#COVID19 Athari za Covid kwa uzazi wa wanaume - Utafiti wafichua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

පිරිමින්ගේ සරුභාවයට කොවිඩ්වලින් බලපෑමක්

Ni miaka miwili sasa tangu virusi vya Covid vigundulike duniani na baadaye kuwa janga, lakini ni sasa ambapo uwezekano wa athari za ugonjwa huu kwa uwezo wa kuzaa wa wanaume zimefichuliwa.

Ingawa kuna baadhi ambao hawajapata chanjo kutokana na hofu kwamba chanjo dhidi ya Covid-19 itapunguza au kumaliza uwezo wa uzazi, utafiti wa hivu karibuni umebaini kuwa wanaume wenye ugonjwa corona wamepungukiwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wa uzazi.
Utafiti ambao ulihusisha wanaume 120 wa Ubelgiji ambao walipona maambukizi ya Covid, waliochunguzwa chini ya mwezi mmoja baada ya kupatikana na maambukizi ya corona, asilimia 60% kati yao walikuwa wamepungukiwa na uwezo wa kusafiri kwa mbegu zao za kiume za uzazi.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi miwili baada ya maambukizi ya covid, asilimia ya wanaume waliopungukiwa na uwezo wa mbegu zao za uzazi ilikuwa imefikia 37% na miezi miwili baadaye ilikuwa ni 28%.

Utafiti huo pia ulibaini kuwa ujazo wa mbegu za kiume miongoni mwa wanaume ulipungua baada ya kupata maambukizi ya Covid-19.

Male birth control pills

Wakati Covid ilipopimwa katika kipindi cha mwezi mmoja wa maambukizi, ilibainika kuwa kiwango cha idadi ya mbegu za uzazi kilikuwa cha 37% miongoni mwa wanaume walioshiriki utafiti kilikuwa kimepungua pia.

Utafiti ulibaini kuwa 29% ya wanaume walikuwa wamepungukiwa idadi ya mbegu za kiume kati ya mwezi mmoja na miezi miwili baada ya maambukizi, na miezi miwili baadaye, 6% ya wanaume walikuwa wamepungukiwa mbegu za uzazi za kiume.

Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la masula ya Uzazi na uwezo wa kuzaa.

Ingawa mabadiliko ya kiwango cha joto la mwili kutokana na ugonjwa kama wa homa ya mafua yanaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa mbegu za uzazi za kiume, watafiti wanasema kwamba kwa ugonjwa wa Covid, mafua yanaweza kutokana na utendaji fulani wa mfumo wa kinga mwili badala ya kuongezeka kwa viwango vya joto la mwili.

Watafiti wanakadiria kuwa tatizo hilo litaisha na mbegu za kiume kurejea kuwa katika hali ya kawaida baada ya miezi mitatu.
Hatahivyo, tafiti zaidi zinafanyika kuthibitisha hili na kubaini iwapo kuna madhara ya kudumu miongoni mwa wanaume wachache waliougua covid.

Mwezi Mei mwaka jana, utafiti kuhusu Covid kuhusiana na uzazi wa wanaume ulichapishwa kwenye jarida la Asia - Asian Journal of Andrology.

ඩිම්බ කෝෂ තැන්පත් කිරීම

Utafiti huo uliojumuisha wanaume 41 ambao walikuwa wamepona Covid, pia ulibaini kuwa jumla ya idadi ya watu waliokuwa na maambukizi ya Covid, kongamano la mbegu za uzazi, na hatimaye asilimia kupanda zaidi kuliko kundi la wale ambao hawakupata maambukizi ya Covid-19.

Utafiti ulifanyika kwa takriban siku siku 56 baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini kwa wagonjwa wanaume baada ya kuugua Covid.
Tafiti hizi pia zilibaini kuwa athari hizi zilibainika kuwa juu zaidi wakati walipopimwa mara ya pili siku 29 baadaye.

Uzazi wa kiume​

Kulingana na Shirika la afya duniani, sababu zinazosababisha zaidi wanaume kukosa uwezo wa kuzaa ni matatizo ya kushindwa kumwaga mbegu za kiume, kiasi cha chini au cha chini zaidi cha kiwango cha mbegu, na pale mwanaume anapokuwa na umbo lisilo la kawaida la mbegu za uzazi.

Kulingana na makala iliyochapishwa mwezi Januari katika jarida la kitabibu la The Lancet, kukosa uwezo wa kuzalisha kwa mwanaume huchangia karibu 50% ya wanandoa au wenzi wanaohangaika kwa kukosa uzazi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Mizungu haina nguvu yakupelekea moto hata kabla ya UVIKO
 
Hakuna kitu kama hicho.

Watafiti waje niwapige miti tuone kama hawatapata mimba na sijachanja.

Naomba hao watafiti niwape mimba huku sijachanja ili kupingana na utafiti wao.
 
Back
Top Bottom