ATCL kuanza safari kwenda China

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1069861


Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Prof Palamagamba Kabudi amesema shirika la ndege nchini ATCL linatarajia kuanza safari za ndege ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka kwenye jiji la Guangzhou nchini China ili kuchochea biashara na utalii kati ya Tanzania na China.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi ndogo za ubalozi wa China jijini Dodoma Waziri Kabudi anasema Guangzhou ndio kitovu cha biashara baina ya nchi hizi mbili na safari hizo zinatarajiwa kuana kati ya mwezi June na Septemba ambapo pia mwaka ujao wa fedha Tanzania itafungua ubalozi mdogo kwenye jiji hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje ulinzi na usalama Mhe Mussa Azan anasema mataifa ya Tanzania na China yana uhusiano wa kihistoria kwa muda mrefu huku balozi wa china nchini Wang ke akisema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania kwenye mambo mbalimbali ya maendeleo.
 
Safari wanatarajia zitaanza katikati ya jun na September!!!! Hata wao hawana uhakika wa hata mwezi gani wataruka kwenda huko. Watu wanafanyaje bookings wakati haifahamiki ratiba ya safari zao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachina hawana lolote, mafisadi tu na wezi hao

China wanatoa rushwa kwenye nchi za Africa ili kupata kandarasi za ujenzi...

China wanamwaga vitu feki huku Tanzania

Tanzania ni shamba la bibi kuuzia vitu feki

Kwa Nini Tanzania inashindwa kuuza Mahindi na Nguruwe China?

China inaagiza Corns (Mahindi) kutoka Marekani (USA)

Unafiki tu na Mazuzu yanashangilia
 
Wachina wanaita wawekezaji wenye maana kutoka Europe na USA - Why


Eti Watanzania wanaita wawekezaji wa hovyo kutoka China?
 
Back
Top Bottom