ATCL kuwaleta wachina 200 kila wiki nchini

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
319
Reaction score
755
Shirika la Air Tanzania limeingia kwenye makubaliano na kampuni ya China iitwayo Touchroad International Holdings Group, ili kutangaza sekta ya utalii Tanzania kwa kuwasafirisha wageni wa kitalii kutoka Hangzhou China na kuwaleta moja Kwa moja hapa nchini kwa kutumia ndege ya Air Tanzania aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Kwa mujibu wa makubaliano, safari hizo zitafanyika kila wiki ikiwa na wataliii sio chini ya mia mbili (200) na Safari ya kwanza itaanza mwezi wa nane mwaka huu.
 
Ila uongo , huwezi kupata watalii wa kichina 200 kila wiki lands kidogo wazungu
 
Shirika la Air Tanzania limeingia kwenye makubaliano na kampuni ya China iitwayo Touchroad International Holdings Group, ili kutangaza sekta ya utalii Tanzania kwa kuwasafirisha wageni wa kitalii kutoka Hangzhou China na kuwaleta moja Kwa moja hapa nchini kwa kutumia ndege ya Air Tanzania aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Kwa mujibu wa makubaliano, safari hizo zitafanyika kila wiki ikiwa na wataliii sio chini ya mia mbili (200) na Safari ya kwanza itaanza mwezi wa nane mwaka huu.
 
Tuache kudanganyana watalii wanatoka Ulaya na Marekani. Sio China wala India.
 
Watalii wa kichina....lets wait and see
Sure; kuna wanaoweza kuja kama watalii wa Kichina halafu wakazamia uchochoroni na kufungua magenge ya kupika chakula ya mama ntilie!.
 
Shirika la Air Tanzania limeingia kwenye makubaliano na kampuni ya China iitwayo Touchroad International Holdings Group, ili kutangaza sekta ya utalii Tanzania kwa kuwasafirisha wageni wa kitalii kutoka Hangzhou China na kuwaleta moja Kwa moja hapa nchini kwa kutumia ndege ya Air Tanzania aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Kwa mujibu wa makubaliano, safari hizo zitafanyika kila wiki ikiwa na wataliii sio chini ya mia mbili (200) na Safari ya kwanza itaanza mwezi wa nane mwaka huu.
Aisee ni short term plan ama ni endelevu? Kwahiyo kwa mwezi litafanya safari NNE zenye jumla ya wavimba macho 800... Kwa hesabu za haraka ukiuza kila tiketi kwa bei ya juu ya USD 1500 utapata wastani wa USD 1.2... M... Ambazo ni sawa na 2.5B kwa makisio ya haraka
 
Sasa piga picha, hizo zote zidisha mara 10, halafu unampa ndugai akalipie matibabu yeye peke yake
 
Watu wanaangalia services

Binafsi bora nipande reputable company kwa masafa marefu
 
hivi safari za namna hii yale sijuii ma "landing laits" , ma "aiata" na yale sijui ma laiti tlaki na nini hua yanawekwa pembeni ??
 
Hao watalii wa hivyo wasitue Dar tafadhali, wapelekwe moja kwa moja Burigi...wakitoka huko moja kwa moja Gwanzuuu
 
Back
Top Bottom