ATCL kuwaleta wachina 200 kila wiki nchini

ATCL kuwaleta wachina 200 kila wiki nchini

Hii ni fursa njema ila inabidi tujifunze na kupika vyakula vyao maana wanapenda mbwa, nge, na vyura
La sivyo watakula mpaka mawe tukiwaachia kila kitu
 
Kuna vitu vinatija Ila kwanini wachina?

REA wamepewa wachina, biashara ndogo ndogo wachina hata hili nalo daah kweli shida
Shirika la Air Tanzania limeingia kwenye makubaliano na kampuni ya China iitwayo Touchroad International Holdings Group, ili kutangaza sekta ya utalii Tanzania kwa kuwasafirisha wageni wa kitalii kutoka Hangzhou China na kuwaleta moja Kwa moja hapa nchini kwa kutumia ndege ya Air Tanzania aina ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Kwa mujibu wa makubaliano, safari hizo zitafanyika kila wiki ikiwa na wataliii sio chini ya mia mbili (200) na Safari ya kwanza itaanza mwezi wa nane mwaka huu.
 
Sure; kuna wanaoweza kuja kama watalii wa Kichina halafu wakazamia uchochoroni na kufungua magenge ya kupika chakula ya mama ntilie!.
Hata mimi na wasiwasi nalo maana hawa jamaa hawapo kama watalii vile wasoma fursa hawa,soon huko Mbugani watajaza mahoteli yao.
 
Aisee ni short term plan ama ni endelevu? Kwahiyo kwa mwezi litafanya safari NNE zenye jumla ya wavimba macho 800... Kwa hesabu za haraka ukiuza kila tiketi kwa bei ya juu ya USD 1500 utapata wastani wa USD 1.2... M... Ambazo ni sawa na 2.5B kwa makisio ya haraka
Bado hapo hawajatoa gharama za kuwaweka Mapilot na other Cabin crew kwenye hotel China mwezi mzima.

Hii biashara ni ngumu sana. Serikali itabidi isubsidies sana.
 
Back
Top Bottom