ATCL saga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATCL saga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Manyi, Jun 7, 2012.

 1. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wadau,

  Nasikitika kwamba badala ya mimi kushangilia maamuzi ya waziri, kwa hili naomba nionyeshe masikitiko yangu makubwa hasa kwa mtu muelewa kama Dr Mwakyembe. Alichokifanya mh huyu ndo yale yale ambayo yalilalamikiwa nab w Lowasa wakati ule, maamuzi ambayo hayatokani na utafiti bali mujungu na kutafuta kuonekana kutenda hata kama unafanya madudu.


  1. ATCL kwa mara ya kwanza mefanikiwa kupata ndege ya kukodi kwa bei chini ya wastani wa bei ya soko (block hour rate below market standard) ambayo kama nakumbuka vema ni USD 1,700 wakati soko liko USD 2,400
  2. Kwenye mkataba huu ambao wakubwa wanasikitika kupigwa chenga ya mkataba ambayo kwa kawaida ndiyo sehemu ya ulaji wa wakubwa wetu, umeondoa yale mazoea ya kulipa kishika uchumba (down/advance payment) ambayo nayo huwa inachakachuliwa na wakubwa. Badala yake hii ya sasa ni kulipa kutokana na matumizi based on block hour usage
  3. Market penetration yao ambayo return ticket ya KIA ni tzs 199k (against 340k ya PW) na Mwanza tzs 199k (tzs 420 ya PW) ambayo kwa wale wanaotumiwa na wazito wa PW, wameona ATCL ni threat at least kwa hizo routes mbili.
  4. Majungu kwamba ATCL management amepokea hela nyingi na kuzifuja during month of May ambapo mpaka waziri na naibu wake walinitembelea hapa J3 asubuhi na kuwapa ukweli bayana (as we are the only banker of ATCL) and yet wamekwenda kufanyia kazi fitna na mujungu
  5. Paul Chizi ambaye alikuwa sourced from Community Air, being of less than 5 Tanzanians who pocess an MBA in Aviation, leo mnasema vifungu vilikiukwa na ukweli unafahamika mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu…So, wa kuwajibika ni Eng Chambo ambaye ndiye alikuwepo Aug last year wakati Paul Chizi anapewa nafasi ya kukaimu u-CEO wa ATCL.
  6. ATCL kulaumiwa kulipa deni la Ultimate Security above $0.9m wakati kesi iliamuliwa na mahakama ya biashara Mar 2011 ambapo uongozi huu haukuwepo madarakani, ATCL hakuwa na pesa na hivyo serikali kupitia barua ya Eng Chambo kucommit kulipa deni ambalo hata hivyo kila wakiandikiwa barua wanapotezea kwa zaidi ya mwaka. Matokeo last week ATCL amepata mpunga wa malipo ya bima ya ndege iliyotembelea tumbo Kigoma, mdeni akawahi mahakamani na kuleta zuio la hela benki (garnishee nisi) na tumezuia pesa ambapo ATCL amerejea mahakamani kuomba kesi itizamwe upya na kukubaliana payment plan, yet wanasemwa kuwa wametumbua pesa.
  Tunabaki tunakurupuka kama kawaida yetu na kuishia kuwaonyesha watanzania kwamba kukosoa kumbe ni rahisi kuliko kuongoza. Tunaishi kwa majungu na utafutaji wa njia za mkato wa kupata umaarufu kwa wananchi.


  Natamani kama ningeyasema haya ana kwa ana badala ya kuyaandika. Lakini naona mazingira hayaruhusu. Binafsi nimefuatilia hili sakata toka early last week, nimeketi na watendaji wakuu wa ATCL, Wizara na mpaka juzi waziri na naibu wake. Ajabu sana, narudia tena ajabu sana uvumi kwamba nia ni kumg'oa Chizi ili awekwe ndugu wa mh toka nyumbani kwetu Mbeya nilikuwa nayo toka 28 May 2012. Mwisho wa siku ndicho kilichotokea.

  Stanbic ndo sole banker wa ATCL, sasa mtu anaposema kuna fedha zimefunjwa wakati ATCL hajawahi kuwa na hela ndani ukiachilia ka-OD kadogo ambako tuliwapa ili waweze kuwa wanalipia mafuta PUMA Energy, maelekezo ya kulipa tumekuwa tunafanya wenyewe hapa ndani, pesa pekee walopata mwezi May ni ya mshahara toka serikalini few millions. Then mtu anasema wamefuja?!?

  Unless mtu anambie kuna pesa ATCL alikuwa anapelekewa cash na serikali pale ofisini kwao, kitu ambacho ni non sense.Wadau,

  ==> Si maneno yangu wana jamvi, bali ni maneno ya mdau wa karibu wa Stanbic<===
   
 2. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,015
  Likes Received: 2,630
  Trophy Points: 280
  Haya tena,thanks mkuu kwa kutuchambulia haya ambayo tulikuwa hatuyajui hasa mie maana sijui wenzangu watakuwa na maoni gani,tuendelee kuvutavuta muda maana wengi bado wanapata Lunch.
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  bora kutenguliwa kwa kutenda mema kuliko kuharubu heshima na utu wako,

  paul chizi ni mzalendo na watanzania tumeona hilo.
  as for mwakyembe,kila lifanyikalo gizani huonekana kwenye nuru,ngoja tuone uteuzi mpya wa binamu ytaleta nini!
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu mdau ndie amekurupuka, alichofanya Mh. Waziri ni ni kutengua uteuzi wa Mr. Chizi ambao ulikiuka sheria husika, na wala sio kwa makosa ya ulaji unaouzungumzia. Hao watendaji wengine wamesimamishwa kupisha uchunguzi na kama hakuna matatizo haki itendeke, sasa wasiwasi wa nini?

