanamvuto wowote?je wanatumika kibiashara? Malengo mafupi, ya kati na muda mrefu ya kusajili hao wageni kwa vilabu, ligi, na tff ni yapo, na je kuna review program ya kuangalia matarajio ya kuwa na wageni kila msimu na tathimini ya mrejesho ipo? Hivi tuna uhalali wa kujifananisha na mataifa yapi na kwa vigezo vipi kwa faida ipi na malengo yapi na je hayo ndio yafananayo na tunaotaka kufanana nao?
Mkuu umeandika vitu vingi au maswali mengi sana kwenye comment yako kiasi kwamba hadi imepoteza mantic ya mada, maana sidhani kama mtu ataweza kujibu maswali yote hayo kwa wakati mmoja

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
 
Kocha wa yanga analalamika eti kwa nini wasiruhusu wachezaji 10 wa kigeni kwa wakati mmoja.

Hapa kati utopolo walikuwa wanapiga kelele timu yao inajitosheleza.

Leo benchi la ufundi linalialia.
 
Kocha wa yanga analalamika eti kwa nini wasiruhusu wachezaji 10 wa kigeni kwa wakati mmoja.

Hapa kati utopolo walikuwa wanapiga kelele timu yao inajitosheleza.

Leo benchi la ufundi linalialia.
Nimemsikia lakini Hana hoja tayari madhara ya kutolewa mapema wanayaona anasahau idadi iliongezwa kutokana na maombi ya vilabu kushiriki kimataifa
 
Back
Top Bottom