SoC02 Athari za kiuchumi katika familia

Stories of Change - 2022 Competition

Josephaty Jumapili

New Member
Feb 1, 2022
2
0
Jamii nyingi za kiafrika zimekumbwa na matatizo mbali mbali katika familia kama:-

1: Ndoa kuvunjika
2: Baba kukimbia familia
3: Vijana kukataa mimba
4: Watoto kuugua magonjwa yatokanayo na ukosekanaji wa vyakula bora nk.

Ukosekanaji wa huduma bora katika familia hutokana na kukokuwepo kwa vyanzo maalum vya kipato katika familia hiyo. Familia nyingi zimekuwa zikiishi kwa taabu itokanayo na kukosekana kwa fedha ambazo ndio msingi mkuu wa mahitaji katika maisha.

Kijana anapoingia katika MAHUSIANO au NDOA pasina kuwa na misingi mizuri ya kuweza kumpa pesa kwaajili ya huduma katika familia au kwa mwenza wake, huleta matokeo mabaya kama kukataa mimba kwa hofu ya gharama wakati wa kujifugua mwenza wake, ama kukimbia familia kwa lengo la kutegemea jamii iliyomzunguka ndio itoe msaada wakati yeye akiwa hayupo.

Vile ukosekanaji wa kipato katika familia hureta athari nyingine kama ndoa kuvunjika,tatizo kubwa likiwa ni kukosa kwa huduma muhimu katika familia ambazo vyanzo vyake vikuu ni fedha.

Sisi kama vijana tutambue kabla yakuwaza kuwa na faimilia bora,basi tutafute vyanzo vizuri ya kipato ambavyo vitatuwezesha kuhudumia familia hizo katika ubora ili ziweze kuwa bora! Kuwaza au kifikiri kuwa na maisha mazuri ni ndoto ya kila mtu duniani,ila kutekeleza na kufikia malengo hayo ni juhudi ya mtu binafsi.

Wakati mwingine tunapitia matatizo sababu tulifanya maamzi bila kujali hali zetu binafsi! Familia bora inajengwa na Uchumi imara, Upendo, Mshikamano, Umoja nk.

NB: Maisha ya uzeeni ni matokeo ya ujanani, tutafute pesa kwaajili ya maisha yetu na familia zetu. Hakuna familia inayokuwa mfano bora katika jamii kama familia iliyo fanikiwa kiuchumi!!
 
Back
Top Bottom