KERO ATCL wamepoteza mzigo wangu, na ukienda ofisini kwao hawatoi ushirikiano

KERO ATCL wamepoteza mzigo wangu, na ukienda ofisini kwao hawatoi ushirikiano

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Niliagiza mzigo kutoka dar kuja kigoma jana tar 15/08/2025 kupitia ATCL kutokana na uharaka niliokuwa nao, ambapo mzigo huo ulifikishwa saa 4 asubuhi na ratiba ya ndege ilikuwa inaonyesha inaondoka saa 7 mchana ilikuwa inafika kigoma saa 10.

Jioni nimeenda kufuatia mzigo huo nikaambiwa haukutoka dar, hivyo napaswa kusubiri hadi jumapili.

Nikapata mawasiliano na watu wa parcel dar wakasema mzigo huo umetumwa, nikabaki njia panda maana kigoma wanasema mzigo haupo na dar wasema mzigo umetumwa.

Kwa sababu cargo wa dar walisisitiza waliutuma, wakanishauri nirudi leo asubuhi.

Leo asubuhi nikarudi airport kigoma, majibu ni yale yale na wanajibu kwa dharau tu kuwa hawana cha kufanya na hawajui cha kufanya.

Nikarudi kuwapigia simu watu wa parcel dar hawapokei simu zangu na mwingine ni kama ameniblock kabisa maana tokea asubuhi simu yake ipo busy.

Sasa wameniingiza hasara maana kazi ya mzigo huo imeisha.
 
Back
Top Bottom