  Imefikia mahala watu tunapewa ku-KAIMU nafasi hata mtu hajathibitishwa akiambiwa atoke inakuwa nongwa?
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  I know Paul Chizi tangu alipokuwa Engineering Dept ya ATCL kabla haijafa na alipokuwa Manager wa ATCL Jo'rburg. Lakini sishangai Mwakyembe kumwondoa Chizi, nina uhakika Mwakyembe amevutwa na hulka za kikabila tu. Sijui aliyeteuliwa na Mwakyembe, bila shaka ni M-Kyela mwenzake au mtu kutoka Mbeya.

  Paul chizi is full grown in aviation industry from engineering to marketing to operation....It is too bad that this country is running on its own bullshit!
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi kukaimu si kama probation!
  After all chuya na mpunga vitajulikana baada ya uchunguzi sasa hawa wanaolalama wakati uchunguzi bado what do u mean?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwani aliteuliwa tu kutoka nyumbani au application zilifanyika?
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Niifananishe na nini siasa ya Tanzania? Nitaifananisha na upele wa mgongoni. Unawasha lakini kukuna unashinda mpaka upate mti. Tena niifananishe na nini siasa hii? Nitaifananisha na na nzi wa wadogo wanaotua usoni na machoni huku ukiendesha baisikeli. Nzi hawa hata ukiwafukuza kwa mkono hawatoko badala yake inabidi usimame tu ili uwafukuze. Inakera sana!
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Chizi anataka kuwa kama Maige kwa style tofauti sasa
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  utachunguza pasipo na tatizo,wanamaliza kodi zetu kwa kuchunguzana upuuzi.makosa yanaonekana lakini wachunguza,haya chizi hana hatia anachunguzwa,pesa izo jamani hizo tume hazifanyi kazi bure ni kodi za wananchi na mie nikiwemo.
   
 11. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kama chunguzi nyingi zinafanyika na zinaishia kuandika majungu, je hapa itashindikana?
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndaga fijo.
   
 13. D

  Don The Great Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Well Said, i believe they will turn back to him.Afterall huyo Lusajo is acting as well tuu. Baada ya haya manung'uniko ya watu wengi huku na i believe Dr mwakyembe naye huwa anasoma huku, namuomba atumie busara zake kumrudisha Mr. Chizi as an appointed CEO and not acting.Tujiulizeni kwanini Community airline ilikufa?Ni kwa sababu ya strategies zao za fare ndogo,watu wakaipiga chini.And nani alikuwa MD wa Community airline kwa wakati huo?Alikuwa Mr. Chizi(He knnows well marketing ya haya mambo ya aviation ndio maana alianza kufanikiwa na kazi yake anaijua ipasavyo.Hivi ni vitu vingapi ambavyo vinawagusa watanzania moja kwa moja na vikiguswa tuu,mkono wa mtu unaingia.Haya mashirika inabidi tuyafungie novena ili yaweze kuamka(ATCL,TRL,UDA,NMC etc).MUNGU atudaidie tuu tuweze kuepuka na hiki kipindi kigumu tulicho nacho kwa sasa.
   
 14. n

  nrashu Senior Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hamjasomeka kabisa.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Paul Chizi amewachishwa kutokana na utaratibu mbovu wa kumuajiri. Kuna uwezekano mkubwa kabisa akarudishwa kwa kufuata taratibu ili baadae kusiwe na malalamiko.

  Sioni ubaya wa kusimamishwa mtu kwa kuwa aliajiriwa bila taratibu kufatwa na ikiwa taratibu zitafatwa na yeye ana qualify kama taratibu zikifatwa sioni sababu kwanini asiajiriwe tena.
   
 16. n

  nrashu Senior Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo ni moja tu. Haya mashirika yote ni bomba la kupitishia fedha kwenda destination fulani.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Guys, huyu jamaa kafukuzwa au kasimamishwa kazi?
   
 18. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,069
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  hayo ni maneno yako. Mwakyembe alicho sema ni kwamba "ajira yake haikufuata taratibu za kuajiriwa" anaweza akawa amefanya mengi lakini mwakyembe anacho taka ni kufuatwa kwa taratibu za ajira.
  Unaweza ukawa unajua kuendesha gali vizuri lakini kama hauna leseni trafiki lazima akukamate.
   
 19. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ..kazi kwelikweli! Bila hata kupoteza muda wa kufikiri "kumteua mtu wa kabila lako, ndugu yako" ktk nafasi yeyote ila wakati wa mtafaruku inatia shaka, hata kama waziri alikuwa na nia nzuri ila kwa hili kachemsha!
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa watanzania siku hizi wakisikia fulani kasimamishwa basi wanashangilia, wanampongeza aliyemsimamisha kazi mwenzake naku "condemn" yule aliyesimamishwa hata kama mtu hana ushahidi wowote. Yani kesho kwenye gazeti itoke waziri wa fedha kasimamishwa na rais basi wtau watashangilia utafikiri nini sijui.

  Tujifunze kwamba sio mara zote anayesimamishwa ndiye mkosaji, na kusimamishwa kunawezakuwa kwa sababu nyingi. Mara nyingine ni uwajibikaji wa kawaida kwa makosa yaliyofanywa na wa chini yako. Tusiangalie performance ya mawaziri kwa kuangalia amesimamisha wangapi walio chini yake! kama ilivyo sasa ambayo naona imewafanya mawaziri wawe busy kutafuta nafasi za kuwatoa watu kafara ili wao wapate ujiko kwa ajili ya 2015!
   
Loading...